CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Ushirika wa Chadema, Christian Democratic Union, Konrad Adenauer Stiftung na David McAllister.
Nimesoma na kufuatilia mjadala kuhusu alichokisema Bwana David McAllister kwenye kikao cha Kamati ya Masuala ya Nje ya Bunge la Ulaya. Kuna machache ya kuyafahamu kwa undani kidogo.
Wakati Tundu Lissu anaondoka nchini alisema, “mimi sio mkimbizi naenda kuendeleza harakati za kisiasa. Nilichobadili ni uwanja wa mapambano tu”. Tusisahau hili. Mapambano dhidi ya nchi yetu na utafutaji dola yanaendelea.
CHADEMA kama ilivyo kwa Chama cha Umoja wa Demokrasia wa Kikristo (Christian Democratic Union - Ujerumani) ni mwanachama kamili wa International Democratic Union (IDU). CDU na CHADEMA ni washirika wa karibu kisiasa.
IDU ilianzishwa mwaka 1983 na Konrad Adenauer Foundation pamoja na George H. Bush. CHADEMA ni mshirika (Partner) wa Konrad Adenauer Stiftung hapa Tanzania tangu mwaka 2004.
Bwana David McAllister ni mjumbe wa Konrad Adenauer Stiftung. Pia, David McAllister ambaye ndie mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Nje ya Bunge la Ulaya ni Makamu Mwenyekiti wa IDU tangu mwaka 2014.
Kamati ya Masuala ya Nje anayoingoza David McAllister ndio imeleta hoja kuhusu Tanzania na baadhi ya wajumbe wake kutoa maoni yao.
Tufahamu zaidi kwamba David McAllister alikuwa ni Mwenyekiti wa Christian Democratic Union - Lower Saxony mpaka mwaka 2016. Ni mwanachama wa CDU mpaka sasa.
CHADEMA ni mwanachama kamili (Full Member) wa IDU hivyo ana haki zote ndani ya IDU ikiwa ni pamoja na kusukumwa kwa maslahi yake kwenye vyombo ambavyo IDU inauwakilishi. Bunge la Ulaya ni mojawapo ya vyombo hivyo.
Hivyo basi, tunapaswa kufahamu kwamba vita na harakati za CHADEMA zinaendelea na mbinu wanazotumia ni kushawishi kwa kadri wanavyoweza kuhakikisha tunawekewa vikwazo ili malengo yao yafikiwe. Lengo lao kuu ni kushika dola hivyo watafanya kila wawezalo kudhoofisha serikali iliyopo madarakani.
Mh. Rais ameliona hili mapema na ndio maana amemteua Prof Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje haraka kupambana na propaganda na shutuma zinazoelekezwa kwetu.
Ni wajibu wetu kuhakikisha tunashinda vita hii. Tusipoteze mwelekeo. Na sisi tupambane kwa levels za huko huko walipo