Tuchukue hadhari kuzuia uagizaji magari makuukuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuchukue hadhari kuzuia uagizaji magari makuukuu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitia, Oct 29, 2008.

 1. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii ina maana kuwa hata magari yaliyozidi miaka mitano ambayo tayari yalikuwepo na kutumika nchini yasiruhusiwe kutumika kwa vile yamekuwa kuukuu? Mimi naona kitu cha kuzingatia hapa ni ubora wa gari, na sio umri, maana gari linaweza likawa na miaka hata mitatu lakini likawa na hitilafu ambazo zinaweza kusababisha ajali.

  Tuchukue hadhari kuzuia uagizaji magari makuukuu

  2008-10-28 16:20:21
  Na Mhariri

  Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama mwishoni mwa wiki alisema kwamba serikali inakusudia kuanza utaratibu wa kuzuia magari yenye zaidi ya umri wa miaka mitano kuingizwa nchini.

  Katika kauli hiyo, Waziri huo alisema sababu kuu ya serikali kutafakari hatua hizo ni baada ya kugundua kwamba ajali nyingi za magari zinachangiwa kwa kiwango kikubwa na uchakavu wa magari hayo.

  Kwa maana hiyo umri wa magari haya kadri unavyokuwa mkubwa ndivyo uwezekano wa kuhusika katika ajali unaongezeka.

  Inawezekana kabisa kwamba Waziri Masha anatoa kauli hii kulingana na utafiti uliofanywa na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.

  Kwa maana hiyo ana ushahidi usiotiwa shaka kwamba magari makuukuu yamekuwa chanzo kikubwa cha ajali nchini.

  Hata hivyo, tunafikiri serikali inawajibika kutafakari vuzuri na kwa kina zaidi juu ya hatua hizi inazotaka kuchukua kuhusu magari makuukuu.

  Tunasema haya kwa sababu tunapotazama uchumi wa taifa hili na watu wake tunajawa na hofu kama kweli ni watu wangapi watakuwa na uwezo wa kununua magari mapya.

  Tunasema haya kwa sababu historia inashuhudia ukweli huo, wakati magari makuukuu yalipokuwa yameharamishwa nchini, idadi ya magari ilikuwa ndogo sana.

  Uchache wa magari haya kwa kiwango kikubwa ulikwamisha kasi ya maendeleo, matokeo yake ni mrundikano wa watu katika vyombo vya usafiri na hata kukwama kusafirisha mizigo na huduma nyingine.

  Ilikuwa ni kawaida kabisa watu kutumia hata malori kusafiri katika maeneo ya mjini, lakini kibaya zaidi upigwaji marufuku wa magari makuukuu wakati huo haukuongeza kasi ya wananchi kujiletea maendeleo yao.

  Kwa hali hii basi, tunaamini kwamba hata kama serikali ina kusudio zuri kiasi gani katika kuyaondoa barabarani magari makuukuu, bila kwanza kutafiti kwa kina na kuelewa vizuri uwezo wa Watanzania, hatua hiyo inaweza kuwa ni ya kufifisha maendeleo kuliko kuyaharakisha.

  Tunajua, kwamba katika sheria na kanuni za kuagiza magari nchini waagizaji wote wanapashwa kuzingatia viwango.

  Kuna vyombo vya ukaguzi wa magari kabla ya kupakiwa melini kutoka kokote katika kona ya dunia hii, lakini pia kuna vyombo vya ukaguzi kabla ya kupakuliwa kutoka melini.

  Kote huko uzingatiaji wa viwango, ubora na uwezo wa vyombo hivyo kutembea barabarani unapaswa kuhakikiwa kwa umakini mkubwa.

  Swali linalosumbua, ni je, magari yote yanakaguliwa vilivyo na hivyo kuruhusiwa kutembea katika barabara zetu?

  Tunathubutu kusema, kama vile tunavyoona bidhaa feki madukani zikiwa zimepitia kwenye bandari au vituo vya forodha katika mipaka yetu zikiwa zimezagaa mitaani, nayo magari makuukuu ambayo hayastahili kugusa barabara zetu, pia hupitia kwenye vituo hivi.

  Kwa hali hiyo, kinachochangia magari mabovu kujaa barabarani si suala la uchakavu wake kwa maana ya kuwa ya miaka mingi tangu kutengenezwa, ila ni udhaifu mkubwa katika kudhibiti bidhaa zote zinazoingia nchini.

  Kwa hali hiyo basi, kukimbilia kutunga sheria ya kuagiza magari kutoka nje kwa kuweka umri wa miaka mitano haitakuwa tiba ya ajali za barabarani.

  Suala la ajali barabarani ni pana, lina mlolongo mrefu; kama vile utoaji wa leseni kwa madereva, uwajibikaji wa trafiki barabarani, lakini kubwa zaidi tabia ya wenye magari ya kutaka kujipatia kipato kikubwa kwa haraka bila kujali usalama kwanza.

  Ni kwa hali hii tunafikiri hatua yoyote ya kuharamisha magari yenye zaidi ya miaka mitano kuingia nchini haitapunguza ajali, ila itazidisha umasikini kwa Watanzania.

  Kazi ya kudhibiti ubora ipewe kipaumbele kuliko sheria za mkumbo kama hii iliyopendekezwa na Waziri Masha.

  * SOURCE: Nipashe
   
 2. M

  Math2009 Member

  #2
  Oct 30, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Ni kweli sheria hii ni ya kukurupuka,na haitasaidia kabisa kupunguza ajali,bali nikuwazuiwa watanzania kutonunua magari,Mimi niko hapa Addis ababa,ethiopia, ambapo kila gari lazima liwe na valid inspection document ambayo inadumu kwa mwaka mmoja,hii ni kwamba gari lazima ichekiwe kila mara baada ya mwaka mmoja na kitengo cha mamlaka ya usalama barabarani na hamna RUSHWA ambalo ni tatizo kubwa Tanzania.
   
 3. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Math009,
  Ukweli ni kuwa Tanzania rushwa na njaa ndio inayopelekea viongozi kufanya maamuzi ya hovyo. Mimi nilikumbana na askari immoja wa usalama barabarani akanisimamisha na kuuliza kama nina stika ya usalama barabarani nikamjibu sina...Cha kushangaza akatoa kwenye kibahasha kidogo stika akataka nimpe 5,000/= nikatoa nikachukua stika nikaweka kwenye gari yangu..nikatimua. Sasa angalia magari mangapi yanapita katika hali ya aina hii. Baada ya kukagua gari na kunishauri kuwa gari langu may be ili liwe road worth linahitaji matengenezp fulani yeye ananiuzia stika naendelea kupeta tu...
   
 4. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Haya ni matitizo ya kutumia muda mwingi kufikiria siasa, na ndio maana mawaziri wengi wanatema "hewa" mara nyingi.

  Kwa maana hiyo, hayo magari yatakayokuwa yameingizwa yakiwa mapya, yakifikisha miaka 5 basi yatakuwa watayaondoa? mimi nadhani sasa tuna magari mazuri mara nyingi kuliko ilivyokuwa kabla ya soko la magazi ya zaliyotumika.

  Tatizo ni kuwa watu wanapenda kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu, kuna ukaguzi wa magari, lakini ukaguzi ni 5000 kwa trafiki. magurudumu mabovu, unahitaji 2000-5000 kwa trafiki! hata kama gari ina miaka 2-3 litaepuka vipi ajali? mimi nadhani magari hayana tabu ila wanaotakiwa kuhakikisha sheria zinafuatwa, wamezigeuza miradi yao.

  Kwa hili, nadhani Masha anatakiwa apuuzwe! Pia, yampasa kujua kuwa sio wote tanzania wanapata fedha za ufisadi.

  Je, shangingi analotumia sasa litakapouzwa baada ya kutimiza umri stahili, yeye hatalinunua kwa kuwa umri wake utakuwa unakaribia miaka 5?
   
 5. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Alianza James Kombe, sasa amefuata Lawrence Masha na hii hoja ya kipuuzi, samahani kwa lugha hii lakini nimeudhika sana. Hawa watu kwa kuwa wao wanatembelea magari ya serikali yanayogharimiwa kwa kodi zetu, wanajifanya kusahau kabisa kuwa wananchi wa kawaida wanataabika kwa kukosa kabisa usafiri. Maeneo mengi ya vijijini bado kuna watu wanatumia usafiri wa mikokoteni inayovutwa na punda na maksai. Usafiri wa kupanda matrela ya matrekta unaonekana "anasa" kwa baadhi ya vijiji vilivyojaliwa kuwa na watu wanaomudu kununua trekta, au yale matrekta ya vyama vya ushirika. Daladala nyingi tunazopanda huko mitaani zina umri wa miaka 10 na zaidi, na zile Landrover za Mererani na Toyota Stout zinazokwenda Narumu na Kirua Vunjo zina umri wa miaka hadi 30. Bado wananchi hawamudu usafiri tofauti na huo, na serikali haijafanya lolote kuwaletea mbadala. Leo inaibuka na hoja kichekesho ya kupiga marufuku magari yenye miaka mitano, ambayo hata kwa mtanzania mwenye kazi nzuri na kipato kizuri sana bado ni magari mapya sana!

  Nanusa kitu hapa, kuna harufu ya ufisadi! Tusishangae kugundua kuna mtu anataka kuleta showrooms zake zenye magari hayo yanayodaiwa yana miaka chini ya mitano, sasa anafanya "market creation" kwa nguvu! Hivi sababu ya ajali ni hiyo tu? Mbona sababu nyingine hazishughulikiwi, mnang'ang'ania hiyo tu ili kutuletea umasikini?

  Tuliyaona haya wakati William Kusila akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi miaka ya mid 1990's. Wakaja na mradi wao wa "speed governors", walipopata chumo lao mradi ukafa! Sasa wanakuja na hii mpya, si bure, iko namna kuna mtu anasukumiza mradi wake kwa nguvu hapa!
   
 6. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  Umri wa magari ni kasabau kadogo miongoni mwa misababu milima inayosababisha ajali. Walio ughaibuni watakubaliana nami kuwa nuna magari hata yana miaka 20 lakini bado yanaonekana kama yana miaka 4 tu.
  Sababu kubwa za ajali nchini ni ubovu wa barabara. kama hazina mashimo basi ni barabara za grade ya chini ambayo huteleza(slipery kama ni ya lami). Pili ni kukosa highways katika barabara kuu. Mwambiye Masha ajenge Highway katika barabara kuu i.e DSM - Mwanza. DSM Mtwara, DSM - Mbeya, DSM - Arusha, makambako- Songea, Songea- Mtwara, Sirari- via Musoma- Mwanza, Kahama- kigoma, Mwanza Bukoba.Iringa Dodoma, Dodoma Arusha. Hizo ni baadhi tu. At least Dual carriageway. na halafu ziwe mkeka. then tuone hizo ajali zitakuwa ngapi.

  Maeneo mengine ni Madereva waliofuzu kuendesha kwakusoma. sio kununua leseni. Shule maalum za kufundisha madereva katika level mbalimbali. POLICE wasihusike na kutoa leseni, Iwepo mamlaka kamili kwa ajilia hiyo. Mitihani iwe ya nadaria na vitendo. software zipo kibao tu kwa ajili ya Computer thery test sio (kusahihishwa na maganga). ukimaliza kujibu maswali majibu unapata sekunde hiyohiyo. then mwalimu aliyesajiliwa ndiye aandikishe dereva mwanafuzi kwa ajili aya Practical test. Hivyo tunakuwa na uhakika kila aliyeko nyuma ya usukani ni mjuzi wa kutosha.

  Magari yawe yanakaguliwa na kupewa kibali cha kuwa barabarani. Sasa ikitokea Fundi aliyeidhinishwa kutoa kibali kuwa gari ni ok halafu kumbe ni bove afungiwe kufanya kazi za ufundi na shitakiwe. hivyo kila ukiona gari una uhakika liko salama na mwendeshani ni mfunzwa na barabara ni swafi.

  Lakini yote hayo hakuna. Masha anafikiria watanzania wote ni mafisadi wa kununua brand new cars!! ASHINDWE!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio upya au uchakavu wa magari ni UKAGUZI hafifu.Halafu hii ya magari ya chini ya miaka 5 watuambie wameitoa wapi kwakua wengi wetu tumetembelea nchi zingine na tumeona magari hata ya mika 50 yako barabarani.Hapa 'ROADWORTHINESS' ndio kiangaliwe.Tatizo letu ni watu kutotaka kufanya kazi,magari yakaguliwe kila miezi 6 sio kuuziwa stika.Kuna mzee mmoja ana Peugeot yake a 1963 aliniruhusu kuendesha siku moja mpaka raha kila kitu kinafanya kazi vizuri,ni matunzo tu.
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Hizi data ni za kupotosha, kwa kuwa majority ya magari ya TZ yana zaidi ya miaka mitano of coz majority ya ajali zitakua zinahusisha magari yenye zaidi ya miaka mitano.

  Ukweli ni kwamba barabara ni mbovu na ndogo sana. Usiku ndo usiiseme, hakuna streetlights so kila mtu anawasha full-light basi unakua hauoni kabisa mbele! Sometime najikuta nendesha kwa kuangalia niko umbali gani kutoka pembeni ya barabara kwa sababu mbele sioni kitu!!
   
Loading...