TUCTA yakaa mguu pande kupinga sheria ya mafao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUCTA yakaa mguu pande kupinga sheria ya mafao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELFU-ONEIR, Jul 31, 2012.

 1. ELFU-ONEIR

  ELFU-ONEIR Senior Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limeandaa maandamano ya amani kupinga mabadiliko ya kupitishwa kwa sheria ya marekebisho ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Maandamano hayo yatafanyika Agosti 4 kuanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi katika Ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholus Mgaya alisema sheria ya mpya ya mifuko ya jamii inaeleza kuwa mfanyakazi mwanachama atakapotokea kuwa ameacha au ameachishwa kazi hawezi kuchukua mafao yake hadi atakapofikisha umri wa kustaafu ambao ni miaka 55 kwa hiari au miaka 60.

  Alisema kuwa mfanyakazi mwanachama wa mfuko wowote wa hifadhi ya jamii, akiacha au akiachishwa kazi akiwa na miaka 35 inabidi asubiri kwa miaka 20 alipwe mafao yake ya uzeeni. “Hiki ndio kipelngele cha sheria ambacho kimeleta taharuki kubwa miongoni mwa wafanyakazi wanachma wa mfuko hiyo,” alisema Mgaya.

  Alisema wanatambua ukweli kuwa malipo ya uzeeni kwa mujibu wa dhana ya mifuko ya hifadhi ya jamii ni kwa ajili ya kumsaidia mwanachama aliyefikia umri wa uzeeni, hata hivyo walishabaini kuwa dhana hiyo ni vigumu kutekelezeka katika nchi yenye uchumi duni kama Tanzania.
  Alisema sababu zinazosababisha ugumu huo ni kutokuwa na uhakika wa ajira, ajira kubwa hapa nchini kuwa mikononi mwa sekta binafsi, na pia mfumo wa hifadhi ya jamii kutokuwa na fao la watu wasiokuwa na ajira.

  Mgaya alisema kutokana na viwazo hivyo, hakuna utaratibu wa hifadhi kwa mwanachama aliyekosa ajira au anayetafuta katika kipindi ambacho ameachishwa kazi na kuhoji kwamba ataishije hadi kufikia miaka 55 kabla ya kupata ajira mahali pengine.

  Alisema maisha ya watu hivi sasa yamezungukwa na mazingira hatarishi yenye magonjwa yasiyotibika, ajali nyingi, majanga ya moto mafuriko mambo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa umri wa kuishi.

  Hata hivyo alisema wanataka kuona mabadiliko ya haraka yafanyike kwenye sheria hiyo ya hifadhi ya jamii ili fao la kujitoa liweze kurejeshwa au uandaliwe utaratibu muafaka utakaohakikisha mwanachama anarejeshewa michango yake na ya mwajiri pamoja na riba mara tu anapokoma uanachama wa mifuko hiyo.

  Alisema Tucta haitasita kuchukua hatua za kisheria endapo mamlaka itaendelea kushikilia msimamo wake wa kubakiza kifungu hicho kinachomtaka mwanachama wa mfuko afikishe miaka 55 ndio alipwe mafao yake.

  Aidha alisema Tucta wamesikitishwa na kushangazwa na kuwahi kutangazwa kwa mabadiliko ya sheria hiyo ya hifadhi ya jamii huku mchakato wake ukiwa bado haujakamilika baada ya kuridhiwa na Rais kama kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kutangaza kwenye gazeti la Serikali.

  Mgaya alisema Tucta inataka mamlaka ya mdhibiti na msimamizi wa mfuko wa hifadhi ya jamii kuchukua jukumu la kutoa elimu kwa wanachama kuhusu sheria hiyo mpya kusaidia kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima.

  Kwa upande wa Tucta Mkoa wa Dar es Salaam, Mratibu Musa Mwakalinga alisema wanapinga mabadiliko hayo kwani mishahara ya wafanyakazi walio wengi haiwatoshelezi hivyo watakosa mtaji wa kuanzisha ujasiriamali au kujiajiri wenyewe na kujikwamua baada ya ajira kukoma. Alisema mabadiliko hayo yataongeza umasikini kwa wafanyakazi pindi watakapoachishwa au kuacha kazi, wafanyakzi wengine watakaotaka wajiajiri wenyewe pindi ajira yao itakapositishwa.
  Alisema sheria hiyo inakusudia kutotoa huduma bora zitakazokidhi mahitaji mbalimbali ya msingi wa wafanyakazi ambao ni wanachama wa mifuko hiyo inayojali zaidi wafanyabiashara, ambao sio wenye mifuko kwa kuwajengea vitega uchumi ambavyo havimnufaishi mwanachama moja kwa moja. MWISHO

  SOURCE: MWANANCHI
   
 2. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sherikisho la wafanyakazi laandaa maandamano tarehe 04 kupinga swala la mafao. Source Habari Leo
   
 3. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ila jamani huu ni uonevu,wake up watz
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hii Tukuta iko week sana.
   
 5. m

  mamajack JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  no tucta hawako weak wala nini,ni sie wanachama ndio tunamatatizo,tukiitwa hatujitokezi,kama huamini subiri hayo maandamano uone.
   
 6. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  [h=6]SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limeandaa maandamano ya amani kupinga mabadiliko ya kupitishwa kwa sheria ya marekebisho ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).:israel:[/h]
   
 7. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  wanamjua 'sterling' wa intelijensia mzee KV au wanamsikia?

  sasa sijui haya atayazuia kwa kisingizio gani ...tatizo ni watu wanaolidhika haraka. Tuna matatizo lakini akitokea mtu mwenye wazo jipya la kusaidia kuleta mabadiliko wenyewe wanayakataa!
   
 8. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mungu awatangulie maana nji hii, macoplo wa mabom ya machozi hawana kazi.lol!
   
 9. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Madudu ya aina hii yatasababisha nchi isitawalike. Sheria hii naipinga kwa kuwa;
  * Wastani wa Umri wa kuishi Mtanzania kwa sasa ni chini ya miaka 50. Ni kwamba hapa pana dhuluma ni Watanzania wachache sana watakaofaidi michango yao
  * uhakika wa kudumu katika ajira ni mdogo, na itawanyima watumishi walioko kazini kujiajiri/kuacha kazi. Inawezekana mwanachama wa mfuko anakusudia akifikisha michango yake kiasi fulani atakuwa na mtaji wa kutosha kujiajiri.
  * Thamani ya fedha ya Tz inashuka, hivyo fedha uliyokatwa mwaka huu, ukiwa na miaka 35 (kwa malipo ya kila mwezi ya pensheni) itakuwa na thamani gani baada ya miaka 20? Au lumpsum uliyotakiwa kulipwa mwaka huu, kiasi hicho hicho baada ya miaka 20 pamoja na riba itasaidia nini?
  * hivi kwa mfano uko kwenye ajira na (una miaka 30) halafu unaathirika na HIV/UKIMWI utaweza kuishi kufikia umri huo? nb. Marekani baada ya miaka miwili itajitoa kutoa ruzuku ya madawa ya kuongeza umri, je Serikali itaweza kugharimia madawa haya bila mwathirika kuchangia?
  HAPA BUNGE LIMECHEMSHA, LISIJALI KULA MATAPISHI YAKE LIFANYE MABADILIKO KUONDOA SHERIA HII KANDAMIZI HARAKA SANA!!!!!!!
   
 10. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tuko pamoja kwani katika hili linatugusa wengi na hakika tutashiriki. hii ni lini na linaanzia wapi maana naona hata bosi wangu naye atashiriki kwani lina muhusu pia. miaka 55 weeee acha mchezo
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hawa TUCTA na Mgaya wao ni WASALITI wakubwa. Wafanyakazi tugomee kuichangia TUCTA michango mpaka itakapokuwa reformed. Huyu Mgaya na TUCTA yake walishirikishwa kwenye muswaada huo wa sheria wa SSRA wa kuondoa mafao ya kujitoa hadi mtumishi afikishe umri wa miaka 55 au 60.

  Leo TUCTA inakuja kujisafisha eti kwa kuitisha maandamano! UNAFIKI wa hali ya juu mimi sitaandamana ng'o kwa utawala wa huyu Mgaya!

  No wonder Mgaya alimpongeza ACP Kova kwa kumkamata mtekaji na mtesaji wa Dr. Ulimboka, yule kichaa Mkenya Joshua Mulundi. Wafanyakazi tuondoe hiki KIRUSI kinachoitwa MGAYA otherwise were are doomed. Kiongozi gani wa wafanyakazi asiyeweza ku connect DOTS akajua ACP Kova anacheza the comedy! Je huyu ataweza ku negotiate na serikali mafao ya wafanyakazi?!
   
 12. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi bado naona hili suala limekaa kama filamu za Kova,hivi ni kweli sheria hii ilipitishwa bila hata
  shirikisho la wafanyakazi kutakiwa kutoa maoni yao? Na kama walitakiwa kutoa mapendekezo yao
  ilikuwaje waliamua kimyakimya bila kutushirikisha wanachama wao?Napata shida wanapoanza kupiga
  kelele wakati sheria imeshapitishwa.Mgaya niliyemfahamu tuliyeambiwa tuchukue akili zake tuchanganye
  na zetu siyo huyu wa sasa bwana!! Haya maandamano yalitakiwa tuyafanye kabla sheria hii hata huyu
  dhaifu hajaisaini.Any way ngoja nijipe moyo kuwa Mungu ataingilia kati na hii sheria itaondolewa"
   
 13. C

  CDM Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hata kama Mgaya ana makosa yake ya nyuma kwa hili lazima tuungane, tuandamane wote hata tukimwacha Mgaya nyumbani. Kwanza tumechelewa ilikuwa tuanze mandamano kitambo. NJooni wote na hakika hata Kikwete anatushangaa kwa ukimwa wetu.
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  i cant wait to see Kova on TV Tonight ............Kitu Boko haramu/Janjaweed/Alshabab..stay tune...Kesi ipo mahakamani:loco:
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi ni kwa nini mnataka kuupa umaarufu wa bure msitu wa pande?
   
 16. D

  Dimmosen Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi wa Tanzania wameonewa vya kutosha, mshahara mdogo, kodi kubwa, bado serikali inaweka sheria ya ukandamizaji, kwani mafao haya nikiwa hai au nikiwa nimekufa? Life expectance according to Demographic Health survey 2004, women is 46 years, male is 44. Kwa hiyo miaka 55 wakati wa kustaafu mafao hayo ya mfu? Tusikubali kuburuzwa.
   
 17. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nitashikriki
   
 18. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi imeingia kwenye giza kubwa sasa, Mgomo mkubwa wa wafanyakazi wote kupinga sheria mpya ya kinyonyaji ya Mafao. Muda wa kutoka nnje na kuonyesha hisia zetu umefika. Kama unapinga sheria hii siku ya keshokutwa jitokezeni kwa wingi kuelekea kwenye ofisi zote zilizoko wilayani, mkoani au hata mtaani zinazochukua mafao yetu.

  TUCTA wamebariki tujitokeze sasa ni zamu yetu na sisi wafanyakazi tuma message hii kwa watu wengine migodini tusiangushane:

  "Sheria Mpya ya Mafao ni yakinyonyaji tujitokeze wote tarehe 04/8/2012 kupinga sheria hii kwa maandamano"

  It's now or never!

  Aluta continua.
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wanahabari nao wagome kushindikiza mwanahalisi litolewe
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,343
  Likes Received: 19,522
  Trophy Points: 280
  kwa nini nchi haitawaliki?
   
Loading...