Tuchukue hatua zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuchukue hatua zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, Jan 5, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hello

  Wakati mapambano ya kudai uhuru wa kweli yakiendelea katika namna tofauti tofauti, hasa ukizingatia kwamba leo kule Arusha Chadema wameamua kuchukua hatua nyingine zaidi katika mapambano haya kwa kuhamasisha UMMA wa wazalendo wa Arusha kuandamana mimi napenda kutoa hoja ya kuchukua
  hatua katika kumudhoofisha Adui.

  Natambua kwamba Rostamu Azizi ni mmoja kati ya watu wanaosimamia misingi ya kutumasikinisha
  watanzania katika kila namna, na kwa sababu fedhuli huyu amepata fursa hii kwa sababu ya nguvu za kiuchumi alizonazo, hoja yangu ni kwamba tushambulie nguvu hizi kwa uwezo wetu wote.

  Sina details za kutosha juu ya vyanzo vya mapato vya huyu fisadi (wenye navyo watatusaidia), lakini
  kwa vile tunavyovifahamu napendekeza tutumie haki yetu katika kuvidhoofisha, bila kuvunja sheria.

  Kwa namna moja au nyingine sisi ndio walaji wa bidhaa zinatoka kwenye Makampuni ya fisadi huyu (na wenzake), hivyo sisi ndio chanzo chake kikuu cha mapato, tusitishe uteja wetu kwa bidhaa zake.

  Tuache kutumia bidhaa zinazozalishwa na makampuni ya fisadi huyu, kwa mfano VODACOM.
  Tuache kutumia mtandao huu, siwezi kusema tugome sababu hakuna mtu anayetulazimisha, ni hiari yetu
  na sababu kwa hiari tumeamua kutafuta huu wa kweli, TUACHE KUTUMIA MTANDAO HUU.

  Wanaofahamu bidhaa zake nyingine, na za mafisadi wengine waweke hapa
  kazi ianze.

  Hima watanzania

  TUCHUKUE HATUA ZAIDI
   
Loading...