Tuchel na Cakir ndio wanaoijua Anfield, siyo Neymar

The Boldly

JF-Expert Member
May 21, 2017
2,324
2,000
USIKU! Yes Usiku wa Alhamisi ya April 14, 2016 ndio usiku pekee wa kusisimua kuwahi kutokea katika dimba letu la Anfield. Usiku uliokuwa na jasho, damu na machozi. Usiku wa vita.

Usiku ambao Borrusia Dortmund yake Thomas Tuchel ilikutana na maajabu ambayo AC Milan na West Ham kwa nyakati tofauti iliwahi kukutana nayo mbele ya Liverpool kwenye viwanja tofauti.

Ni usiku ambao mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Ugiriki alipuliza kipyenga cha mwisho huku Dunia ikishuhudia Liverpool ikiibuka na ushindi wa magoli 4-3.

Hujanielewa bado: Huu ulikua ni mchezo wa second leg hatua ya robo fainali kati ya Liverpool na Dortmund. Mchezo wa awali ulimalizika kule Ujerumani kwa sare ya bao 1-1.

Unabakia kuwa usiku wa maajabu kwa namna ambavyo Liverpool ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi.

Tayari kikosi cha Tuchel kilishatanguliza mguu mmoja nusu fainali lakini goli la dakika ya 90+1 kutoka kwa beki Dejan Lovren likashuhudia vijana wa Jurgen Klopp wakipindua matokeo.

Wakati huu ambao unajaribu kunielewa nikueleze kwamba leo Tuchel anarejea tena pale Anfield. Safari hii anakuja na PSG katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi.

Tuchel anaielewa atmosphere ya Anfield anajua namna ambavyo yeye na wanae wa BVB walikutana na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki, watu wa Liverpool na wachezaji wake ndani ya uwanja.

Ubora wa Liverpool huanzia nje ya uwanja ilipo mitaa ya 11th Street Pub hadi St Elsie..huwa hatupoi..tunakinukisha ile kinoma na Tuchel anajua hilo.

Sasa punde tu baada ya makundi kupangwa staa wa PSG, bwa'dogo Neymar alikaririwa akiitupa nje ya mbio za ubingwa wa EPL, Liverpool. Kwamba anatuchukulia poa.

Hapa ndipo hasira zetu dhidi ya PSG zilipozidi na kwa sababu huyu mtoto hajawahi kutua Anfield nafikiri ni vema angemuuliza Tuchel nini alichokutana nacho.

Mtu pekee tofauti na Tuchel ambaye anaweza kumueleza Neymar ugumu wa kucheza na sisi kwenye uwanja wetu wa nyumbani hasa linapokuja suala la usiku wa Ulaya basi ni Cakir.

Huyu ndie refa ambaye pia leo atachezesha pambano letu na PSG, anajua watu wa Anfield walivyo, anaijua roho ya kipiganaji tuliyonayo. Pengine anawaonea huruma PSG kimoyo-moyo.

Kinachofurahisha ni kwamba PSG wamekuwa na rekodi mbaya pindi wanapokutana na refa huyu ambapo hawajashinda kwenye mechi mbili ambazo Cakir alisimama katikati.

Sisi tuna bahati nae, tuliichapa Dortmud ya Tuchel yeye akiwa katikati ya uwanja hivyo hatuna shaka na nyota yake kwetu.

Niwasihi mabeki wa PSG wakiongozwa na babu Thiago wawe makini spidi waliyonayo wale wakorea weusi wetu kule mbele si ya kitoto.

Wasidhani tutaleta utani hata kidogo, Bobby Firmino imethibitishwa kuwa atacheza na jicho moja baada ya kuumizwa na Vertogen juzi Jumamosi.

Hatuna shaka na hilo msimu uliopita alipiga magoli manne bila kuangalia goli 'no look' nini game moja na PSG? Waleteni hao matozi bwana!.

Eddie Cavan na Mbappe wanapaswa kutambua uwepo wa Le Commandment Field Marshall, Virgil Van Djik kule nyuma. wakumbuke wanacheza na beki ghali duniani.

Neymar huyu hatoamini jinsi ambavyo Trent Anord atamficha ndani ya viatu vyake vya Armour Magnetico..nawahakikishieni alichokutana nacho Gaucho kwa Arbeloa miaka 10 nyuma ndicho huyu tozi atakutana nacho.
download%20(2).jpg

Muungwana
 
Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,715
2,000
Mkuu liver mmeanza panic mapema mno hivi Van Dijk,Gomez na Anold wa kumficha Neymar,Mbappe,cavan nani hahahahaha.......

Liver leo ukuta mzuri hamna cha kujovunia leo muweze kumiliki mpira 70% hivi hivi mnaumia sasa wenzenu katikati anasimama Verrati,Rabioti very talented midfielders.......kazi ipo but game itakuwa nzuri mnooo ila msiseme mnashinda tegemeeni na bahati pia
 
kamarah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
843
1,000
Well said mtoa mada, ila UEFA droo yao sijui ilikumbwa na nini maana teams hizi zilitakiwa kukutana Robo au nusu fainali huko na sio mwanzoni namna hii
 
radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,151
2,000
Well said mtoa mada, ila UEFA droo yao sijui ilikumbwa na nini maana teams hizi zilitakiwa kukutana Robo au nusu fainali huko na sio mwanzoni namna hii
Unaweza kukuta hao wakaenda hizo hatua za juu maana huku ni kukusanya point tu hatua za awali
 
Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,715
2,000
Well said mtoa mada, ila UEFA droo yao sijui ilikumbwa na nini maana teams hizi zilitakiwa kukutana Robo au nusu fainali huko na sio mwanzoni namna hii
Hakuna kilichokosewa katika kuoanga timu hapo mmoja alikuwa mshindi wa kwanza mwingine mshindi wa 4
 
dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,881
2,000
Mkuu liver mmeanza panic mapema mno hivi Van Dijk,Gomez na Anold wa kumficha Neymar,Mbappe,cavan nani hahahahaha.......

Liver leo ukuta mzuri hamna cha kujovunia leo muweze kumiliki mpira 70% hivi hivi mnaumia sasa wenzenu katikati anasimama Verrati,Rabioti very talented midfielders.......kazi ipo but game itakuwa nzuri mnooo ila msiseme mnashinda tegemeeni na bahati pia
Mkuu nakuomba urudi kutetea hii comment yako
 
Collo96

Member
Sep 17, 2018
22
75
Ndio shida ya vjana kujua mpira juz bas wanajikuta wachambuz wazur lakn ukwel utabak Liverpool n moja ya klabu bora ulaya kila atakaye pangiwa naye lazma atambue hilo kuwa amepangiwa na timu kisiki ACHENI USHABIKI WA MAJINA YA WACHEZAJI UMEPITWA NA WAKATI VIJANA JIULIZE JANA HUYO NRYMAR KAFANYA NN JANA
 
Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
16,950
2,000
Ndio shida ya vjana kujua mpira juz bas wanajikuta wachambuz wazur lakn ukwel utabak Liverpool n moja ya klabu bora ulaya kila atakaye pangiwa naye lazma atambue hilo kuwa amepangiwa na timu kisiki ACHENI USHABIKI WA MAJINA YA WACHEZAJI UMEPITWA NA WAKATI VIJANA JIULIZE JANA HUYO NRYMAR KAFANYA NN JANA

Kwani Neymar alicheza?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom