Humphrey Polepole
Member
- Nov 15, 2010
- 19
- 230
Naendelea kuwasisitiza watanzania wenzangu, jitahidini kusoma Rasimu ya Katiba Toleo la Pili, nasema hivi kwasababu ili muweze kuona tofauti kati ya Rasimu na Katiba inyopendekezwa ni lazima uijue Rasimu, fuatilia Bunge Maalum na uje uione Katiba inayopendekezwa. Kama hujui Rasimu huwezi kujua kama Mjadala katika Bunge Maalum unavuruga Rasimu au unaboresha Rasimu. Timiza wajibu wako. Mimi natimiza wajibu wangu kwa kuendelea kuwafahamisha yaliyomo katika Rasimu na kuendelea kufafanua yale yanayopotoshwa hivi sasa.
Wiki hii Jumatano Tarehe 20 Agosti Saa 3 usiku nitakuwa Channel 10 na nitafafanua Masuala ya Mchakato wa Katiba (Hapa tulipo), Muundo wa Muungano kama ulivyo kwenye Rasimu, Kwanini Serikali za Mitaa hazijawekwa kwa kina katika Rasimu, utaratibu wa kuwapata viongozi na watumishi katika Rasimu. Nitazungumzia pia suala la Uraia Pacha. USIKOSE
Jumatano Agosti 20 kuanzia saa 6-8 nitakuwa Kikaangoni LIVE ya East Africa Television. Fuatilia ukurasa wao wa facebook nitakuwa huko kujibu maswali yenu na kutoa ufafanuzi. USIKOSE
Alhamisi Agosti 21 Katika Gazeti la RAI, nimefafanua kwa kina juu ya masuala ambayo yamekuwa yakipotoshwa ama kwa kutokujua ama kwa makusudi. Makala hiyo imejikita katika hoja ya Katiba mpya: tupuuze hadaa tusimamie ukweli,
Wanaosema rasimu inapendekeza serikali 2 wamepotea au wanapotosha makusudi. USIKOSE
Niwasihi tena na tena, Kazi ya kulijenga Taifa katika Mchakato huu si lelemama, inapasa tusome, tuelewe na tushiriki na zaidi tuendelee kujadiliana na kutafuta maarifa huku tukilifuatilia kwa ukaribu Bunge Maalum la Katiba.
Asanteni