Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,442
Nilipokuwa shule (ya msingi) tulikuwa tunakumbana na maswali yanayondikwa kwa namna tofauti tofauti, mfano unaweza kuulizwa kuwa "Kokotoa mzingo wa mduara iwapo kipenyo chake ni mita mbili". Lakini vile vile unaweza kuulizwa kuwa "Tafuta mzingo wa mduara iwapo kipenyo chake ni mita mbili." Kuanzia huko nilikuwa najua kuwa "Kukokotoa" maana yake kwa kiingereza ni "Calculate" Utakuta maswali yale yaliyokuwa yakihamishwa kutoka vitabu vya hesabu (hisabati) vilivyokuwa vikitolewa na Oxford University Press kama vile Highway Mathematics Book 8 au Entebbe Mathematics Book 1 na kuwekwa katika lugha ya kiswahili yalikuwa yanatumia sana neno kokotoa. Baada ya miaka hiyo sijawahai kuhanganika tena na neno hilo mpaka hivi majuzi kilipotokea kililo cha Kikokotoo!
Sasa wajuzi wa kiswahili naomba tusaidiane maswali matatu tu: (1) Je ni kweli kuwa neno Kokotoa maana yake ni Calculate? (2) Iwapo imani hiyo ni sahihi, je Kikotoo, kwa vile hiyo ni noun, maana yake ni kile kifaa au kimashini kinachoitwa Calculator?, yaani kikokotoo cha kukokotolea mahesabu mbailmbali (3) Iwapo tafasiri hii ya Calculator ni sahihihi je kumekuwa na matumizi mabaya ya neno Kikokotoo kwenye media siku hizi?
Kwa maoni yangu, malumbano yote yaliyokuwa yakiendelea kuhusu kikokotoo cha mafao yanaonyesha kuwa yalihusu formula ya kukuotolea mafao hayo, yaani kanuni za kukokota mafao au fomyula ya kukokota mafao, siyo kile kimashini kinachotumiwa kukokotoa mahesabu.
Je nina maoni sahihi?