TUCTA, siasa si jukumu lenu. Jukumu lenu ni kuwatetea Wafanyakazi wa Nchi hii

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Haiingii akilini TUCTA kuacha majukumu yake na badala yake kufanya siasa.

Kitendo cha TUCTA siku za Mei mosi kuandaa Mabango, Risala na Nyimbo mbalimbali ambavyo hadi kwa 90% hubeba ujumbe wa kuwasifu tu watawala na asilimia chache kueleza matatizo ya Wafanyakazi ni kwenda kinyume kabisa na malengo ya kuanzishwa kwake.

NB: Naomba Uzi huu usifutwe haraka haraka.
 
Haiingii akilini TUCTA kuacha majukumu yake na badala yake kufanya siasa.
Kitendo cha TUCTA siku za Mei mosi kuandaa Mabango, Risala na Nyimbo mbalimbali ambavyo hadi kwa 90% hubeba ujumbe wa kuwasifu tu watawala na asilimia chache kueleza matatizo ya Wafanyakazi ni kwenda kinyume kabisa na malengo ya kuanzishwa kwake.

NB:- Naomba Uzi huu usifutwe haraka haraka.
Achana na Jumuia ya Chama tawala itakupotezea Muda. Hukumsikia kiongozi wao anasema CCM huwa inawashirikisha kuteua Wabunge 2 wa Viti maalum?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Nchi hii ili upate kitu kwa watawala unafanyaje ?

Wamegundua mbinu ya kupata chao kwahio ndicho wanachofanya (ili indirectly wanawatetea wafanyakazi wao) ukizingatia kwa sasa mfanyakazi yeye anaangalia tu ujira hayo mengine ni ziada...
 
Wananzengo wako bize na ole Sabaya, subiri siku ipite akili zikiwarudia ndio watajuwa bei ya mafuta bado haijashushwa.
 
Walimu wamefanywa vibaraka wa serikali. Hapa wametamgaziwa kazi ya sensa Ila hawajaambiwa watalipwa bei gani. Kazi ikishafanyika wanalipwa kama watakavyo hao walipaji. Terrible!
 
Back
Top Bottom