Tufahamishe: Uliijuaje JamiiForums? Unawaambia nini wasio wanachama?

niliijua kupitia Zitto Kabwe alikuwa akitoa hoja bungeni 2013 akataja neno jamiiforums fasta nikajikonekti kama kawaida yangu nikijiunga ktk mtandao wowote wa kijamii siwekagi jina halisi basi mpk leo am on in it
 
tigo ndiyo iliyonisaidia kuijua kupitia vichekesho vya shilingi 95 vikanipeleka jf mwaka 2012 ila kujiunga ilikuwa tabu nimekuja kujiunga 2014
 
Mi nilipo kuwa naingia google kuuliza maswali mara nyingi majibu mazuri nilikuwa nayapata jamii forum ndo nikaanza kuisurvey hatimaye kuwa member
 
Mimi nilijua kupitia mkurugenzi Mkuu Wa Jamii forums nilipokutana naye aliongea mambo muhimu sana pia akanitambulisha kuhusu huu mtandao toka siku hiyo nimekuwa member
 
Wakuu habari zenu?

Wakuu hivi ilikuwaje ukaijua jf ,uliisikia wapi au alikuambia nani ,ilikuaje kuaje ukaijua?

kwa upande wangu siku mbuki kabisa ilikuje kuaje nikaijua.

nakumbuka 2011 ndio nilianza kuijua ,ila nilikuwa msomaji tu.

Nawasilisha
 
Wapendwa salaam!!

Ninaamini kila mmoja wetu aliifahamu JF kwa namna yake. Ukiwa kama miongoni mwa Member wa huu mtandao pendwa wa Jamii Forums Al-maarufu kama JF unaozidi kujizolea sifa lukuki siku hadi siku ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Tafadhali tujulishe ilikuaje hata ukaufahamu huu mtandao na hatimaye kuwa Member rasmi.

Kwa upande wangu ni mwaka 2009 nipo kidato cha tatu. Ni kupitia kwa mwalim wangu aliyehamishiwa shuleni kwetu Fresh from University tulikua ukaribu karibu kiasi cha kuwa kama ndugu. Teacher alikua ni mtu flani hivi deep kwa chochote anachokuelezea pia alikua updated na current issues zinazotrend Ulimwenguni na hata ndani ya Nchi kwa kifupi ni mtu anayefahamu vitu vingi ndicho kitu kilinifanya kuwa karibu naye.

Tukiwa nyumbani kwake siku moja aliingia kuoga akiwa ameacha Laptop yake sebureni tulipokua tumeketi (Bila shaka alijisahau). Ndipo nilipopata fursa ya pekee kuchungulia ilikua mara ya kwanza kabisa kuona Jamii Forum kwakweli nilivutiwa sana nikanogewa kusoma habari mbalimbali hadi Teacher akanikuta alinifoka sana na kuniuliza nimeona nini sikujibu chochote (Nadhani alikua na wasiwasi na ID yake). Basi kuanzia hapo nikawa naingia kila ninapopata Access ya kuniwezesha kuingia mtandaoni na nilidumu kuwa msomaji (Guest) mpaka pale nilipoamua kujiunga kuwa Member Rasmi 2014 na kwa hakika najivunia kuwa mwanachama Nguli wa JF.

Tujuzane hapa ilikuaje ukaifaham Jamii Forums.Karibuni.
 
Nmeijua kupitia Google nlipokua natafuta maswali mbalimbali na hadithi
It was late 2013
Bdae nikawa busy kdg na issue zangu ad mwaka huu nkaamua kujiunga
 
niliifahamu JF kwa kuambiwa uwepo wake na msera wangu mmoja ambaye ni mtandawazi sana kuliko mimi. Nilikuwa nikimrushia mada tofauti za kuhitaji uwajibikaji na uzalendo, lakini siku moja akaniaambia mada zako ni nzuri sana, lakini tunazifikia wachache kwa sms unazotuma. hebu panua wigo, nenda kwenye mitandao ya kijamii kama face book na jamii foramu.

nilipoanza kuhudhuria huku, JF palinivutia sana, kwani unaweza hata ukamlipua boss wako bila yeye mwenyewe kujua nani katoa taarifa zake kwenye mitandao.

naipenda sana JF
Kwa hyo ulipokuja huku mada hizo nzuri uliziacha wapi.. mbona unaandikaga upupu tu huku
 
Niliiona tu playstore nikaidownload sasa nimekuwa Addicted nayo balaaa...mpaka najuta kuijuaa...
 
Back
Top Bottom