Tuelekeako na Chadema - Tutafika tu but the price is high. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuelekeako na Chadema - Tutafika tu but the price is high.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 12, 2011.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema wanatupeleka ile sehemu ambayo kila Mtanzania atakuwa anajua anaelewa kuna nini ndani ya nchi yake na kinachotaka kifanywe ni kitu gani ,ujumbe ambao Chadema wameufikisha si mdogo ni mkubwa sana ,naamini kabisa kuwa hivi sasa Ndani ya Taifa hili na pia nje ya mipaka yake watu wanauelewa mkubwa juu ya mabadiliko na mwamko wa kisiasa walionao WaTanzania.

  Chadema kwa kutumia mitego na njia ambazo Chama tawala CCM na Serikali yake wanashindwa kuitambua ,CCM na Serikali yake wamenasa katika mtego wa Chadema ambao umegharimu maisha ya WaTanzania ,faida iliyopatikana ni kubwa sana na ndio chimbuko ya mambo ambayo yatakuja mbeleni kwa urahisi kabisa,tayari imeshajulikana kuwa utawala uliopo hauendeshi nchi kibinadamu ni unyama unyama tu ,hiyo ni faida kwa WaTanzania wapenda maendeleo na nchi yao ,walio ndani na wale waliopo nje.

  Njia kama hizi ambazo Chadema imeanza kutumia ni njia za kubeba majukumu na viongozi nilazima wajue hivyo na ni lazima wawe wakiwaeleza wananchi kuwa panapopiganiwa haki na usawa ni lazima kutatokea patashika kwani sio rahisi kumpokonya mtu tonge inayoelekea mdomoni ,ni mapambano hivyo katika mapambano hayo maisha ya watu pia yanaweza kupotea na isichukuliwe kuwa Chama kinapendelea hivyo ila ni njia ambayo ni lazima tuipite ili kuiweka sawa Taifa hili la Tanzania, na pia watawala waliopo madarakani hawapo tayari kuachia utawala kwa wengine kwa njia za uadilifu hivyo njia za kupita ili kukabiliana nao zitacost even life kama nilivyosema.

  Tukubalianeni tu kuwa njia ambazo Chadema inatupitisha ni njia zisizokuwa na tatizo katika kulikomboa Taifa hili na mkoloni mweusi.
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani chama tawala ni Chadema?
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Dalili za Mvua ni Mawingu
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ni wewe au kuna mtu kachukua password yako
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  If the price is high try the cheapest.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nimempa thanks with my reservation! Akianza yale mambo yake naifuta
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mwiba Umeongea
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hii njia chadema wanayotupitsha lazima tupite tutake tusitake la sivyo tutaibiwa mpaka nguo zetu za ndani
  karibuni nchi zote za africa zimepitia hii route na hata nchi nyingi za ulaya kabla ya kuheshimiana zimepitia hii route
  hata cuf na maalim znz wamepitia hii route ila kosa alilolifanya maalim ni kukubali serikali ya umoja wa kitaifa, maalim alizani ccm watakubali wakishindwa kwa ajili ya serikali ya umoja wa kitaifa kumbe ccm hawawezi kuachia ngazi bila msukumo
  clearly seif alishinda uchaguzi na angekuwa hajakubali serikali ya umoja wa kitaifa inamaanisha ingekuwa patashika, sasa hivi yuko kimya sana
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Miaka nenda miaka rundi tumekuwa tunalishwa hiyo kasumba ya kisiwa cha amani, matokeo yake nchi yetu imegeuzwa shamba la bibi. Hatudanganyiki tena, amani na utulivu wa kweli haupatikani bila ya kuwepo haki.
   
 10. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapa ni lazima tukubaliane kuto kukubaliana. Ni ukweli ulio wazi ukombozi wa wanyonge upatikana kwa shida,tabu na mateso ni lazima machozi, jasho na damu vimwagike historia hipo wazi kuhusu suala hilo. Njia wanayotupitisha CHADEMA kuelekea ukombozi ni ngumu kuipita kama wewe si mpambanaji wa ukweli. Ukiamua kuifuata CDM na kuiunga mkono ktk mapambano ya ukombozi wa nchi kutoka ktk mikono ya wakoloni weusi na MAFISADI ni lazima ujikane nafsi yako na uwe tayari kwa mapambano. Kama CCM kuachia UMEYA wanaua na kujeruhi je Kuachia IKULU (Urais) itakuwaje?

  Tuangalia yanayojiri IVORY COAST ( JE JK ametoa kauli ya kulaani hadi leo?), angalia wenzetu kenya, zimbabwe hata Zanzibar (jan 2001 CUF walifanywa nini na serikali ya CCM), hivyo kumtoa mtu madarakani una maanisha utukufu na ubwana mkubwa unakuwa BYE BYE hakuna tena kwenda JAMAICA kubembea, kwenda kwa OBAMA kukutana na BOYZ II MEN, kukaa ndani ya nchi miezi 5 na nje ya nchi miezi 7 kwa mwaka inakuwa historia(utalii wa Jk) hivyo watawala wa aina hii lazima watoe roho za watu kulinda utukufu huo.

  Hivyo njia ya ukombozi si rahisi mfano ni jan 5 ARUSHA kilichotokea ndio kashkash za mapitio ya njia hiyo, Tusiwe wachangiaji wazuri humu JF na kunyoosha vidole kwa wengine, tujiulize je Twaweza pita njia hiyo? je tupo radhi kuipita? je tu tayari kukejeliwa na wakina MALARIA SUGU, KISHONGO, MTU WA PWANI, NGOGO,JEYKEY na wengine wengi? tupo radhi kuitwa wachochezi, wadini, na kufunguliwa mashtaka kila wakati? Je tupo tayari kulaumiwa/kutengwa na familia zetu(baada ya kuongwa na ) kushinikizwa na ccm, je tupo tayari kupoteza kazi au kuwaacha watoto zetu kuwa mayatima na wake zetu kuwa wajane. Hiyo njia ya ukombozi ambayo CDM wanatupitisha na ni UKWELI KABISA KUWA HAKUNA NJIA NYINGINE HILA NJIA HIYO,maana njia zote CCM wameweka vibao vya NJIA HII IMEFUNGWA/NJIA HII HAITUMIKI/HAKUNA NJIA HAPA/URUHUSIWI KUPITA NJIA HII nk. Ndugu zetu wa ARUSHA wamekubali kupita njia hiyo je wewe na mimi tupo tayari kuipita?
  VIVA SLAA, VIVA MBOWE, VIVA MNYIKA, VIVA LEMA, VIVA LISU, VIVA ZITTO,VIVA OWENYA,VIVA NDESA, VIVA MDEE NK.
  ALUTA CONTINUA
   
 11. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa tunaomjua mwiba, nadhani hakuwa amelog-off, mtu mwingine akatumia computer yake
   
 12. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,240
  Likes Received: 1,172
  Trophy Points: 280
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  what do you need to believe that?
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahahaha,mkuu nimejiuliza mara mbili mbili ila sikupata jibu kwa nini kaandika haya,ngoja tuone analenga nini haswa
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hata mimi... maneno yake mazito sana haya leo... sijui kimetokea nini
   
 16. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aliyeweka hii thread ni Rev Masanilo au Mwiba? Naona kama naota.
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mwiba,
  kwa comments ninazozisoma inaonekana ulikuwa unawachoma wengi!
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  ni mwiba huyuhuyu au kivuli?

  au naota?
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  CCM ni sawa na hadisi moja kwenye Biblia. Watu walikuwa wanajenga jumba refu kwenda kwa Aliye Juu.

  Wamefika mahali wamemuudhi Mungu. Kila mtu anaongea kwa lugha yake.

  Hongera Mwiba!!

  Bado Malaria Sugu naye atakuja na yake kama hii
   
 20. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  Huyu mwiba anabusara za kisiasa sana...!
   
Loading...