Tuelimishane kuhusu jela na ufungwa maana inaelekea wengi hawajui

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Mwaka 2015 Umoja wa mataifa uliridhia masharti (rules) 122 kuhusu jela na ufungwa. Masharti hayo yalipewa jina la MASHARTI YA MANDELA (MANDELA RULES).

Ni kweli masharti haya yalilenga kulinda haki za wafungwa wa aina mbalilmbali: watoto, wazee, wanawake, wanasiasa, wakimbizi, mahabusu, walio kizuizini, wagonjwa, n.k.

Kwa leo tutizame sharti la kwanza kabisa (Mandela Rule 1).

Linakataza manyanyaso,ukatili, mateso, na udhalilishaji dhidi ya mfungwa. Lakini mwisho wa kanuni hii inasema hivi; 'the safety and security of prisoners, staff, service providers and visitors shall be ensured at all times'.

Tafsiri ni kuwa ili mfungwa afaidi Mandela Rule 1 huyo mfungwa au jamaa zake asitende au kunena au kuonyesha hisia au ishara itayoadhiri uhai na usalama wa mfungwa mwenzake, watumishi wa gereza, watoa huduma wa gereza, na wageni wa gereza.

Haya sio maneno au kanuni yangu au ya serikali au ya CCM! Ni kanuni ya Umoja wa mataifa ambayo inasimamia na kamisheni ya haki za binadamu (UN Human Rights Commission).

Mbowe anadai kuna watu watawajibika ICC! Ni vyema akajua ICC itatizama hii kanuni ikiwa itaona kuna haja ya kufanya hivyo Yaani ICC haiwezi kuchunguza tukio la ufungwa ambalo halina mashiko kwa mujibu wa hizi MANDELA RULES!

Sasa swali la kujiuliza ni hili: waliokwenda kumpokea au tuseme kumchukua mfungwa walitenda au kunena au kuashiria wangehatarisha uhai na usalama wa wafungwa, watumishi wa gereza, watoa huduma wa gereza au wageni wengine wa gereza siku na muda husika?

Wenye gereza wanasema ni kweli walitenda haya yote! Na wanadai ushahidi wanao na wanaandaa mashitaka wawafikishe wahusika mahakamani.

Mbowe yeye anadai kama askari magereza waliotimiza wajibu wao kwa mujibu wa hii Kanuni Namba 1 ya Mandela (Mandela Rule 1) ataenda kushitaki ICC na eti mpaka mkuu wa nchi atafika ICC kujibu mashitaka!

Jamani kusoma kuna faida somesheni watoto wasije kufanya vichekesho ukubwani!

Ni kanuni hii itawahukumu wahusika Kisutu! Askari magereza walitekeleza Mandela Rule 1. Waliopigwa walivunja hii kanuni waziwazi!
 
Kaka umeongea Mandela Rule 1 ukatuaminisha sheria unazijua sana. Hiyo ni sehemu ndogo katika sheria zinazotumika ICC.
 
Africa jela ni mateso na unyanyasaji,,,haki za mfungwa na haki za binadamu ni ULAYA,,,kufungwa ulaya ni zaidi ya maisha ya nje ya MTU huru Africa JELA ULAYA NI SAWA .NA HOTEL....ulaya wao wanakunyima Uhuru wako lakini wanakupa kila kitu na pesa unapewa,,huku kwetu wafungwa wanalimishwa mashamba mshahara mi ugali mbichi na maharage...AFRICA NI NANI ALIYETUROGA?Africa hakuna haki za binadamu...na ukiingia CORONA huko magerezani ni MSIBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Africa jela ni mateso na unyanyasaji,,,haki za mfungwa na haki za binadamu ni ULAYA,,,kufungwa ulaya ni zaidi ya maisha ya nje ya MTU huru Africa JELA ULAYA NI SAWA .NA HOTEL....ulaya wao wanakunyima Uhuru wako lakini wanakupa kila kitu na pesa unapewa,,huku kwetu wafungwa wanalimishwa mashamba mshahara mi ugali mbichi na maharage...AFRICA NI NANI ALIYETUROGA?Africa hakuna haki za binadamu...na ukiingia CORONA huko magerezani ni MSIBA

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna jela za brazil huko au kongo na UN wapo niaka yote wamepiga kimya wanakula tu posho
 
Back
Top Bottom