Tuelezane uzuri, ubaya, faida na hasara za utumiaji wa 'Vumbi la Mkongo'

Nikweli kabisa mkuu mimi nadhani watu hawafikirii adha na kejeli tunazokutana nazo kwa hawa wake zetu..
Just imagine umeoa then tangu uoe mwanamke hajawahi kufurahia mchezo unafikiri aibu gani unapata...
Aaa aaaaa aaaa, Mkuu @Bwanamisitu pole sana, unatia huruma yaani nakuona vile unavyopata maumivu moyoni, pole mtu wangu. Nilikua nasoma tuu comment na kupita ila niliposoma hii comment ya kwako nimehuzinika sana.

Ngoja tupeana ushauri kidogo, kabla sijakwambia kitu gani ufanye; ngoja nijaribu kuweka ama kuuliza masuala yatakayosaidia kufahamu kiini cha tatizo lako. Utajijibu kimoyomoyo mwenyewe huko.

Jiangalie kama tatizo lako liko la kitabia, yaani uliwahi kujihusisha kupiga puu ama kujichua siku za nyuma kabla ya kuoa? Kama ni hivyo maana yake tatizo lako ni la kisaikolojia na kimwili hivyo utadeal nalo katika kujibiidiisha kuachana na hiyo tabia kama bado unayo na kuweka fiti kwa mazoezi ya mwili jumla na mazoezi ya kuukanda uume ili uindoe ulegevu wake na hatimae kuwa imara wakati wa kufanya tendo. Aidha, unatakiwa kula vyema na kupumzika vya kutosha. Ondoa wasiwasi na wahaka wakati ukijiandaa katika kufanya mapenzi na mwenzio.

Hapa panapo kula vizuri nataka nikutajie walau aina fulani fulani za vyakula ambavyo mm binafsi huwa natumia kama chakula na sio kama dawa, (yaani nakula kiasi kidogo kila siku) lozi ama almound, aina hii ya njugu imefanyiwa utafiti sana na watafiti duniani na imegundukllika kuwa huwa inaweka sawa na kuimarisha uimara wa mbegu za kiume na kumfanya mtumiaji awe na "sexual stamina" ambapo humuwezesha awe muamuzi wa muda gani anataka kuwaruhusu wagiriki kushuka.

Kwa utafiti wanapendekeza ule kiasi cha kigao kimoja cha mkono, yaani walau upate punje za lozi 10 hadi 15 kwa siku kwa matokeo mazuri. Kwa sababu sijajiandaa sitaweka rejea za hizi tafiti kwa sasa. Naweka tuu hii link unaweza kujisomea kidogo, kama unataka kusoma tafiti za kisayansi unaweza ukagoogle zipo za kutosha huko mjtandaoni. Naamini utafanikiwa inshaalah.

Eating a handful of almonds daily can reduce belly fat, waist circumference, leg fat and improve a man's sperm count and quality..

Chakula chengine ni mronge, ule mti wenye vijani vidogovidogo ambao huwa unakuwa mkubwa kiasi. Huu nitajuwekea faida zake tu maana unatumika katika namna tofautitofauti.

Wengine hutumia kama mboga, chai na tunda zake huliwa, mm binafsi nilkshawahi kutumia kwa kunywa chai ya majani ya mronge na wakati mwengine huwa najikuta natafuna zile mbegu zake na kunywa na maji yabkutosha kama masihara tuu na si kwa lengo hasa ya kurudisha hamasa ya tendo ila faida huiyona baada ya muda mdogo sana.

Nenda kajifunze kuhusiana na matumizi mazuri ya mronge katika kuimarisha afya ya uzazi kwa mwanaume.

Jichunguze kama tatizo lako linasababishwa na shida za kijini ama mapepo, ukijijua uko hivyo jitafutie tiba haraka kupitia mrengo wa imani yako, maana haya mapepo yanachangia kwa kiasi kikubwa binaadamu kuharibikiwa katika mambo yake ya kimapenzi.

Pole sana mtu wangu, Mungu yuko pamoja nasi. Tusikate tamaa na maisha ya duniani, Mungu katuwekea starehe ile ili tutulize nafsi na miili yetu kupitia viumbe wenzetu wa kike nao kutuliza hisia zao kupitia sisi, sasa inapofika wakati ikiwa mwanaume ama mwanamke hapati kitulizo cha aina ile binafai huwa napata huzuni sana. Maana ndio starehe pekee ambayo maskini na matajiri hupata namna moja ya utamu kutegemeana na jinsi utavyojitahidi kuweka sanaa utakayo.

Ooohhhhh pole sana mtu wangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya mazoezi dogo, hili vumbi la mkongo la siku hizi limeshaingiliwa na wahuni kwani wengi wanachanganya na kinyesi cha binadamu au wanyama pori, matokeo yake inakuvunja nguvu za kiume...shauri yako. Fanya mazoezi kwa bidii upate nguvu na kuweka mwili sawa.
 
Aaa aaaaa aaaa, Mkuu @Bwanamisitu pole sana, unatia huruma yaani nakuona vile unavyopata maumivu moyoni, pole mtu wangu. Nilikua nasoma tuu comment na kupita ila niliposoma hii comment ya kwako nimehuzinika sana...
Dah kwanza naomba nikushukuru sana kiongozi wangu kwa kuguswa na hii changamoto yangu, hii inaonyesha ni namna gani ambavyo wanaume tunathaminiana.

Ndugu kwa %90 nimekuelewa na nimeelewa ushauri wako na ninaahidi nitaufanyia kazi inshaAllah pajapo majaaliwa baada ya mfungo nitaanza kila jambo ambalo baadhi ya wadau humu wamenishauri kupitia uzi huu.

Naamini hakuna lishindindikanalo chini ya hili jua isipokuwa muda na saa tu ikifika kila jambo linathibitika.

Kaka nimekuelewa sana na asante sana na nakuahidi kufanya maandalizi katika haya yote uliyonishauri..

Ikipita miezi kadhaa nitarudi kukushukuru ndugu yangu na kukupa mrejesho wa nilipofikia ila umenitia moyo sana asante sana kwa kuguswa na hii changamoto yangu ndugu..

Allah! Azidi kukujaalia kheri na kukuzidishia fadhira, Kila la kheri brother..
 
Fanya mazoezi dogo, hili vumbi la mkongo la siku hizi limeshaingiliwa na wahuni kwani wengi wanachanganya na kinyesi cha binadamu au wanyama pori, matokeo yake inakuvunja nguvu za kiume na kuwa shoga....shauri yako. Fanya mazoezi kwa bidii upate nguvu na kuweka mwili sawa.
Ni kweli mkuu, Wala sikupingi katika hili hii idea ya kutumia hilo jambo nimeshaweka kapuni siwezi kujaribu

Asante kwa kunifahamisha, nashukuru sana Kaka mkubwa.
 
Ni kweli yote yanawezekana mkuu ila ninaimani this time nita improve, mmejitahidi kunipa shauri tofauti naamini nitazifanyia kazi. Matokeo nitayaona nasubiri mfungo upite nianze taratibu zote.
Unapokuwa kwenye gemu...usiirembe sana..maana wewe hisia zako zipo karibu... ..bandua..mapema mapema...sio unaitazamaa...mpaka jamaa..anasizi!

Timing na kichwani tu..jikaze hapo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una miaka mingapi tangu uanze kulitumia na ufanisi wake ukoje! Kuna comment tofauti watu wanasema hawawezi kurudia kulitumia, sijui halina ishu, mara hakuna utamu, mara hii mara vile.

Wew unasemaje kwa uzoefu wako labda..
Acha ujinga na kutisha watu wewe. Vumbi la congo bei ni 5000 hadi 10000. Unajua bei ya gram 1 ya cocaine au heroine wewe? Yani mtu achanganye madawa hayo halafu still uuziwe bei rahisi. Vumbi linafanya kazi ila wengi hatujui madhara yake (potelea mbali)
N.B: mtumiaji mzoefu wa vumbi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa anayehitaji vumbi anitumie no. ake PM then tufanye biashara, kama upo dsm ntakupa kidogo bure ukaijaribu
 
Wakuu habarini.

Nina omba kufahamishwa madhara yatokanayo na kutumia vumbi, madhara ya muda mrefu na yanayojitokeza ndani ya muda mfupi. Niko njia panda wakuu, nahitaji niagize mzigoo hapa kwa mwana mmoja aniletee. Sasa nahitaji nifahamishwe haya madhara nisije nikatumia halfu badae kazi inaharibikaa.

Msaada tafadhari.

Asanteni mabibi na mabwana ,nawasilishaa


its yooo boy yULEboy 001 katika ujenzi wa Tz ya viwanda..
 
Back
Top Bottom