Tuendako sitting allowance za waheshimiwa nazo sijui kama zitasalimika

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,917
Hiki kikombe cha ukata cha awamu hii ninahakika kitamgusa kila mtu na huko tuendako hata sitting allowance za waheshimiwa zinaweza kufutwa,kupunguzwa au kuwekewa mashariti mapya kwa lengo la kujikongoja ili mradi tu tufike ingawa sijui kama kweli tutafika.

Wakati wa mzee wa Msoga tulikuwa tunakimbia lakini alipoingia mzee wa Chito pumzi ikaanza kupungua na hivyo tukaanza kutroti walau tufike na sasa pumzi inakata tunaanza kujikongoja na sijui kama tutafika na kama tukifika sijui tutakuwa na hali gani zaidi ya kuwa mahututi.

Haihitaji "ramli" ya mganga wa kienyeji kulijua hili wala "darabuni" ya mwanasayansi kuiona hali hili.
 
Hiki kikombe cha ukata cha awamu hii ninahakika kitamgusa kila mtu na huko tuendako hata sitting allowance za waheshimiwa zinaweza kufutwa, kupunguzwa au kuwekewa mashariti mapya ya namna ya kuwalipa kwa lengo la kujikongoja mradi tu tufike ingawa sijui kama kweli tutafika.

Wakati wa mzee wa Msoga tulikuwa tunakimbia lakini alipoingia mzee wa Chito pumzi ikaanza kupungua na hivyo tukaanza kutroti walau tufike na sasa pumzi inakata tunaanza kujikongoja na sijui kama tutafika na kama tukifika sijui tutakuwa na hali gani zaidi ya kuwa mahututi.

Haihitaji "ramli" ya mganga wa kienyeji kulijua hili wala "darabuni" ya mwanasayansi kuiona hali hili.
Impeachment defence/fear itawa save!
 
Hivi bado wanalipwa? Kwa kazi gani na mshahara wanapata? Tena naomba zifutwe haraka sana.posho ya makalio haina maana kwa sababu per diem wanapata + salary.
 
Uzuri wa wabunge wetu koooooooooote kila chama kitakuwa na lwake lakini linapokuja suala la posho; wee!!

Mwakajuzi ile cjui! NIliwahi kuwashauri CHADEMA kwamba watanie tu kwamba wanapinga possho kwa nguvu zote... tena wakomae kweli kweli lakini wasiwe na hofu; posho zitaendelea tu manake Wabunge wa CCM ni wengi na hawawezi kukubali kwamba posho ziondelewe! Kwahiyo itakuwa wamewatanguliza CCM kibra na wataonekana kwamba ndio wapenda posho lakini mwisho wa siku; mkwanja upo pale pale!!
 
Hivi bado wanalipwa? Kwa kazi gani na mshahara wanapata? Tena naomba zifutwe haraka sana.posho ya makalio haina maana kwa sababu per diem wanapata + salary.
Leo watabana hapa,kesho watabana kule,n.k lakini mwisho wa siku watakuwa hawana pengine pa kubana zaidi ya kuwageukia wao.
 
Back
Top Bottom