Tuepukane na mtazamo hasi dhidi ya UKAWA kwa mtazamo wa UKAWA kukibeba chama fulani

mendz

Senior Member
Dec 9, 2013
144
49
UKAWA ni lulu na itaendelea kua lulu kwa wale wote wanaotaka mabadiliko hapa Tanzania mpaka pale CCM itakapong'olewa rasmi madarakani.

UKAWA imewezesha kufuta doa la udini na ukabila lililopandikizwa na CCM dhidi ya wapinzani ili kuwagawa na kuwadhoofisha katika juhudi zao za kuleta demokrasia ya kweli hapa Tanzania.

UKAWA imewezesha ufanisi katika zoezi zima la kuzisimamia kura na kuzilinda wakati wa uchaguzi huu kwani kila chama kilichounda UKAWA kilikuwa na Wakala wake ndani ya chumba cha kupigia kura na hivyo kufanya zoezi la kupenyeza kura feki au kuhonga mawakala wa upinzani kuwa gumu.

UKAWA imewapa matumaini Wazanzibari ya kupata uhuru kamili wa taifa lao na hivyo kuwaunganisha bila kujali vyama vyao ndani ya nchi yao na kukipigia kura CUF kwa wingi na kuzilinda kura zao kiasi cha CCM kushindwa kabisa kuchakachua kura za Wazanzibari.

Ushindi wa CUF Zanzibar ambao unasubiriwa kutangazwa tu kwa sasa utaongeza nguvu sana UKAWA kwenye mapambano dhidi ya kudai katiba mpya kwani CUF watakuwa wakifanya hivyo wakiwa wameshika hatamu Zanzibar na hivyo kuongeza nguvu ya wapinzani Tanganyika kwa ujumla wao katika mapambano ya kudai katiba mpya na demokrasia ya kweli ndani ya Tanzania.

UKAWA imewawezesha viongozi mahiri wanaotengwa na CCM kupata platform ya kuendeleza harakati zao za kisiasa nje ya CCM na hivyo kuongeza demokrasia na ushindani ndani ya Tanzania.

Ni kwa sababu ya UKAWA tunashuhudia mwaka huu wabunge wengi wa upinzania kutoka pembe zote za Tanzania wakiingia bungeni na hivyo kuwawezesha wapinzani kuwa na nguvu kubwa bungeni katika bunge lijalo.

UKAWA imeiwezesha CHADEMA kwenda Ikulu mwaka huu kama zoezi la CCM la kuchakachua kura likidhibitiwa na kuiwezesha CHADEMA kupata wabunge sehemu ambazo ingekuwa shida kwa wao kuzipata bila support ya muungano wa UKAWA. Nakumbuka kabla ya UKAWA Watanzania waligawanyika mno kwenye mtazamo wa kidini na kikabila uliorutubishwa na mikakati ya CCM ambao ulikuwa wazi ukiangalia uchangiaji wa hoja za kisiasa kwenye mitandao ya kijamii kama hapa JF, Facebook, n.k. Lakini UKAWA iliposimamisha wagombea wa coalition hali hii ilipotea kabisa kwenye mitandao ya kijamii na Watanzania wakaungana katika harakati ya kudai mabadiliko chini ya mwamvuli wa UKAWA.


Sababu za umuhimu wa UKAWA kwa mustakabali wa nchi yetu ni nyingi. Hizi ni chache tu.

Hivyo ni maadui wa demokraia ya kweli na maendeleo ya Tanzania tu ndio ambao watajenga mtazamo hasi kuhusu UKAWA kwa kutumia matokeo yanayojiri kwa sasa kwa kudai UKAWA imekibeba chama fulani badala ya kuona umuhimu wa UKAWA kwa ujumla wake katika uchaguzi huu.
 
Back
Top Bottom