Tufahamishane magonjwa mbalimbali katika lugha ya kiswahili na kiingereza

Mr Kiroboto

JF-Expert Member
May 3, 2008
350
87
heshima mbele wakuu,

AIDS=UKIMWI
CHICKENPOX=TETEKUWANGA


NA MAGONJWA YAFUATAYO YANAITWAJE KWA KIINGEREZA?

(1)KIPANDA USO
(2)PEPOPUNDA
 
Mzee unataka kwenda kuwapiga bondeni mitishamba ya kitz nini?...Nasikia waganga wa kibongo huko bondeni wanakubalika......!tehe tehe....
 
Mzee unataka kwenda kuwapiga bondeni mitishamba ya kitz nini?...Nasikia waganga wa kibongo huko bondeni wanakubalika......!tehe tehe....

siyo kweli mkuu,lengo ni kuelimishana tu,maana tuna magonjwa mengi sana tunayasikia kwa kiswahili tu kiingereza chake hatukijuhi na kuna mengine tunasikia kwa kiingereza tu kiswahili chake hatukijuhi.Najua magonjwa mengi hayana maneno ya kiswahili,lakini itabidi tuelimishane yale yanayowezekana
 
Acne =kipele
tetanus=pepopunda
tapeworm=tegu
whooping cough=kifaduro
jigger=funza
leprosy=ukoma
rabies=kichaa cha mbwa
measles=surua
scabies=upele/ukurutu
plague=tauni
gland/swollen=mtoki
hookworm=safura
kama bado una taka zaidi tell me.
 
Acne =kipele
tetanus=pepopunda
tapeworm=tegu
whooping cough=kifaduro
jigger=funza
leprosy=ukoma
rabies=kichaa cha mbwa
measles=surua
scabies=upele/ukurutu
plague=tauni
gland/swollen=mtoki
hookworm=safura
kama bado una taka zaidi tell me.

you mean taeniasis ni Tegu?
funza ni ugonjwa au?
 
tape worm ni tegu, funza ni ugonjwa ndio.
Kuna baadhi ya watu haswa vijijini utakuta wanaingiwa na funza kwenye vidole au miguuni. hivyo ni ugonjwa nao.
 
measles=ukambi

na haya nayo yanaitwaje kwa kiingereza
(1)mkamba
(2)matumbwitumwi
 
Back
Top Bottom