Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,278
- 37,402
Leo Mei 1, 2021 ni siku maalum kwa wafanyakazi duniani kote. Ni siku ya kumbukizi la wafanyakazi kudai maslahi na mazingira bora ya kazi. Ni siku ambayo waasisi wake walikiwasha kweli kweli kuhakikisha wanawasukuma waajiri kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa mashambani na viwandani, na kuhakikisha mazingira ya kufanyia kazi yanaboreshwa kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi na ufanisi wa kazi. Kama waanzilishi wa vuguvugu hili la kudai haki za wafanyakazi wasingeweka msukumo thabiti kwa waajiri, mpaka Leo wafanyakazi wangekuwa wanachapwa viboko mara tu wanapoinua pua zao kudai haki.
Lakini tofauti na viongozi wa wafanyakazi wa kipindi hicho, Leo tuna viongozi nyoronyoro, viongozi mchelemchele ambao hawajui hata wanasimamia nini. Viongozi wanagombea uongozi wa vyama vya wafanyakazi si kwa lengo la kutetea maslahi ya wafanyakazi, bali kutetea matumbo yao kwa kulipana mishahara/posho zilizonona bila kujali wanaowaongoza wako dhofli khali. Kiongozi mkuu wa wafanyakazi unasimama mbele ya mwajiri mkuu na kusema:-
1.Mheshimiwa ikikupendeza waweza kutuongezea mshahara.
2.Mheshimiwa ukiona inafaa utupandishe madaraja
3.Mheshimiwa kwa vile Jana umechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama tawala kwa kishindo nasi njoo uonyeshe moto kama utaona tunastahili.
4.Mheshimiwa kama hali ya uchumi ni nzuri basi utulipe madeni tunayoidai serikali.
Kwa sitahili hii nakubaliana na wanaosema viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni watumwa wa chama tawala cha siasa waliowekwa pale kwa lengo la kuhakikisha maslahi ya chama hicho kimachoongoza serikali hayachahafuliwi.
MODS TAFADHALI, NAOMBA UZI UJITEGEMEE.