Tufahamishe: Uliijuaje JamiiForums? Unawaambia nini wasio wanachama?

Binafsi niliijua kitambo kidogo wakati ikiitwa Jambo Forum...enzi hizo sikuwepo hapa Umatumbini bali nilikuwa mbele hukooo...

Sasa kupata taarifa za nyumbani haswa kisiasa ilikuwa inanilazimu kuingia Jambo na kuangalia yanayojiri humu kama guests.

Enzi hizo kuna watu walikuwa wanadadavua mambo humu hadi unajikuta huna cha kuandika, maana walikuwa wakiweka na vielelezo...

Pia nilikuwa napenda kujiachia na burudani za nyimbo sana sana za Gospel(kulikuwa na real time player hapa ya nyimbo mbalimbali kama Zilipendwa, taarab, Bongo Flavor, Gospel)...

Baadaye nadhani nilijiunga lakini sikuwa mchangiaji kwa wakati huo nikaendelea kuwa njuka hadi nikaja kusahau credentials zangu...

Nilipokuja kuibuka tena ikawa hiyo 2010 na hapo nikajiunga tena...
 
Nilifahamu JF toka mwaka 2008 kwa kujulishwa na college mate wangu ila sikuwahi kuwa member.

Nilikuwa nikipita kama mgeni mara chache nipatapo muda. Ilipotimu mwaka 2009 mwezi may nkajisajili but sikuwah kuchangia chochote toka nlpojiunga.. Hata iyo ID nikaisahau..

Ilipofka mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu ndpo nkajiunga rasmi ili niweze kushiriki mijadala kadha wa kadha humu ihusuyo uchaguzi...
 
nikiwa member mzuri wa fb moja ya matangazo yanayopita kule ni ya jf kuna siku nikaamua kuclick link bikaanza kusoma maswaiba ya wadau ndo nikaswawishika kujiunga, vinginevyo sikujua kama kuna kijiji huku na watu wanaishi, its nice I'll be here now and then. Big up to founders!!
 
Back
Top Bottom