TUCTA kujadili kima cha chini cha mshahara 2019

Hivi folio by a posho,mshahara mdogo ni vingi sana chamsingi tutafte fursa tupige kazi maisha yanaendelea

Sent from my SM-J810F using Tapatalk
 
Hii nchi tuishi tu maana kuna mambo mengne ukiyafatilia unaweza kutamani ufe uwaache na maigizo yao.Hao TUTA(TUCTA) wamekaa kimya kwa miaka mi4 halafu tunakaribia uchaguz ndio sarakasi zinaanza.Kweli wajinga ndio WALI WAO.
 
BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
Hawa TUCTA walikuwa wapi muda wote huo mpaka waone uchaguzi utadhani na wao ni ccm!
Wanafiki sana hawapaswi kuwawakilisha wafanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni mantiki ya kuwepo kwa hawa tucta..maana serikali inafanya inavyopenda kwa wafanyakazi wake
 
Kwani mwenyekiti wa tume ya Waziri Mkuu ya kuboresha mishahara anasemaje?

Point hapo ni kuwa na scale za mishahara inayofanana no matter what. Kama Engineer II basi atalipwa sawa na Wahandisi wenzake wote wa Daraja II awe Halmashauri/Wizarani/Tanesco/Tarura/Tanroads/ N.K

Dereva wa Gari la Rais alipwe sawa Na wa Gari la wafungwa? Hahahahaha
 
Suala la kulinganisha Mishahara kwa watu wenye sifa zinazofanana ila wanao fanya Kazi katika Idara tofauti tofauti za Serikali;
Kwa mtazamo wangu;

  • Hiyo italeta tija kama watatazama pia mfumo wa kutoa Posho kwenye idara za Serikali. Nimesema hivyo nikimaanisha zipo Taasisi ambazo mfumo wa kupewa posho unawafikia/unawapendelea zaidi kuliko wafanyakazi wengine wa level moja hii hufanya wengine kufikia kujipatia ziada ya kwenye 25% to 100% ya mshahara wa kila mwezi.
  • Aina ya kazi; wapo wafanyakazi wenye fursa na muda wa kufanya na kusimamia miradi yao binafsi kulingana na nature ya kazi yao; mfano: Idara ya kilimo, Engineer wa Ujenzi nk ukilinganisha na mkufunzi wa Idara ya kilimo/Engineer.
  • Naamini kazi zote zinahitaji dedication, ila idara kama ya taaluma inamfumo mzuri wa kufuatiliwa na pia kule ndiko wanako toka wafanyakazi bora na waliopikwa vizuri hivyo nafikiri hii sector isihusishwe na hili suala badala yake Iboreshewe zaidi. Kwa hili la Elimu nafikiri tuwe makini tusije kuharibu Msingi wa nyumba, tukaishia kujivunia kuwa tumepaua kwa bati la msouth?
  • Angalizo: mimi sio Mwalimu wala sifanyi kazi idara ya Elimu!
Mapendekezo yatapelekwa ila Uncle haongezi hata mia mpk mwakani tena ataongeza 30

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa
Huwa una uelewa mpana sana ila huwa unajitoa ufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dereva wa Gari la Rais alipwe sawa Na wa Gari la wafungwa? Hahahahaha
Itakuwa hivyo mkuu Pohamba though wanaweza kutofautiana kwenye posho tu za kujikimu. Kwa maana yule dereva atakayekuwa anamwendesha Mhe. Rais atajikuta anapata posho mara kwa mara kulingana na uwingi wa safari za Rais.

Pia mishahara itatofautiana kulingana na seniority kwa maana Dereva Daraja I hawezi kulipwa sawa na dereva Daraja II
 
Kwani mwenyekiti wa tume ya Waziri Mkuu ya kuboresha mishahara anasemaje?

Point hapo ni kuwa na scale za mishahara inayofanana no matter what. Kama Engineer II basi atalipwa sawa na Wahandisi wenzake wote wa Daraja II awe Halmashauri/Wizarani/Tanesco/Tarura/Tanroads/ N.K
Mkapa alipoingia madarakani alifanya kila shirika/kampuni kulipa watumishi wake mshahara kutokana na jinsi wanavyoingiza kipato, hii ilileta tija na ufanisi wa kazi maana kila shirika/kampuni walifanya kazi kwa bidii ili kuinua kipato cha shirika/kampuni. Sasa kama tunarudi tena kule kwa watu wote kulipwa sawa bila kujali umeingiza kiasi gani, nadhani tunaenda kuua morali wa kazi kwa yale mashirika/kampuni zilizokuwa zinafanya vizuri kitendaji
 
Sasa kama tunarudi tena kule kwa watu wote kulipwa sawa bila kujali umeingiza kiasi gani, nadhani tunaenda kuua morali wa kazi kwa yale mashirika/kampuni zilizokuwa zinafanya vizuri kitendaji
Of course Morali inaweza kuathiriwa na hili ingawa inaweza kuwa maintained kwa kuboresha posho zao za extra duty na per-diem.
 
Nyinyi sio wafanyakazi wa serikali, ni 'wafanyishwa kazi' wa serikali. Na kulipwa mshahara/ posho si haki yenu, ni fadhila tu. Kama ni haki yenu basi acheni kufanyishwa kazi na mje mfanye kazi tuone.
Wao wenyewe wameamua kwa hiari yao kufanyishwa kazi wewe kipi kinakuwasha.Wewe unaye fanya kazi kwanini hawakuonei wivu?,acha wivu wa kike.
 
BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
Hili tumwachie Mh. Rais siku akiona inafaa ataongeza mwenyewe. Kila mwaka mnajadili then tunaishia kusikia sauti tu za TUCTA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUCTA,mei mosi imekaribia mmeanza maigizo yenu ili kuwavutia watumishi wahudhurie MEI MOSI,halafu mei mosi ikiisha wanatoka wamechoka na wamenuna.Duniani humu hakujawahi kutokea urafiki kati ya MDAI HAKI na MTOA HAKI.Ni TUCTA pekee ndio walio na urafiki na mtoa haki kwenye sayari hii ya dunia.
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa
Point yako nimeipata

Happiness is a choice
 
Back
Top Bottom