TUCTA: Wafanyakazi kugoma nchi nzima kama kodi isipopunguzwa na mshahara kuongezwa

Natamani mgomo uanze mapema nipumzike mie
Mimi naona kwa mwendo huu tusidanganyane.Wafanyakazi bila kuungana mkono hakuna litakalofanikiwa.Mgaya aliwahi kutangaza mgomo akapigwa na akili ya mbayuwayu akanywea.Leo hii badala ya kuunga mkono juhudi za madaktari ili haki itendeke,tucta inatangaza eti mgomo,na dr Ulimboka anaugulia maumivu ambayo yamesababishwa na kudai haki za waliowengi,akili ya mbayuwayu inaibua jambo jipya ili watu wakose pa kushika na maisha yaendelee kana kwamba dr.Ulimboka aliyehujumiwa bado hatma yake haijajulikana.Mimi binafsi ndo maana sipo kwenye vyama vya wafanyakazi maana havina tija,Angalia wanavyochanganya mada.Mimi nilitarajia TUCTA iseme kama madaktari hawajatendewa haki wafanyakazi nchi nzima watagoma.hapo ningeelewa somo,UMOJA NI NGUVU UTENGANO NIDHAIFU.hivi wafanyakazi tutakuwa dhaifu mpaka lini?angalia wenzetu wafanya biashara walipotishiwa na ewura juu ya bei ya mafuta waliungana leo bei ya mafuta iko juu kuliko ilivyokuwa kabla ya ewura kujitutumua,sababu ni kwamba wafanya biashara walishikamana.Madaktari ni wafanya kazi idara za afya,leo tukifurahia kuona wanaonewa,tusubiri kesho itakuwa idara nyingine.Huu ulikuwa wakati muafaka wafanyakazi wote tanzania kushikamana hadi wenzetu watendewe haki lakini tukigawanyika tutegemee kuona na idara nyingine zikionewa.
 
Huyu Mgaya kazidi uoga hata Mie nahitaji kupumzika hebu fanyeni mambos tupumzike
 
Kama watumishi wa kada nyingine mishahara yao hata haifiki nusu ya nadaktari afu madaktari wenyewe wapo kwenye mgomo kwa nini watumishi wa kada nyingine tusiungane na sisi tudai haki yetu...au ndo kusema kuwa tukeridhika na hii hali?
 
Unategemea nn au unataka Roho mtakatifu awaambie viongozi wa Tucta wanakula sahani moja na serikali.... wanahongwa.... then wanafanya comedy as if wanawatetea wafanyakazi na kuanza kujidai KUGOMA ILI WAONEKANE WANAFANYA KAZI KUWATETEA KUMBE MAIGIZOOOOOOO......
 
kila mtu anastahili malipo mazuri lakini pia kila mtu anao wajibu wa kulipa kodi. Unapotaka mshahara upande na kodi ishuke sasa unataka huo mshahara upande utoke wapi.

Haki na wajibu huenda pamoja

we std 7 eh?it seems like u dont know wat u r talking
 
kinachonifurhisha katika nchi hii ni kuona watu wanataka maendeleo then wanataka kodi ipunguzwe na kuwepo na misamaha ya kodi.je tutafika kwa hili
 
Tucta hawana ubavu huo; walishajifunika blanketi moja na watawala wakati wa mgomo wa madaktari sijui kama wana uthubutu huo...


Mzee Mwanakijiji i greet you!

Mimi naanza kushangaa nature ya hii migomo and hili la Dr. Ulimboka linatisha zaidi! hivi sasa hivi ndio hali ya nchi imekua mbaya sana? mbona miaka ya nyuma hali ilikua mbaya zaidi lakini wananchi woote waliipenda nchi yao? tulikuwa tunaminyana kwenye UDA lakini tunachapa kazi! enzi hizo gari zote za maana zilikua ni ST , JW na SU, leo hii hali si hivyo na chuki baina ya watu, vyama inazidi kupamba moto tatizo ni nini? hospital zetu zilikuwa nzuri kabla ya vita vya kagera baada ya hapo hali ngumu! ma dr hwakuwahi hata kuwaza kugoma leo hii kuna nini kipya? mbona wazungu wanatoka kwao kuja huku africa na kufanya kazi vijijini remote areas bila kujali hali kuna madaktari wasio na mipaka (medicine sans frontier) mbona wanafanyakazi kokote hali mbaya njaa bila kujali hali ili mradi kuokoa maisha sisi waafrica tuna tatizo gani?

naanza kupata mawazo mabaya kuhusu hali hii na hasa ukizingatia hii gas ya ma-trillion ya dollars liyogunduliwa inatupeleka pabaya! na hayo ma-Uranium, tunaenda Congo taratibu. dhahabu tushaibiwa tumekubali inaonekana wanaona tumestuka katika hili la gas matatizo yanaanza taratibu.

kwa nini tusijifunze kwa Ghana? wamepata mafuta wakatulia sasa wanavuna, waganda walipo confirm uwepo wa mafuta, kila Mganda na hata M7 waliomba yasiwagombanishe. sisi tunaanza kuumizana hata pipa moja halijatoka! its so sad. Taratibu tunapoteza ile sifa yetu ya utanzania, What is going on?

mimi nafikiri there is some force behind this! This called SUBOTTAGE! au wasiwasi wangu?
 
tudta wanafiki tu, kima cha chinincha 315,000 kimeishia wapi leo wadai 200,000????!!!!
 
hawa TUCTA hawako consistent kwenye madai yao,mbona kwenye mgomo ule walipoitwa wana akili za 'mbayuwayu' madai ya kima cha chini ilikuwa 315,000/= ,sasa hiyo minimum wage ya TZS 200,000/= inatoka wapi tena?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom