TUCTA yapata mbunge viti Maalum kupitia UWT-CCM

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,292
24,172


Mbunge wa viti maalum kupitia Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania TUCTA TUCTA | Trade Union Congress Of Tanzania baada ya kupitishwa na Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania UWT .

Mbunge huyo Viti Maalum kutoka TUCTA kupitia UWT-CCM mkoa wa Dar es Salaam amesema amepokea kwa furaha jukumu hilo na kupitia vyama zaidi ya 13 vya Wafanyakazi wa Tanzania vinavyounda Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania atafanya kazi kwa kushirikisha na wizara ya kazi na wadau wengine ili kufikisha matamanio ya wafanyakazi katika chombo cha kutunga sheria cha Bunge la Jamhuri ya Muungano ili kutetea haki za wafanyakazi wote Tanzania.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA lina vyama shirikishi chini yake vya waalimu, makuli bandarini n.k listi ya vyama hivyo ni

TUCTA ni shirikisho linaloundwa na vyama 13 vya wafanyakazi lenye wanachama kutoka sekta mbalimbali na vyama hivyo ni:

  1. Tanzania Teachers Union (TTU)
  2. Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers Union (TUICO)
  3. Researchers, Academicians and Allied Workers Union (RAAWU)
  4. Tanzania Local Government Workers Union (TALGWU)
  5. Tanzania Mines and Construction Workers Union (TAMICO)
  6. Tanzania Plantations and Agricultural Workers Union (TPAWU)
  7. Tanzania Railways Workers Union (TRAWU)
  8. Tanzania Union of Government and Health Employees (TUGHE)
  9. Tanzania Seamen’s Union (TASU)
  10. Communication and Transport Workers’ Union of Tanzania (COTWUT)
  11. Conservation,Hotels, Domestic and Allied Workers’ Union (CHODAWU)
  12. Telephone Workers’ Union of Tanzania (TEWUTA)
  13. Dock Workers’ Union of Tanzania (DOWUTA)

Source : TUCTA Affiliates
 
Siwezi kusahau tucta ilivyomtesa JK miaka ya 2012
Mfumo Kristu huo. Wanasubiri aje rais Muislam watoe matamko na vitisho. Makasisi na Maaskofu nao waamke na matamko

Sasa hv vijana wa altareni huwezi kuwasikia.

Kwa maana hiyo TUCTA ni tawi la CCM. Wafanyakazi kuna kila sababu ya kuangalia kama kuna ulazima wa kuwa mwanachama wa vyama vyenye mafungamano na TUCTA
 
kumbe ni jumuiya ya ccm !
Yaani vyama vya wafanyakazi TUICO n.k chini ya mwamvuli wa TUCTA na vyama vinavyounda shirikisho wameamua kuwa sehemu ya mhimili wa watawala na hivyo watashindwa kuwatetea kwa uhuru haki na stahiki za wafanyakazi mfano kikokotoo maana TUCTA imekuwa Jumuiya mojawapo ya CCM kama UVCCM, UWT, WAZAZI n.k
KIKOTOO CHA PENSION: Rais DKT John Mafululi akutana na Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi - TUCTA KIKOTOO CHA PENSION: Rais DKT John Mafululi akutana na Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi - TUCTA
waTanzania na wafanyakazi au vyama vya kitaaluma na wakulima hawajaelewa agano la Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu mfano Maendeleo ya Watu kupitia vyama huru au Mashirikisho huru ya wafanyakazi,makuli, wakulima, wavuvi kuibana serikali iliyopo madarakani ili wapate haki zao.

waTanzania wameamua kuipa CCM Mpya kila kilicho chao cha kupazia sauti wakiwa na imani na fikra potovu kuwa serikali na chama tawala kilichopo madarakani kitaweza kuwainua kupitia hisani . Mfano sakata la kikokotoo na mifuko ya jamii.
 
9 Aug 2018

Chama kipya cha walimu (CHAKAMATWA) chaibuka, chajipanga kuishtaki CWT


Chama cha Kutetea Maslahi ya Walimu (CHAKAMWATA) kimejipanga kufungua kesi mahakamani kutaka viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kueleza mali zao ziko wapi ambazo zilipatikana kutokana na kukatwa fedha zao kiasi cha asilimia 2 ya mshahara kila mwezi.
Source : Azam TV
 
9 Aug 2018

Chama kipya cha walimu (CHAKAMATWA) chaibuka, chajipanga kuishtaki CWT


Chama cha Kutetea Maslahi ya Walimu (CHAKAMWATA) kimejipanga kufungua kesi mahakamani kutaka viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kueleza mali zao ziko wapi ambazo zilipatikana kutokana na kukatwa fedha zao kiasi cha asilimia 2 ya mshahara kila mwezi.
Source : Azam TV

Hii kesi wamefikia wapi?
 
Ndio maana TUCTA walikubali maoni ya kufuta FAO la kujitoa

Kubadili Kikotoo

Watu wanakufa bila mafao yao

Hivi hizo Pesa zinaendaga wapi?

Pesa nyingi mno NSSF wanabaki nazo baada ya watu kufariki...kwa Nini wasisaidie watoto wanaolala barabarani...au Nyumba za yatima au kutoa mikopo elimu ya juu.

Pesa wanapeleka wapi?
 
Huyu ni mbunge wa ccm na sio wafanyakazi
Haiingii akilini eti mbunge mwakilishi wa wafanyakazi anapigiwa kura za kuteuliwa na UWT DSM ambao wengi hata sio wafanyakazi
Na pia katiba za vyama vya wafanyakazi zinaeleza wazi kwamba hakitakuwa na political affiliation
Yaani hili linchi la kikuuma Sana
Vitu vingine haviingii kabisa akilini
Ubunge wa huyu mama ukienda kuwa challanged mahakamani na mahakama ikawa fair ubunge wake unakuwa null and void
Haikubaliki eti mbunge kuwakilisha wafanyakazi apitishwe na UWT na sio TUCTA
Huyu aseme ni mbunge anayewakilisha wafanyakazi ambao ni wana ccm ila sio wafanyakazi wote Tanzania
TUCTA imetumika kisiasa kwenye hili wakati katiba ya TUCTA inaelekeza kabisa kwamba haitajihusisha na mambo ya siasa
 
Kwa maana hii Wafanyakazi wote Tanzania ni wanachama wa Jumuiya mojawapo ya CCM mtake msitake maana TUCTA "imetekwa" hivyo lazima kuitetea CCM Mpya kama wafanyavyo UVCCM.
 
Kwa maana hii Wafanyakazi wote Tanzania ni wanachama wa Jumuiya mojawapo ya CCM mtake msitake maana TUCTA "imetekwa" hivyo lazima kuitetea CCM Mpya kama wafanyavyo UVCCM.
Tena ni jumuiya ya wanawake Tanzania dar es salaam
 
Back
Top Bottom