TUCTA inashindwa kufuatilia utekelezaji wa agizo la Rais lakini inaandamana kumshukuru Rais

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Kwa waliosoma gazeti la NIPASHE la leo tarehe 8/1/2019, watakuwa wameona habari inayoripoti jinsi ambavyo watu na wanachama wa mifuko ya jamii wanavyosumbuka na kupigwa danadana juu ya mafao yao.

Siku ya tarehe 28/Desemba/2018 Rais alisema utaratibu wa zamani ulipaji mafao uendelee kwa kipindi cha mpito mpaka mwaka 2023. Lakini jambo la kuudhi, kusikitisha na kughadhabisha ni kwamba hawa NSSF, wamegoma kufuata maelekezo yaliyotolewa na Rais yaliyotolewa mbele ya hawa TUCTA.

Nimeseikia taarifa kwamba, TUCTA mkoani Dodoma wamefanya maandamano kumpongeza Rais, lakini wakati wakifanya maandamano hayo wanashindwa kufanya ufuatiliaji juu ya maelekezo ya Rais iwapo yanatekelezeka au lah.

Sasa mmeshindwa kufanya ufuatiliaji halafu mnaanza kufanya maandamano ya kumpongeza Rais, je mnapongeza Rais kwa lipi wakati waliokuwa wanachama wenu wanataabika, mnampongeza Rais kwa lipi wakati wanachama wa mifuko ya jamii wanaodai mafao wanateseka?

Nyie TUCTA mbona mmekuwa wanafiki kiasi hiki? Mbona mmekosa aibu, mbona mmekosa huruma?
 
Viongozi wa tucta ni kama Nyumbu tu!!! Hivi hakuna bodi ya TUCTA! Ilipaswa kuvunjwa na uongozi uliopo kusambaratishwa ili waje viongozi wenye kutetea maslahi ya wafanyakazi wenzao!!! Namkumbuka sana Mgaya!!! Japo kuna wakati alikuwa analegea but the man was strong!!! Sio hizi Mburrulaaz Nyumbuuz zilizoko hapo tucta sasahivi.
 
Back
Top Bottom