TUCTA: Pendekezo la Wafanyakazi lilikuwa ni kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na si kanuni mpya ya vikokotoo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limepinga kanuni mpya ya kukokotoa mafao ya wastaafu iliyotolewa hivi karibuni likisema inakandamiza wafanyakazi.

Shirikisho hilo limesema pendekezo la wafanyakazi lilikuwa ni kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na si kanuni mpya ya vikokotoo inayolalamikiwa.

Mjadala mkubwa unaendelea nchini baada ya kutangazwa kwa kanuni mpya za sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2014 ambazo zinaelekeza pamoja na mambo mengine, kuwa wastaafu wote watalipwa mkupuo wa asilimia 25 ya mafao pindi wanapostaafu na asilimia 75 inayobaki watakuwa wakilipwa kama pensheni ya kila mwezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kikao cha 35 cha shirikisho hilo mjini hapa, Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema kanuni hizo ni kandamizi na zimepokewa na wafanyakazi kwa mtizamo hasi na zitashusha ari yao na ufanisi.

“Kuunganishwa kwa mifuko ni hoja ya Tucta tangu mwaka 2004 lakini kanuni mpya ni kinyume cha mapendekezo yetu. Sisi tulitaka kanuni zibaki kuwa za mwaka 2017 ambapo kikokotoo ni 1/540 na mkupuo ni asilimia 50, huku wastani wa umri wa kuishi ukiwa ni miaka 15.5,” alisema Nyamhokya.

Alisema hoja ya ufanisi wa mifuko kwa mkupuo wa asilimia 50 hakutakuwa na shida yoyote endapo Serikali italipa madeni yote ya mifuko na mifuko kuacha uwekezaji usio na tija au kuuza kabisa.

Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imewahi kufafanua kuhusu deni hilo ikisema Serikali haijakopa katika mifuko ya hifadhi ya jamii tangu mwaka 2013 kwa sababu tayari ilifikia ukomo ambao ni asilimia 10 kwa mujibu wa mwongozo.

“Kwenye vitabu vya Serikali madeni yake kwa mifuko ya hifadhi ya jamii bado yapo. Serikali haijakana madeni yake tangu kuunganisha mifuko hii na mara ya mwisho ilisema itatoa hati fungani ili kulipa hayo madeni yake,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka.
 
wamelazimishwa kusema wameshirikishwa... ila muamuaji wa kila kitu tunamjua
 
Kama walishirikishwa je waliweza kuchukua maoni kwa wafanyakazi? Ili kujua wangapi wanaunga huo mpango ama la
 
TUCTA, nashangaa mpaka sasa mnaendelea kutoa matangazo kwa waandishi wa habari! Hiyo haiwasaidii wafanyakazi mnaowatangulia mbele. Nilitegemea sasa tuandike historia mpya kupitia kudai haki hizi. Zipo njia kibao ambazo hazimwagi damu wala nyama ila zinaleta heshima kwetu iwapo tutazitumia.

(i). Hivi inawezekana vipi mimi nifanye kazi miaka 30 kisha unilipe mafungu as if ndiyo makubaliano yangu na Mwajiri wakati naanza kazi?
(ii). Hivi inawezekana vipi Serikali awajibu kwa kujiamini hivyo wakati jasho letu linapotezwa na wachache?

USHAURI
TUCTA SEMENI NENO LA KUTUTIA MOYO (TUIRUDISHE SERIKALI MEZANI KWA NGUVU - SI KUJA KUJADILIANA BALI KUISHINIKIZA).
 
Tuct ipi bro kama hiyp ya Nyamuhokya basi ni sifuri. Wanasubiri kuona rais amecheka akinuna hawawezi kuthubutu
 
Tuna kiongozi mmoja tu kwa sasa ambaye anajiita Jiwe ,wengine wote hawana meno maana wawakilishi tu wakijifanya wanajikuna tu tayari wanapelekewa sms za vitisho na wale vijana wa mkuu wa mkoa DAB
 
Rais wa Tucta Tumaini Nyamhokya ametoa msimamo wa TUCTA leo
Amesema wao hawakubaliani na wafanyakazi kulipwa 25% kutoka 50% kwa kuwa kuna gape kubwa sana, wanataka iwe angalau 40% kama imepunguzwa

 
Serikali ijiangalie, watumishi wa uma wengi wanalia ... Ila ndio hivyo ni makondoo wanaishia kuumia ndani kwa ndani na kupeleka vilio vyao kwa Mungu na miungu yao iwajibie kwa mapigo... Utawala huu dhalimu
 
TUCTA ni kitengo maalumu cha ccm cha kukandamiza wafanyakazi, tunachotaka wafanyakazi ni 75% kwa mkupuo halafu hiyo 25% ndiyo iwe pensheni
 
Hivi kama siku ya kuajiriwa Mtumishi wa Umma uliajiriwa kwa masharti ya AJIRA YA KUDUMU NA MAFAO YA UZEENI "Permanent and Pensionable terms" ambapo huyo pensheni ilikuwepo ikiwa na vikokotoo vyake, je ni halali Mwajiri (Serikali) kutumia ubabe na kubadili terms of Employment Contract bila ridhaa ya Mtumishi husika!!? Hapa naona TUCTA waanze kuangalia namna ya kusaidia Wanachama wao waende Mahakamani hata kama Mahakama ni Sehemu ya Dola huenda akajitokeza mmoja wa waheshimiwa akaelewa na kuondoa hili giza kwa Watumishi wa Umma.

Pili, ni vyema watanzania tukafahamu kuwa, kama ilivyo ngumu kwa namna yoyote ile kumshushia mtu kiwango cha malipo ya mshahara aliokwishafikia hata kama unamemshusha cheo, ndivyo ilivyo kwa Pensheni.

Naungana na TUCTA pale wanaposema kuwa Watumishi wa Umma waliokuwepo watumie Kanuni za 2017 zinazobakiza kanuni za zamani kwa watumishi wote ambao Kanuni mpya zimewakuta tayari ni wanachama wa mifuko iliyounganishwa. Hawa walisaini mikataba ya ajira zao Kanuni za Pensheni zikiwa 1/540 (Commutation factor), 50% (Commutation rate) na kadirio la miaka ya kuishi 15.5. Kihalali kabisa hawakustahili kuingizwa katika kanuni mpya za 1/580, 25% na 12.5 za sasa. Hii ingekuwa kwa Wanachama wapya wa PSSSF na siyo vinginevyo!

TUCTA, pitieni barua za ajira za Watumishi wa Umma mtaona Wanachama wenu wamesaini aina gani ya mikataba na hakikisheni suala hili linatinga Mahakamani haraka iwezekanavyo. Hii itasaidia pande zote Serikali na Watumishi kutoingia katika mgogoro mkubwa hata kusababisha athari katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Langu ni hilo kwa leo.
 
wanatumiwa na mabeberu hao TUCTA,washughulikiwe kikamilifu,wanarudisha nyuma juhudi za mheshimiwa kununua mandege na kujenga madaraja
 
mdee.jpg
 
Nawakumbusha,

Mh Kangi Lugola anaomba "Wananchi kuwa na huruma, mwachangie ASKARI hela za kuwajengea nyumba, kama mnavyotoa michango sehem nyingine kama vile michango ya ujenzi wa zahanai, shule n.k"
 
Back
Top Bottom