TUCTA siku 14 zimekwisha kuna lolote?

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,891
1,212
TUCTA mlisikika mkisema mnaipa serkali siku 14 waturudishie pesa zetu walizokata kwenye mshahara wa mwezi wa pili.

Mwezi wa tatu waelekea ukingoni na hakuna majibu yoyote wala mrejesho wowote dhidi ya pesa zetu tulizokatwa kibabae na bado ya mkopo kinyume cha mnakubaliano yetu ya awali.

Ni kipi kinafata baada ya serkali kulipuuza agizo lenu na je ndo tukubali kuumia kwa kuruhusu makato ya 57% kila mwezi kwa kila kipato chetu?
 
Vyama vya wafanyakazi wamekuwa kupe wanachojua ni kutafuna michango ya wanachama bila kuwatetea hasa tunaposhindwa kupandishwa madaraja bila sababu, vijana 3000 kuondolewa kazini baada ya kuajiriwa...


Tucta sio wakuwaamini,

Goooo TL ukasimie haki za watanzania ikiwemo wafanyakazi
 
Kwani hukusikia alichosema alipokuwa Kusini?

TUCTA mlisikika mkisema mnaipa serkal siku 14 waturudishie pesa zetu walizokata kwenye mshahara wa mwez wa pili...mwez wa tatu waelekea ukingon na hakuna majibu yoyote wala mrejesho wowowte dhidi ya pesa zetu tulizokatwa kibabae na bdo ya mkopo kinyume cha mnakubaliano yetu ya awali....
Ni kipi kinafata baada ya serkali kulipuuza agizo lenu?na je ndo tukubali kuumia kwa kuruhusu makato ya 57% kila mwez kwa kila kipato chetu?
 
Hao jamaa wamebaki kama vibogoyo tu . Hakuna lolote jipya watalo leta.
Jambo liliobaki tuwachongee bao wawe wanacheza ili kusukuma siku zisonge mbele.
 
TUCTA WAMEKUTANA NA TUTA... Hawajiwezi, muda huu ndio ulikuwa mzuri kuonyesha uwezo wao......ila hamna kitu.
 
walisema zoezi la kuhakiki limeisha hata hivyo walivyochungulia hazina wakakuta kweupe wakadai bado watumishi hewa hawajaisha !!
 
Hao wengi wanao iuliza TUCTA sio wanachama wa vyama vya wafanyakazi .....jiunge kwanza ndo uhoji...
 
Ni bora wangekaa kimya, ona sasa nilikuwa nachungulia chochote humu nmb,, looh mara Salio lako halitoshelezi
 
TUCTA hawana ubavu wakuitunishia misuli serikali.Tanzania bado hatuna vyama vya wafanyakazi.Kila mtu ni mganga njaa ndiyo tatizo.Nadhani kwa mwendo huu wengi tutaelewa.Wazazi nao walipoambiwa elimu bure wamewatelekeza wanafunzi.Sasa vijana wanaomba walimu kalamu na daftari hii kali ya karne.
 
Vyama vya wafanyakazi ni vyama vya hiari. nadhani unapaswa kuwaandikia barua ya kuomba kujitoa. Unless huko CWT kuwe na utaratibu ambao ni "legally binding".
Eti waliga mkwala kuwa ipo kisheria na ni lazima kila mtu awepo......nisaidieni pliz nitajitoa suun.....
 
Vyama vya wafanyakazi vyote vya Tanzania viongozi wake ni wachumia tumbo hawana dhamira ya kweli kuwasaidia wafanyakazi ndomana matamko yao hayachukuliwa kwa tahadhari na kuwa tishio kwa waajiri na serikali kwa ujumla nchi za wenzetu chama cha wafanyakazi wakitoa tamko nchi serikali inatetemeka hapa kwetu bure kabisa toka kipindi cha uchaguzi wao ni vigisuvigisu tu
 
Vyama vya wafanyakazi ni vyama vya hiari. nadhani unapaswa kuwaandikia barua ya kuomba kujitoa. Unless huko CWT kuwe na utaratibu ambao ni "legally binding".
Ndivyo ilivyo. Katika sehemu ya kazi idadi ikishazidi kiwango fulani, ni lazima kuwepo na chama cha wafanyakazi. Iwapo mfanyakazi hatakuwa mwanachama, atakatwa michango ya mwezi kama wafanyakazi wengine kwa kisingizio kwamba yakitokea matatizo chama kinawashughulikia wafanyakazi wote. Kwa jinsi Vyama vyenyewe vilivyo, sherehe za siku ya Wafanyakazi katika kipindi hiki zitadorora kwa vile Vyama havisaidii wala kuwatetea wafanyakazi ambao hawatendewi haki kama sheria ya usalama kazini inavyoelekeza.
 
Tawi la CCM hili, tunahitaji akina Tundu Lisu na huku ili wainyooshe serikali
 
Back
Top Bottom