Lowassa anaisubiri hukumu ya Kikwete
Absalom Kibanda
MANENO rahisi yalitushinda wanahabari. Haya si mengine, bali yale yaliyotokana na utafiti wa siku mbili uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Vyombo takriban vyote vya habari viliukwepa mtego rahisi wa REDET ilioutega na ambao kwa bahati mbaya ukanasuliwa na wao wenyewe - watafiti hao.
Ni bahati mbaya kwamba, REDET taasisi ya kisomi, ikitumia ujuzi wa shule, iliamua kwa makusudi kumungunya maneno na ikakiuka misingi ya awali ya utafiti wake.
Kwa bahati njema, baadhi yetu tuliweza kuubaini mtego wa kumungunya maneno wa REDET kwa sababu, gazeti hili wiki kadhaa kabla ya matokeo ya utafiti huo kutangazwa, liliandika taarifa kuhusu jambo hilo.
Ni ajabu kwamba, kile ambacho gazeti hili ilikiandika kuwa sehemu ya maswali yaliyokuwa katika hojaji hiyo ya REDET, hakikuonekana katika majibu yaliyotangazwa wiki iliyopita.
Moja ya maswali katika hojaji hiyo ya REDET ilisomeka; Kama Rais Kikwete angeamua leo kubadilisha baraza lake la mawaziri, ni waziri yupi usingependa ateuliwe tena katika serikali?
Katika kipengele hiki, watu waliohojiwa na REDET walitakiwa kutaja jina la waziri au baadhi ya mawaziri wasiostahili kuwemo kwenye baraza jipya litakaloundwa na Kikwete, ambalo kila mtu anayefikiri sawa sawa amekuwa akilisubiri kwa hamu.
Baadhi yetu tulipopata taarifa kuwa utafiti ule ulikuwa umekamilika na matokeo kutangazwa, kikubwa tulichokiangalia kilikuwa ni waziri gani (mawaziri gani) alikuwa amechangia kuiangusha serikali (kwa mtazamo wa wananchi).
Kwa sababu ambazo binafsi sizijui, REDET hawakuweka bayana majibu ya kipengele hiki muhimu na badala yake wakaishia tu kutamka kwamba, Rais Kikwete alikuwa amelipiku baraza lake la mawaziri kwa kukubalika.
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, hata sisi wanahabari kwa sababu ambazo bado zisielewi, tuliingia katika mtego wa matokeo hayo ya REDET na tukasalimu amri kwa kuyatii na kuyaona yakiwa yamekamilika. Katika hili tumefichwa kitu muhimu.
Pamoja na kutambua na kukubali kuwa kazi iliyofanywa na REDET pamoja na kufinyangwafinyangwa imetoa matokeo yenye mwelekeo stahili, binafsi nayaona matokeo hayo kuwa yaliyotolewa yakificha taarifa nyeti iliyopaswa kuwekwa hadharani kwa maslahi ya taifa hili.
Baadhi yetu tunaamini kuwa, matarajio ya matokeo ya hojaji hiyo ya REDET, yalipaswa kukamilika kwa kututhibitishia iwapo yale yanayoandikwa na tunayosikia kuhusu akina Edward Lowassa, Zakia Meghji, Nazir Karamagi, Andrew Chenge na mawaziri wengine wengi, yamepenya vichwa vya wananchi na kuathiri muonekano wao katika jamii.
Kwangu mimi taarifa hizo zingesaidia kujua athari za sifa na tuhuma wanazomwagiwa mawaziri wetu kupitia katika vyombo vya habari, ambavyo mara kadhaa viongozi hao hao wamekuwa wakivinyoshea vidole kwa kuripoti masuala ya kubuni.
Pamoja na udhaifu huo wa REDET ambao unaweza ukawa ni wa makusudi (si wa bahati mbaya), bado tunaamini kuwa matokeo yake yatakuwa changamoto muhimu katika mabadiliko makubwa yajayo.
Haihitaji kuwa na akili za ziada kutambua kuwa, matokeo ya REDET yanayomuweka Kabwe Zitto, mbunge wa upinzani katika nafasi ya pili kwa kukubalika katika utendaji wake wa kazi akivuna asilimia 10 dhidi ya asilimia 30 ya Rais Kikwete akimchukua Waziri Mkuu aliyepata 5.8% ni ya kuifedhehesha serikali na chama tawala.
Ni jambo lisilohitaji elimu ya chuo kikuu kuyaona matokeo yanayoonyesha kuporomoka kwa umaarufu wa Rais Amani Karume Zanzibar kutoka asilimia 47.8 za mwaka jana hadi kufikia 35.5% za sasa kuwa huenda yanahusiana na hali tete ya kisiasa ya huko visiwani na kuporomoka kwa utendaji wa serikali yake.
Kama hiyo haitoshi, habari kwamba, Rais Kikwete aliyevuna asilimia 80 ya kura zote katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na mwaka mmoja baadaye kura ya maoni ikamuona akikubalika kwa asilimia 67 kabla ya sasa kufikia asilimia 44 ni mbaya na isiyopaswa kuachwa ikaendelea kubakia ilivyo.
Lakini pengine jambo baya na la lazima kufanyiwa kazi na Kikwete mwenyewe, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali kwa ujumla, ni lile linaloonyesha kuwa rais wetu anapendwa na watu wenye elimu ndogo zaidi kuliko wale waliosoma vyema.
Ni jambo la hatari na fedheha kwamba, rais wetu anaungwa mkono zaidi na watu wasiosoma shule kabisa na wale wenye elimu ya msingi kuliko ilivyo kwa watu wenye elimu ya sekondari na walioelimika zaidi ya hapo.
Watanzania tunapaswa kuikataa fedheha hii ya wajinga kutuchagulia viongozi na aibu ya kiongozi wetu mkuu kutoungwa mkono na wasomi wetu.
Ni kwa sababu ya kujua hatari hiyo ambayo sasa imethibitishwa na REDET, ndiyo maana miezi takriban miwili iliyopita, kupitia safu hii hii, nilipata kumtahadharisha rais wangu kuhusu tukio la kuanguka kwake machoni mwa wapigakura.
Katika makala hiyo, nilimtahadharisha rais kuwa macho na wanaounda baraza lake la mawaziri ambao sifa kubwa inayowatia nguvu ya kuendelea kujiona wakistahili kushiriki katika ufalme wa Kikwete si rekodi zao za utendaji, ukada wenye utii na wa mfano kwa chama chao, mchango wao kwa maendeleo ya taifa, uadilifu na umakini walionao katika kazi, bali ushirika wao na Jakaya zama zile kabla hajawa mkuu wa nchi.
Katika moja ya aya za makala hiyo, niliandika maneno yafuatayo; Katika mazingira ya kusikitisha, miongoni mwao hawa, ndiyo wale wale ambao, uamuzi wa Kikwete kuwapa nafasi za uteuzi katika baraza lake la kwanza la mawaziri wakiwa mawaziri kamili au manaibu, leo hii unawaweka katika kundi la watu ambao hawana hata jambo moja la wazi unaloweza kusema wanajivunia katika utendaji wao wa kazi.
Pasipo kutafuna maneno, hawa ndio waliomuangusha Kikwete. Hawa ndio waliowasaliti Watanzania. Hawa ndio wale ambao baada ya kupewa dhamana ya kuwatumikia wananchi, wameshindwa kuitambua dhamana hiyo na kuiona kuwa ni wajibu mzito mabegani mwao, uliokuwa ukihitaji uchapakazi usiomithilika, uadilifu usio na shaka na visheni yenye kujenga misingi imara ya kuliondoa taifa hili kutoka katika msongamano wa matatizo yanayojenga usugu kila kukicha. Hawa ndio ambao Kikwete anapaswa kuwangoa.
Sikuishia hapo, niliandika bayana kwamba, miezi takriban 22 (wakati huo) tangu Rais Jakaya aingie madarakani mawaziri na manaibu wa namna hii, ndio waliosababisha yeye rais na Waziri Mkuu wake, Edward Lowassa wageuke wao ndio wasemaji na watendaji wa kila kitu kikubwa serikalini hata katika masuala ambayo yalipaswa kuamuliwa katika ngazi za wizara.
Leo hii hayo si maneno ya magazeti kama walivyozoea kutuambia wasaidizi wakuu wa Kikwete na Lowassa, bali ni kilio cha wananchi wengi waliohojiwa na REDET.
Binafsi naamini kwamba, iwapo REDET wangepata ujasiri wa kuyataja majina ya mawaziri ambao wamekataliwa na wananchi katika kura ya maoni iliyoendeshwa nchi nzima, leo hii mambo yangekuwa magumu kweli kweli serikalini.
Hata hivyo, pamoja na udhaifu katika ripoti hiyo ya REDET, ukweli unabakia pale pale kwamba Baraza la Mawaziri la Kikwete limepwaya, umaarufu wa rais mwenyewe umeporomoka na imani ambayo wananchi waliijenga miaka miwili iliyopita imeendelea kupotea.
Kwa kutambua uhalisia huo usiopingika, Kikwete anapaswa kufanya jambo moja tu, kugeuka nyuma na kusikiliza wasia wa Nyerere na kuchukua maamuzi magumu ilimradi tu yawe ni kwa maslahi ya taifa.
Katika kufanya hivyo, anapaswa kuanza na Waziri Mkuu Lowassa. Ampime kwa vigezo vya kiutekelezaji, kimaamuzi na kimaadili na ampe hukumu anayostahili. Kama atajiridhisha kwa moyo wake wote kwamba amekuwa msaada mkubwa kwake katika maeneo hayo matatu aendelee kumpa fursa ya kuwaongoza mawaziri na kusimamia utendaji serikalini.
Katika kulitekeleza hili, anapaswa kutogeuka nyuma na kuangalia upacha wao kisiasa tangu walipokutana miaka ya mwanzo ya 1970, wakajaribu kwa pamoja mwaka 1995, wakapanda ngazi pamoja serikalini na wakashirikiana tena kwa ajili ya mwaka 2005. Huko kutakuwa ni kuwasaliti Watanzania milioni tisa na ushee waliompa kura za ndiyo.
Katika hili anatakiwa kumpa Lowassa hukumu anayostahili. Anawajibika ama kumlinda kwa mema au kumwadhibu kwa makosa. Katika hili haitaji kuwa vuguvugu. Analazimika kuwa ama moto au baridi. Analazimika kusuka au kunyoa.
Atakapokuwa amemalizana na Lowassa, ageukie kwa mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wa wilaya. Kazi itakuwa rahisi kabisa, hakuna atakayekuwa na ubavu wa kusema lolote kwani watajua kwa uhakika kabisa kuwa umeamua kwa haki. Huko ndiko tuendako.