Tuelimishane namna ya kupokea/ kutoa taarifa za msiba za mtu umpendaye zaidi

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,900
2,000
Wakuu,

Suala la kutoa taarifa zinazohusiana na msiba wapo watu wanaojua kufikisha taarifa hizo ila watu wengi hawajui namna ya kumpa mtu taarifa za msiba.

Kuna watu wanatoaga taarifa za msiba kwa ghafla, bila huruma. Utasikia 'flani kafa'. dahh! Wakati mwingine huweza kusababisha mstuko kwa mpokeaji.

Mtaua mnaowapa taarifa jamani punguzeni makali kidogo.

Tuelimishane
 
mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,900
2,000
modes rekebisheni kichwa cha habari nilimaanisha umpendaye
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,848
2,000
Wakuu kuna watu wnatoaga taarifa kwa gafla, bila huruma.

Utasikia flani kafa.
dahh !!!
mtaua mnaowapa taarifa jamani punguzeni makali kidogo
Kwani hata ukimficha na baadae ukaja kumwambia ukweli wote yule Marehemu atafufuka? Acheni uswahili Mtu akifa kama upo karibu na Ndugu yake au Rafiki yale au hata Mwanafamilia wake ni ' Kufunguka ' tu moja kwa moja Kwake kwamba ' amefiwa ' full stop. Hizi tabia za ' Kipuuzi ' tulizonazo Waswahili ndiyo zimetufikisha hapa Waswahili hadi tunaonekana ni wa ' hovyo hovyo '. Mbona Mtu anaposhinda ' Bingo ' ya ' Mipesa ' kibao huwa hatumzungushi katika kumwambia ukweli? Tena usiombe Mimi nikawa Rafiki yako au Nduguyo kwani nikipata tu taarifa kwamba umefiwa natiririka na naserereka nayo Kwako hivyo hivyo bila kuichelewesha wala kuipunguza makali.
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,852
2,000
Sawa tutapunguza... Tutatumia maneno kama Fulani hatunaye, Ametutoka, ameaga dunia, Mungu kamuita' n.k
 
mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,900
2,000
Kwani hata ukimficha na baadae ukaja kumwambia ukweli wote yule Marehemu atafufuka? Acheni uswahili Mtu akifa kama upo karibu na Ndugu yake au Rafiki yale au hata Mwanafamilia wake ni ' Kufunguka ' tu moja kwa moja Kwake kwamba ' amefiwa ' full stop. Hizi tabia za ' Kipuuzi ' tulizonazo Waswahili ndiyo zimetufikisha hapa Waswahili hadi tunaonekana ni wa ' hovyo hovyo '. Mbona Mtu anaposhinda ' Bingo ' ya ' Mipesa ' kibao huwa hatumzungushi katika kumwambia ukweli? Tena usiombe Mimi nikawa Rafiki yako au Nduguyo kwani nikipata tu taarifa kwamba umefiwa natiririka na naserereka nayo Kwako hivyo hivyo bila kuichelewesha wala kuipunguza makali.
mkuu utaua nakwambia
mfano mtu kafiwa na mamake
unamfata na kumwambia
mamako kafa? utazimisha mwingine wewe
 
Mbassa jr

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,030
2,000
Unamfuta mfiwa unampa za kihenga 'ndgu yangu kufa kufaana na alokufa kafa...ndugu yangu mwenzio kafa. Ful stop!
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,848
2,000
mkuu utaua nakwambia
mfano mtu kafiwa na mamake
unamfata na kumwambia
mamako kafa? utazimisha mwingine wewe
Mkuu Mimi huwa ' nanyoosha ' tu na hiyo ndiyo desturi yangu na sitoibadilisha hadi naingia Kaburini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom