TUCTA yapinga mpango wa Rais Magufuli kukata malipo ya mishahara

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) limepinga mpango wa Rais John Magufuli wa kukata malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh40 milioni kwa mwezi hadi Sh15 milioni.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Kanda ya Ziwa jijini Mwanza jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya alisema uamuzi huo ni kinyume na sheria na utaligharimu Taifa iwapo wahusika wataamua kwenda mahakamani kupinga mishahara yao kupunguzwa.

“Watendaji hawa hawakujipangia mishahara wao wenyewe, bali malipo haya yalipangwa na bodi za mashirika na taasisi husika ambazo kisheria zimepewa mamlaka hayo. Malipo haya hayawezi kupunguzwa kwa kauli za kisiasa bila kuzingatia mahitaji ya kisheria,” alisema.

“Iwapo Serikali itatekeleza lengo hili bila kuwapo mjadala mpana na makubaliano ya kisheria kati ya wahusika, basi ijiandae kulipa mamilioni ya fedha kama fidia iwapo watakaokatwa mishahara yao watakwenda mahakamani.”

Akiwa mjini Chato wakati wa mapumziko ya wiki moja, Rais Magufuli alitangaza kupunguza mishahara ya juu kutoka Sh40 milioni hadi Sh15 milioni kwa mwezi, akisema wapo watumishi wa umma wanalipwa masilahi manono na kuishi kama wako peponi, huku wanaolipwa Sh300,000 wakiishi kama wako jehanamu.

Kaaya aliishauri Serikali kuendelea kuwalipa mishahara hiyo minono wahusika hadi mwisho wa mikataba yao, ndipo lengo la kuipunguza litekelezwe ama kwa kuwapa wahusika mikataba mipya au kuajiri watu wengine.

“Serikali inaweza kuwa na nia njema kupunguza tofauti kubwa ya mishahara kati ya kada ya juu na chini, lakini utekelezaji wake lazima usubiri muda mwafaka mikataba ya sasa itakapomalizika,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine; Tucta imepinga hatua zinazochukuliwa na baadhi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya ya kutangaza kuwasimamisha kazi watumishi wa umma ambao hawapo chini ya mamlaka zao kinidhamu.
 
Kwanza kwa kawaida Employment andam labour relation act ya mwaka 2004 ,hairuhusu mtu kushushiwa mshahara ,inatakiwa wale walioko chini wapandishiwe ili angalau walingane au waendane na wajuu...
 
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) limepinga mpango wa Rais John Magufuli wa kukata malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh40 milioni kwa mwezi hadi Sh15 milioni.
.

Hawa TUCTA nao wamekurupuka.Kazi yao ni kutetea wanachama wao.Hao wananaowatetea sio wanachama wao .Hakuna mwanachama wa TUCTA anayepokea mshahara hata wa milioni 15!!! pia hao wanaowatetea ni watu wa mikataba huteuliwa na Raisi kwa mikataba ya miaka michache michache KAMA VILE MWAKA MMOJA,MIWILI AU MITATU nk!

TUCTA wahangaikie walio wengi na wawasemee wanachama wao wasiwe DOMOKAYA la kusemea watu wasio wanachama wao.Hivi uchaguzi uko lini wang`olewe viongozi hao wa juu wa TUCTA?
 
Haiwezekani mtu Mmoja alipwe milioni 40 bhana

Kwani alijipangia yeye huo mshahara au alipangiwa na bodi au kamati maalumu yenye mamlaka kisheria? Na naamini pia kulikuwa na washindani wengine, kama aliwashinda basi anastahili kupewa! Ni heri ya huyu anayelipwa nyingi kuliko mafisadi wanaokwapua mabilioni na hawafanywi kitu!
 
kama wao hawakujipangia mishahara basi lazma wapangiwe tena, mbona tucta siwaelewi, raisi hafanyi mambo kwa kukurupuka, aliseme kaagiza mamlaka zinazohusika zipange viwango vya mishahara. yawezekana na nyie tucta mnajilipa mishaharamikubwa. mbona mwaka 2012 raisi alipadilisha mishahara ya wafanyakazi? too late vyombo husika vishakaa kupanga mishahara kw watumishi wa umma na mashirika ya umma, subirini mwezi wa 7, mishshara mipya itakapotangazwa.
 
Kaduguda milioni 40 sio hela ndogo kwa mwezi halafu,wengi wao walipewa ili walinde maslahi ya mtu alie wapa.Unafikiri Rais anavyosema ataipunguza hiyo mishahara haelewi huo mchezo??M 40 kwa kazi gani bhana.
 
Lazima ifyeke tu nyie si ndiyo mnaotumiwa ili kueneza hizo propaganda; TUCTA unafiki mtupu mbona wameshindwa kuwatetea wafanyakazi wa chini kwa miaka yote hiyo, mpuuuuuuuuzi kabisa huyo jamaa haya ndiyo majipu mengine, je ni wafanyakazi wangapi kwenye sector binafisi nchi hii wameajiliwa na wanalipwa kiwango kidogo cha mshahara na hao tucta wanavuta vitambi maofisini tu bila hata kufanya uchunguzi juu ya hilo?

Leo Rais ameliona hilo na kulitolea maamuzi eti
tucta inakuja na porojo za kuwatetea wanaolipwa 30-40 milioni, badala ya kuungana na Rais ili angalau wakatwe ili waongezewe wanaolipwa laki 3 ili angalau uwiano eti tucta nayo inatoa tamko kutokata hiyo mishahara!! maajabu haya kumbe tucta ipo kwa ajili ya walewanaojilimbika mishahara ya 40 milioni, aibu yao tucta.

Rais ameshawaambia kama wakiona hiyo mishahara ni midogo waanze kutafuta kazi zingine mapema!! mbona 15 milion kwa Tanzania bado ni nyingi tuu! waache kwanza mie naona Rais awatumbue tuu na ateuwe wapya wengine.
 
Kwani alijipangia yeye huo mshahara au alipangiwa na bodi au kamati maalumu yenye mamlaka kisheria? Na naamini pia kulikuwa na washindani wengine, kama aliwashinda basi anastahili kupewa! Ni heri ya huyu anayelipwa nyingi kuliko mafisadi wanaokwapua mabilioni na hawafanywi kitu!

hiyo bodi au kamati ndio itakayo mpangia mshahara mpya. labda hukumsikia raisi alisema ameagiza vyombo husika kupanga mishahara upya.
 
TUCTA nao hamnazo! Wanafikiri Rais hajui yote hayo? Sijui kuna sheria sijui act gani inakataza sijui kufanya nini hayo yote yanajulikana. Serikali ikiamua itakachofanya ni kupeleka mswada Bungeni wa kutengua visheria vyote hivyo tena kwa hati ya dharura, utajadiliwa kidharura, utatiwa saini kidharura, na mishahara itapunguzwa. Mbona ni very easy!
 
Lazima ifyeke tu nyie si ndiyo mnaotumiwa ili kueneza hizo propaganda; TUCTA unafiki mtupu mbona wameshindwa kuwatetea wafanyakazi wa chini kwa miaka yote hiyo, mpuuuuuuuuzi kabisa huyo jamaa haya ndiyo majipu mengine, je ni wafanyakazi wangapi kwenye sector binafisi nchi hii wameajiliwa na wanalipwa kiwango kidogo cha mshahara na hao tucta wanavuta vitambi maofisini tu bila hata kufanya uchunguzi juu ya hilo?

Leo Rais ameliona hilo na kulitolea maamuzi eti
tucta inakuja na porojo za kuwatetea wanaolipwa 30-40 milioni, badala ya kuungana na Rais ili angalau wakatwe ili waongezewe wanaolipwa laki 3 ili angalau uwiano eti tucta nayo inatoa tamko kutokata hiyo mishahara!! maajabu haya kumbe tucta ipo kwa ajili ya walewanaojilimbika mishahara ya 40 milioni, aibu yao tucta.

Rais ameshawaambia kama wakiona hiyo mishahara ni midogo waanze kutafuta kazi zingine mapema!! mbona 15 milion kwa Tanzania bado ni nyingi tuu! waache kwanza mie naona Rais awatumbue tuu na ateuwe wapya wengine.

ndg yangu kweli raisi anakazi ya kuibadilisha nchi yetu. yaani tuliotegemea kuwa ni watetezi wa wafanyakazi wamuunge mkono raisi kuondoa tofauti kubwa ya mishaara iliyopo lakini wao wanapinga.
 
Tucta & CWT nacheka sana. In short hawawezi kuzuia mkono wa presidaa hawa. Tuliwahi ambiwa walimu kuwa ambae hawezi kulipwa mshahara wa laki tatu na nusu kima cha chini aache kazi hawa wote walikuwa active and in high peak perfomance na hiyo kauli ilitolewa wakati huyo msemaji akiwa anapata labda mara 1000 zaidi ya hicho kima cha chini kinachoombwa na wafanyakazi wa uma. Sasa jaman kama mgonjwa alifikia hatua ya kushindwa hata kujamba kujisaidia ataweza kweli??
Be serious!!
 
Hivi huyu jamaa bado yupo TUCTA?

TUCTA+MGAYA.JPG
 
Back
Top Bottom