Tufahamishe: Uliijuaje JamiiForums? Unawaambia nini wasio wanachama?

Kuna link ilinileta hapa na wakati wa zeutamu,JF link zililuwa nyingi.
Ila ilinichukua muda mrefu kujiunga na hisi ukiwa mbali na tz kwa
muda una wasiwasi wa kuchangia ukifikiri utakacho andika kime-
pitwa na wakati.
 
  1. Je, kuna mtu alikuambia juu ya JF?
  2. Uliona mtu akisearch?
Binafsi sikuambiwa, sikuwahi kuona mtu yoyote akisearch ila nili google kapersky antivirus katika majibu Jf ilikuwepo na nilipo select nikagundua kuna mambo mengi mazuri.
kwa sasa JF imekuwa zaidi ya dozi ya kutwa mara tatu mpaka wife anadai JF is second wife/ nyumba ndogo
karibu

Sikumbuki!
je kwenye account yako ya Facebook....? napo umesahau?
 
Familia yangu walinijuza, wakati huo nipo chuo 2007. Lakini nikawa natizama post tu kama guest hadi nilipojiunga majuzi
 
Mkuu it is a lovely and interesting topic... ndio naiona leo... Ipo thread sio ya mda mrefu saana (kama miezi mitatu ago) ambayo members walijitokeza kusema hasa why na jinsi gani waliifahamu JF na mimi nikiwa mmoja wao.... Link (kama utakua interested)
 
kupitia Google kuna information nilikuwa nazitafuta nikakumbana JF kama sijasahau ilikuwa issues za General Tyre.
 
Nilikuwa nasoma magazeti ya Raia Mwema kila wiki. Nikaona mara nyingi waandishi wana refer jf nikaamua lazima niitafute. Nilipoifungua nilivutiwa nikawa napitia mara kwa mara hadi nilipoamua kujiunga baada ya uchaguzi. Nilijiunga na jambo forum mwaka 2006 ila sikuwa mchangiaji sana. Baada ya kupotea nikawa nasoma Dar Hotwire!
 
Ni Google Search ktk kutafuta maujanja kila nikitafuta kitu jamii forum inakuwepo, basi kwa vile mie ni great thinker nakiona niungane na walimu wangu ili kushare yale maujanja ya ukweli.
 
ilikuwa kipindi cha sherehe na maonyesho ya miaka hamsini ya uhuru (yaliyokuwa na kauli mbiu "Tumethubutu, tumejaribu, tumeweza") mwaka 2011,nilipokuwa nikifuatilia kipindi kilichorushwa na TBC1 kikiongozwa na Pascal wa PPR (Big up Pascal wa PPR kwa kutupiamo!) ndipo nilisikia Pasco akiuliza swali kwa afisa mmoja wa serikali huku akisema swali hilo aliuliza kwa kwa niaba ya wanachama wa Jamii Forums. Hapo ndipo nilipoanza kutafuta Jamii Forums ni nini? Nilipo google haikunichukua muda kuipata. niliitumia tangu hapo kama guest mpaka Mwaka huu mwezi wa May nilipoamua kujisajili kama mwanachama. Sijajuta kuwa mwanachama. Nadhani wengi hawajui uwepo wa JF, tutawajuzaje? Wewe uliijuaje JF?
 
Mie nilikua natafuta demu,nilivyo google kumsaka mwali!mala hi!si ikatokea jf,basi nikawa mwanachama mpaka leo,but wananitwanga ban za mara kwa mara kichizi msela.
 
Mimi nilialikwa na rafiki yangu ambaye ni member huku. nikashangaa tu nimepata ka-email kananiambia fulani anakualika kujiunga na Jamiiforum..... nikajua tu ananitega, nikajiunga.

Kabla ya hapo nilikuwa msomaji tu na mara nyingi tulikuwa tunaongea sana na huyo rafiki kuhusu JF lakini sikuwa member.

Swali la kizushi kwa Invisible..... huyo rafiki aliyenialika hapa na mimi nikajiunga kuna uwezekano wowote akawa anaijua ID yangu hata kama sijamtajia? Maana siku nyingine nawekaga stori zake huku, huwa hachangii lakini kuna siku nikajishtukia usikute anaijua ID yangu
 
Mimi hata sielewi nilivutiwaje nakujikuta nimekuwa mwana wa JF nakumbuka nilialikwa Sheraton ni email niliyoipata kutoka JamboForums wakisema ni konfamu na mgeni wa heshima alikuwa Waziri Simba kipindi hicho!......

Then hadi leo hila sijui kama wewe unajua JF wanachama wake ni waina gani je JF ni yaaina gani!

Toa maoni yako hapa!
 
Nakumbuka mume wangu alikua akiingia mara nyingi JF kusoma habari za siasa ,na alikua akiniita na kunionyesha michango mbali mbali basi siku moja akaamua kuwa member humu.

Nilitaka kuchangia mada flani ilikua imewekwa na lara 1 sikuweza ndipo nilipogundua ukiwa guest huwezi kuchangia mada. Basi nikalazimika nami kujiregister.

Kiukweli JF ina watu wa aina zote na nimejifunza mengi. Kinachonifurahisha zaidi ni namna members wanavyochangia mada.
 
Back
Top Bottom