Tufafanue tunachokitaka kwa usahihi, pengine Washika Mpini watatuelewa na kutekeleza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufafanue tunachokitaka kwa usahihi, pengine Washika Mpini watatuelewa na kutekeleza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUJITEGEMEE, Nov 24, 2010.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Nimesoma gazeti moja litokalo kila wiki leo (Mwanahalisi-ukurasa wa pili). Gazeti hilo pamoja na mambo mengine limeeleza madai ambayo yameorodheshwa na Viongozi wa CHADEMA katika kikao kilichofanyika Dar-es-Salaam Jumamosi iliyopita.Madai hayo wanataka yatekelezwe ndani ya miaka miwili. Madai hayo ni:
  1.Kuandikwa kwa katiba Mpya(serikali iandae mchakato kwa kupatikana Katiba mpya),
  2.Serkali iunde upya Tume ya uchaguzi(Tume itakayo kuwa huru), na
  3.Serikali ikubali kuunda tume huru ya kuchunguza wizi wa kura.

  Kwangu madai hayo ni ya msingi na yanatakiwa kutekelezwa kwa maendeleo ya demokrasia nchini na jamii ya watanzania kwa ujumla. Ninachoshauri CHADEMA waeleze kinagaubaga jinsi madai hayo yatavyotekelezwa ili baadaye serikali isije ikayateleza inavyojua yenyewe malalamiko yakaanza upya. Au kama CHADEMA wameisha yatoa maelezo hayo basi na sisi wananchi ambao hatujayaona tunayaomba tuweze kujiridhisha.
   
Loading...