TUCTA imeendelea kutetea haki za wanyonge, jamani wafanyakazi wanyonge tuunge mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUCTA imeendelea kutetea haki za wanyonge, jamani wafanyakazi wanyonge tuunge mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PROFESA KYANDO, Aug 5, 2012.

 1. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUCTA: katiba iboreshe maslahi ya wafanyakazi

  Thursday, 02 August 2012

  Zaina Malongo na Patricia Kimelemeta
  SHIRIKISHO la Vyama Vya wafanyakazi (TUCTA) limeitaka serikali kuhakikisha kuwa, mchakato wa marekebisho ya katiba mpya yalenge kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla.

  Hayo yalisemwa kwenye mkutano ulioshirikisha wadau mbalimbali wa shirikisho hilo kwa kushirikiana na Jukwaa la katiba ili kutoa maoni yao juu ya marekebisho ya katiba mpya hasa kipengele cha wafanyakazi.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa tucta Nicolaus Mgaya alisema lengo ni kuhakikisha kuwa, maslahi yao yanaondoa migongano baina ya wafanyakazi, serikali na waajiri.

  Alisema kutokana na hali hiyo wadau hao watatoa maoni yao ambayo yatawasilishwa moja kwa moja kwenye Tume ya Kukusanya maoni kuhusu katiba ili yaweze kuingizwa na kuleta maslahi ya wafanyakazi.

  “Lengo la Tucta ni kuhakikisha kuwa maslahi ya wafanyakazi yanalindwa, yanaheshimiwa na kutathiminiwa pindi mfanyakazi anapokuwa kazini au amestaafu, jambo ambalo litaweza kuondoa migogoro na migongano ya hapa na pale,”alisema Mgaya.

  Aliongeza kutokana na hali hiyo maoni hayo yameangalia mambo mbalimbali likiwamo maslahi ya wafanyakazi, masuala ya mgomo, haki zao pamoja na kujiunga kwenye shirikisho hilo ili waweze kutetea maslahi yao kwa ujumla.

  Alisema kutokana na hali hiyo wanaamini kuwa matatizo yaliyopo nchini yakiwamo migogoro, migomo na maandamano yanaweza kuondoka ikiwa serikali itazingatia mapendekezo yatakayowasilishwa.

  Alisema kutokana na hali hiyo wanachama walio mikoani watapelekewa mapendekezo hayo ili waweze kuyapitia na kurudisha majibu.

  “Tumeangalia katiba yetu na tukaangalia marekebisho ya katiba za nchi zilizoendelea, zikiwamo Kenya, Ghana, Afrika ya Kusini lengo ni kupata katiba bora ambayo itajali maslahi ya wafanyakazi, jambo ambalo tunaamini linaweza kuleta mafanikio,” aliongeza.

  Alifafanua kuwa, wakati uliopo ni muhimu kuangalia matatizo yaliyopo na kuyafanyia marekebisho ili yaweze kuingizwa kwenye mchakato wa katiba mpya ambayo itajali maslahi ya wananchi zaidi kuliko viongozi.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa vipengele vyenye umuhimu haviondolewi ili kulinda maslahi ya wananchi.

  ‘’Jukwaa la katiba limepanga kuhakikisha kuwa vipengele vitakavyofanyiwa marekebisho vinalindwa ili viweze kutumika kwenye vizazi vijavyo ili kuboresha utawala bora,” alisema Kibamba.
   
Loading...