Tuelimishane kuhusu gsm,cdma, hd, hdtv, ig,2g,3g,4g | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuelimishane kuhusu gsm,cdma, hd, hdtv, ig,2g,3g,4g

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Jan 20, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jana kulikuwa na thread watu unapeana ufahamu wa mambo mbali mbali kuhusu misamiati. niliyotaja hapo juu

  Nimeamua kufungua uzi tuelimishane tukosoane kistaarabu kwa lugha nyepesi ili tuelewe. Wataalam na wasio wataalam karibu mueleze uelewa wenu. tuosme kwenye google na tutumie uelewa wetu tufundishane

  • Tofauti za kiteknoloji CDMA na GSM ni nini?TTeknolojia gani kinadharia ina uwezo mkubwa .

  • Tofauti iliyopo kati ya Huduma za 2G na 3G na 4G katika simu ni nini? Sifa hasa za 3G ni nini?

  • Huduma gani zinatakiwa kupatikana kwenye 3G ambazo kwenye 2G hazipo na je ni sehemu gani duniani kuna huduma za 4G?

  • Mtu mwenye Iphone 4G tanzania anafaidika nini na simu yake kwa provider wa tanzania tofauti na mtu mwenye simu za 3G
  Pia kuna Issue ya HD. Tunaeleweshane nini maana ya neno HD?

  Nawasilisha
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hiyo Ni HD
   
 3. j

  jerry monny Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Great,thanks alot.u realy meant a great thinker.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  thanks
   
 5. Ncha ya Upanga

  Ncha ya Upanga Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDMA inasimama badala ya code division multiple access.
  Kwenye teknolojia ya CDMA mawasiliano kati ya watumiaji wa simu na kitovu cha kuunganisha mawasiliano(Mobile switching center) zinatofautishwa kwa kutumia codes badala ya kutumia frequecy au time channel yaani kitaalamu FDMA naTDMA. Hivyo kuondoa uwezekano wa kutokea muingiliano wa mawasiliano au Interference kitaalam

  Hizi FDMA na TDMA nazo ni miongoni mwa teknolojia zinazotumika kwenye GSM(global system for mobile communication), ambapo kila mtumiaji anapewa kiportion katika frequency au time iliyopo hivyo kama channel ya frequency ikiisha baadhi ya watumiaji inabidi wasubiri mpaka users wengine waachie frequency.  CDMA inauwezo mkubwa dhidi ya GSMkwa sababu ina reserve bandwidth kubwa kutokana na kutumia code katika channel ya frequecy au time iliyopo, hivyo kuwezesha ku accomodate users wengi. Na pia kuwezesha transmission ya data au internet connection kuwa ya kasi zaidi.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu umetumia lugha ya kitekenolojia sana naamini wengi hawatakuelewa lakini vile vile nadhani umefanya makosa kusema CDMA ni teknolojia ndani ya ya GSM. Ninavyoelewa na nilivyosoma mimi GSM inatumia TDMA kwa simu na FDMA kwa minara.

  GSM ni teknolojia iko huru kutumika wakati teknolojia ya CDMA inahodhiwa na kampuni ya Qualcom USA.kampuni au mashirka ya kutengeza vifaa kutumia CDMA inabidi wawalipe kiasia fulani hawa Qualcom.Miaka ya nyuma Nokia walikuwa na Kesi na hawa jamaa kuhusu hii issue ya kuhodhi teknlojia.

  KIfupi CDMA na GSM ni teknolojia mbili tofauti. Utakuwa na simu/ modem iliyotengenezwa specific kwa ajili ya CDMA au GSM tu. Hakuna modem au simu inaweza kutumia teknolojia zote mbili.

  Kwakutumia mfano rahisi tofauti ya GSM ambayo inatumia TDMA na CDMA amabayo sometime inatumia majina kama EVDO ni huu
  Pia GSM technlogy inatumia kuna simcard wakati CDMA techology inatumia internal Memory.(ie. hakuna simcard) Hii ndio sabbau utaona hata uchakachuaji wa modem za CDMA ni mgumu sana wakati kuchakachua modem za GSM sio kazi sana.

  Huyu jamaaa kwenye mjadala uliopita aliweka video clip nzuri yenye maelezo ya G's kwenye simu


  Maelezo mengine rahisi kuhusu hizimaana ya hizi kwenye simu waweza yasoma hapa [FONT=&quot]http://technology.globalthoughtz.com/index.php/understanding-the-gs-in-telecom-networks-1g2g3g4g5g-explained/

  [/FONT]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ncha ya Upanga

  Ncha ya Upanga Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu mtazamaji, nimerekebisha mistari yangu ili nieleweke vizuri, thanks anyway
   
 8. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  1.Tofauti za kiteknoloji CDMA na GSM ni nini?TTeknolojia gani kinadharia ina uwezo mkubwa .
  - Tofauti yake ni jinsi ya kufikisha mawasiliano CDMA hutumia code na GSM hutumia frequency. (Mfano wa CDMA ni kama mna wazungumzaji sita na wasikilizaji kibao sasa hapa wazungumzaji wote watazungumza kwa pamoja ila kwa kutumia lugha tofauti hivyo basi kila msikilizaji atamsikiliza yule lugha anayoielewa ILA kwny GSM ni kwamba kila mzungumzajia atapewa mda wake wa kuongea kwa kupokezana)

  - Kwa kweli hakuna ushahidi wa kititaalamu ni ipi nzuri zaidi ila kwa mtizamo wangu CDMA ni best kwenye data na security. GSM ni nzuri kwenye voice(simu) na pia inahuduma za ziadi nyingi zaidi(Vallue Add Service (VAS)). Kampuni ya ZANTEL inatumia teknolojia zote mbili(Voice ni GSM na Data ni CDMA)
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani hapo powa kabisa kamanda

  Pia nimeona kuwa EVDO (Evolution Data Only)ni enhencment ya teknology ya CDMA. Kwahiyo modem za EVDo zinatumia teknology ya CDMA na kwajina la kitalaamu zinaitwa CDMA2000. Soma hapa http://www.wisegeek.com/what-is-evdo.htm na hapa http://en.wikipedia.org/wiki/EVDO

  Sasa swali Je kwa Tanzania ni provider gani wanatoa huduma zao kwa teknolojia ya CDMA na ni wapi wanatoa Huduma zao kwa teknolojia ya GSM.?
   
 10. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  2.Tofauti iliyopo kati ya Huduma za 2G na 3G na 4G katika simu ni nini? Sifa hasa za 3G ni nini?
  - Tofauti yake kubwa ni data rate(uwezo wa upitisha data kwa haraka) 2G ni maarufu kwa GPRS, 3G inauwezo wa datarate hadi 6.2Mbps

  3.Huduma gani zinatakiwa kupatikana kwenye 3G ambazo kwenye 2G hazipo na je ni sehemu gani duniani kuna huduma za 4G?
  - mfano ni video call , 4G(superfast) inapatikana Norway and Sweden etc ila si nchi nyingi wanayo

  4.Mtu mwenye Iphone 4G tanzania anafaidika nini na simu yake kwa provider wa tanzania tofauti na mtu mwenye simu za 3G
  - Mimi kama mtaalamu wa VAS(Value Add Service) sioni kwasababu hatuna mtandao wa 4G maana hata hii 3G kampuni nyingine ndio wanaupgrade sasa hivi. Kumbuka hizi latest technology kuzitumia ni ghali sana hata kule China wanatumia bado 2G

  -Mdau na wakilisha -
   
 11. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante mkuu Mtazamaji,
  Hapa TZ kampuni ya ZANTEL wanatoa huduma kwa CDMA upande wa data na GSM kwa upande wa Voice, ila hata CDMA yao unaweza kupigia simu kama kawa ila mtandao wao wa CDMA uko tu sehemu za miji kwa huku bara. Tena wanazo modemu za CDMA zinatoka nduki kweli.

  Vodacom, Zain(Airtel) na Tigo wana2mia GSM tu.
  TTCL mobile wao wanatumia CDMA, pia SASATEL na bila kusahau kampuni ya Benson online iko opp na French Embbassy wata2mia CDMA tu
   
 12. Njaa

  Njaa JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 60
  Asante kwa maelezo mazuri, lakini si kweli kuwa CDMA hazina sim cards, simcards zipo na ZANTEL wanauza, simu na moderm ambazo zinatumia simcard za CDMA nyingi tu siku hizi. Ila nilikuwa sijui scientific differences
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuuu powa nadhani umeeleza vizuri kabisa .sasa swali na hoja nzuri niliyona mjadala wa nyuma ni :-
  kama mitandao yetu ya tanzania ya simu inasema inatumia 3G kwa nini wateja hawawezi kudowload katika kasi ya 6.2Mbs hata pale wanapokuwa karibu na mnara na hawako kwenye movement. Je inawezekana bado wanatumia 2G au 2.5

  na kama ulivyosema kweli ni gharama naamin hata Provider wa Tanzania wanatumia 2G au 2.5.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  1 G Maana yake ni First Generation Mobile networks ( Mfano AMPS, TACS, NORDIC na kadhaa)

  Sifa zake

  - Analogy Teknolojia
  - Haikuwa Cellular Technology
  - Multiple Access technology iliyotumika ni Frequency Division Multiple Access ( FDMA) yaani kila Mtu anapewa frequency yake katika kipindi chote cha call na hakua Sharing of frequency
  - Transmission Power ilikuwa kubwa sana kwa maana Mji mzima ulitegemea Mnara mmoja kucover ( Kama FM Radio)
  - Modulation technique ni Frequency Modulation
  - txt Msg was not possible with this with this technology

  Nitaendelea na 2G
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ok basi Desa nilisoma limenipotosha . ndio uzuri wa forum. kweli somtime theory za kwenye vitabu zinaweza kuwa tofauti na kitu kinachowezekana practically. Inawezekan pia Desa nilisoma ni la mwaka 2008 na teknolojia inabadilika kila kukicha.

  Thanks for updating my understanding
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  jamani katika Huu Mjadala inabidi tutofautishe baina ya Maneno Haya mawili

  1: Standard; 1G, 2 G, 3 g , 4 G ni Standard zilizowekwa na ITU ( Shirika la mawasiliano la dunia)
  2: Technology;FDMA, TDMA, CDMA ni technology upon which the above Standards are Built
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuna Mapungufu Mengi yaliyomo kwenye First Generation Network yaliyopelekea mashirika mbali mbali kuandaa mchakata wa Kuwa na Second Generation network (2G)

  1: matumizi yasiyo ya Faida ya Masafa
  2: muingiliano wa Mitandanao ( Interoperability) Maana kila nchi ilikuwa na Standards zake Ambazo zilikuwa haziingiliani na Nyingine

  Pamoja na Nyingine nying, Shirika la mawasiliano la Dunia likaweka Specifications za 2G networks. Lengo la ITU lilikuwa ni kuwepo na Standard Moja tu lakini Hilo halikuwezekana kwa maana kulikuwa na Standards zaidi ya tatu za 2G

  Nazo ni:

  A: GSM ( Global System for Mobile Communications)

  Sifa zake:

  1: Ilikuwa na digital Communication
  2: Teknoljia iliyotumika ni TDMA
  3: Short txt was possible
  4: Sharing of frequency in time basis was possble
  5: Due to its Cellular nature, Frequency Re-use was possile, yaani Frequency iliyotumika manzese inaweza kutumika tena Buguruni na hii iliongeza capacity ya Network

  B: PDC ( Pacific Gidital cellular)

  Sifa zake

  1: Digital
  2; Technolojia: TDMA
  3: Haikupata Umaarufu sana na ilikuwa sana Japan


  C: IS=95 Interim Standard

  Technolojia : CDMA
  Digital

  Ilipata Umaarufu sana Marekani

  D: IS-136 Interim Standard 136

  1: digital
  2: teknlojia: TDMA
  3: Ilikuwa Maarufu huko Marekani

  Ndugu zangu hizo ni Standards ambazo zipo katika 2G netwrks
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ukiangalia Vizuri Katika maelezo yangu ya 2G, Kuna Standads 4 ( Nne) lakini zimejikita katika Teknolojia Mbili TDMA na CDMA, GSM, PDC na IS-136 zilitumia TDMA wakati IS-95 ( CDMA one) zilitumia CDMA

  technolojia ya Mawasiliano ya Cellular Imekuwa sana na Imeekuwa na Wateja wameongezeka sana Lakini MASAFA HAYAJAONGEZEKA. Kutokana na Hitaji kubwa la Masafa Shirika La Kimataifa la Mawasiliano (ITU) Liliamua kuweka Vigezo vivya kwa ajili ya 3G Network na Moja ya kigezo ni Kwamba Standard Zote Lazima zitumie teknolojia ya CDMA. Lengo la ITU likiwa ni kuwa na Standard Moja tu, lakini haikuwezekana maana yaliibuka Makundi makuu mawili, nayo ni:

  1: 3GPP, hili liliundwa na Standard zilizokuwa zinafauata GSM, PDC na IS-136, hawa Jamaa walikuna 3G Standard yao Iliyotwa UMTS au WCDMA

  Sifa zake:

  Teknolojia: CDMA
  Backward Compatible with GSM, ndiyo Maana Vodacom, zain na hata Tigo wamadopt hii Standar
  High Data rate

  2: 3GPP2 , Hili limeundwa na IS-96, Group hili limekuja nz Standard iitwayo CDMA 2000, CDMA 2000 EV-DO nk

  Hii ni Standard ambayo kwetu wanayo Zantel, TTCL, Dovotel nk

  Sifa zake

  Teknojia: CDMA  Sammary: Kwa hiyo ndugu zangu katika Three G (3G) Teknolojia inayotumika ni CDMA kwa Hiyo its Miss leading kusema kwamba Vodacom hawana CDMA.
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  4 G! Hii inaitwa LTE yaani Long Term Evolution, hii nadhani bado inafanyiwa test hata huko marekani bado hawajalaunch, kwa jina Lingine wanaita Mobile Broadband Service

  Hii itakuwa na Dowload speed inayofikia 150MBps

  Tuendelee kueleimishana
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nakubaliana katika Mengine ila Hapo Kwenye red hapana, Vodacom, Zain na Tigo Wameshalauch WCDMA network yao ambayo na yenyewe inatumia Technolojia ya CDMA
   
Loading...