KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,600
Nimetafakari sana kwa chama hiki ambacho kinajiita chama chenye sera mbadala ambacho ni CHADEMA na kugundua kuwa chama hiki kimekosa agenda na sasa kinaelekea kupoteza dira kwa watanzania. Katika kutafakari kwangu nikapata majibu haya mawili: La kwanza, CHADEMA hakina pumzi ya kusimama yenyewe mbele ya CCM na la pili, CHADEMA hakina uwezo wa kuongoza unaofikiriwa kuwa nao( uwezo wake wote unatokana na CCM au vyama vya vingine na huu ndio ukweli ila mchungu).
Kabla ya utawala wa Rais Magufuli, kulikuwa na kauli mitaani kuwa CHADEMA hakina agenda sikujua ukweli wa kauli hiyo mpaka Rais Magufuli alipoingia madarakani. Sikuelewa mapema kwa nini, mitaani ambapo watu wa kawaida kabisa wanaishi kufikia hatua ya kusema CHADEMA hakina agenda lakini sasa ninaelewa vizuri sana.
Nikikumbuka CHADEMA ya dkt. Slaa ilivyojimbanua kwa mapambano ya Rushwa na ufisadi lakini CHADEMA ya dkt. Mashinji ikijipambanua kwa kutetea yaliyokuwa yanapingwa na kupiganiwa na dkt. Slaa. Hii ndio sababu watu mitaani kusema CHADEMA hawana agenda na ushuhuda ni leo agenda kubwa ya mapambano ya ufisadi na rushwa ya CHADEMA imewekwa pembeni na kuanza kushughulika na mambo madogomadogo ambayo hayana hata umuhimu kwa nchi na wakiacha mambo ya msingi.
Kuna kauli Rais Magufuli alizitoa kama jiwe na kichaa. Hizi ni kauli kwa hakika nilitegemea zingechukuliwa kama kauli za utani na alitumia kukazia alichosema lakini leo upinzani unatumia kauli hizo kama agenda na mbaya Zaidi hata wabunge wao wanatumia kauli hizo kama agenda. Huku ni kukosa agenda na kupoteza dira. Nilitegemea kauli za maendeleo na kujenga nchi kutoka kinywani mwa Rais zikatumiwa na wapinzani kama agenda lakini matokeo yake zile kauli za utani ndio agenda zao.
Nikimnukuu maneno aliyosema Rais siku hiyo aliyesema jiwe’ Na ninataka muamini watanzania mna Rais wa kwelikweli, ni jiwe kwelikweli. Sitishwi wala sitishiki. Mimi jikumu langu kwa ajili ya watanzania, ni kuhahakikisha ninawavunsha watanzania kutoka mahali pa shida mpka pa raha’. Ni aibu sana nukuu kama hiyo ikiwa imebeba matarajio makubwa ya Rais lakini CHADEMA wanaamua kutoka sehemu ya utani kama agenda. Ni aibu
Mwanafalsafa Socrates aliwahi kusema’ strong minds discuss ideas, average minds discuss events and weak minds discuss people’, kwa tafasiri Nyepesi ’ akili kubwa hujadili mawazo, akili ya wastani hujadili matukio na akili ndogo hujadili watu’. Watanzania sasa wameanza kujadili vitu vidogovidogo na vya kawaida tu. Kujadili kauli kama “jiwe”, “kichaa”, “kiongozi wa malaika”, n.k ni sawa na kujadili watu na hiyo ni sifa ya akili ndogo. Kauli kama hizo zichukuliwe kama utani tu. Kuendelea kujadili kauli kama hizo ni kukosa agenda na kupoteza dira.