Tuchangie kwa nguvu zote hoja kwamba serkali inayo uwezo kuwalipa madaktari mshahara wanaodai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuchangie kwa nguvu zote hoja kwamba serkali inayo uwezo kuwalipa madaktari mshahara wanaodai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 1, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WanaJF:

  Tusikubali hoja hii ya JK ikazama katika akili ya Watz kwani ni ya uwongo mkubwa. Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, JK kasema serikali yake haina uwezo kuwalipa madaktari mshahara wanaotaka.

  Wapenda ukombozi - tuchangie kwa nguvu zote hoja kwamba serkali inayo uwezo kuwalipa madaktari. Kuna madudu mengi serikali ya JK inayofanya yanayotafuna mabilioni bila tija yoyote.

  Ripoti za CAG kwa mfano, kuuzwa tayari kwa gesi yetu na vigogo kuwekewa hela Uswisi etc etc.

  Tusikubali hoja hii ikapita. Ni wajibu wetu kui-derail kabla haijaondoka Ikulu. Hata yeye akibanwa na nguvu ya hoja, anaweza akakiri kwamba "ni kweli, iwapo serikali yangu ingesimamia rasilimali zetu kikamilifu, tungeweza kuwalipa madaktari hata mara mbili ya hela wanazodai."


   
 2. U

  UNO Senior Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama haukufikia wanaoudai, mimi ningeshauri angalau 1.6m, kwa kuanzia. Hivi kweli mtu kasoma miaka mitano. Intern mwaka mmoja; jumla miaka 6. Kazi yenyewe unaifahamu risk zake; anaanzia mshahara wa sh. 900,000 ikikatwa kodi labda anabakiwa na sh 700,000, akikatwa PSPS mfuko wa jamii labda unabaki 500,000. Hapa hajalipa nyumba ambayo hana wala hapewi. hapo hajapeleka mtoto shule, hapo hajala chakula akiwa kazini na familia wanangoja...Akija kurudi mtaani aliokuwa anawaacha kwa mbali darasani wanabadilisha gari moja hadi lingine, eti kwa sababu yuko TRA, Benki kuu nk. Hana nafasi ya kufanya chochote cha ziada kwa sababu ya kazi yao, wanashinda wodini. Mimi sio daktari lakini; surely this is not fair.
   
 3. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wana jf mkikataa haizuwii wala kubadili chochote
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye blue nakubaliana na wewe kabisa, tatizo ni mgawanyo mbovu wa raslimali na ubinafsi wa viongozi wetu.Kuna mambo yanafanyika ya ajabu sana katika nchi hii
   
 5. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,453
  Likes Received: 10,656
  Trophy Points: 280
  kama wanatupenda wananchi basi wajipunguzie posho iende kuwalipa wataalamu wetu na kuboresha afya zetu.
   
 6. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Serekali hii dhaifu, ikipenda na kuwa na dhamira ya dhati inaweza kabisa kabisa kuwalipa madaktari malipo manono. Bandari, Gesi, dhahabu, mbuga za wanyama, maziwa makuu, uranium, Almasi, Tanzanite, vyote hivyo kwa uchache vyaweza kuifanya Tanzania ni Pepo ya kidunia. Na watanzania tukazisahau shida zetu zooote. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
   
 7. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nani anawapangia madaktari walipwe mishahara yao?:A S-baby:
   
 8. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshahara wa madaktari ni wao wanajipangia? na kama ni serikali kwaini wasisubiri tamko la serikali ili wajue watakalo fanya?
   
 9. RUV ACTVIST.

  RUV ACTVIST. JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 471
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hoja ya msingi sio mshahara tu, tunapojadili tujadili kwa upana unaostahili, Madaktari wetu wengi wapo nje ya nchi kwa nini? Mawilayani hatuna madakatari kwa nini? Badget ya kupeleka wagonjwa nje inazidi ya kuendesha hospitali za ndani kwa nini? hamna kiongozi anayetibiwa ndani ya nchi kwa nini? haohao wanaotibiwa nje ndo wanaotuibia, hawakusanyi kodi, wansamehe kodi, wakwepa kodi, wanasign mikataba mibovu, hizi ndo hoja za msingi na ndo kiini cha mgomo.
   
 10. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unafikiri Serikali ikiwalipa Madocta na kuboresha huduma za afya kama wanavyodai, fungu la pesa za kuibiwa litapungua sana!
  Unajua nchi yetu ina wezi wengi sana kila idara. Wataiba nini? Tutahatarisha fedha za masurufu ya safari na posho! Wezi hawa hawashindwi kitu!

  Kama ujuavyo hatuna ubavu wa kudhibiti hawa wezi! sanasana wakituibia tutaomba waturudishie polepole!
  isije nchi ikatikisika na kuhatarisha Amani, Utulivu na Mshikamano wetu Watanzania
   
 11. j

  jhumbiza New Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashauri tuje na hoja zilizo-based kwenye facts na tuonyeshe implications(in figures), badala ya kuja na hoja za kishabiki ambazo hazitawasaidia drs wetu
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wakitaka kutafuta pesa watapata...wapunguze wizara ziko nyingi mno, sisi tuna mawaziri wengi kuliko nchi za ulaya zilizoendelea. Mfano kwanini tuna waziri asiyekua na wizara maalum, ni kupoteza hela tu. wapunguze wizara ili pesa badala kupelekwa kwenye wizara ambazo hata haziperform vizuri hiyo hela ipelekwe wizara ya afya na elimu.
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wakitaka kutafuta pesa watapata...wapunguze wizara ziko nyingi mno, sisi tuna mawaziri wengi kuliko nchi za ulaya zilizoendelea. Mfano kwanini tuna waziri asiyekua na wizara maalum, ni kupoteza hela tu. wapunguze wizara ili pesa badala kupelekwa kwenye wizara ambazo hata haziperform vizuri hiyo hela ipelekwe wizara ya afya na elimu.
   
 14. T

  TATOO Senior Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pesa ipo wapunguze posho za wabunge...sisi tunawajua wabunge hawana kazi ya kupewa pesa yote hiyo...na pia na kikwete naye apunguze safari za nje ataona pesa ya dr..z itatosha na itabaki kwanni anaweweseka huyu kikwete???? da kweli nyerere alikuwa anaona mbali sana...sikio la kufa halisikii dawa wananchi kwa kuwa wepesi wa kusahau tukasahau maono ya nyerere kwa kumpinga huyu jamaa kuwa kiongozi wa nchi hii....nataman kufa kiukweli kwa madudu anayosema huyu kikwete...hvi kweli hiyo ratiba amewasomea watanzania au wale wasomali na wa ethiopia wanaokimbilia malawi na africa kusini????
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio mishara Mikubwa wala ya kati wala Midogo.

  Serekali ya JK imepoteza Uwezo wa kutatua matatizo ya waanchi wake. Serekali yake imegawanyika imesambaratika Cancer terminal stage ...

  Hakuna ugumu wa Kutatua tatizo rahisi kama hilo la Ma Dr.

  Serekali lege lege haina uwezo wa ku manage na kuafikiana na Ma Dr hadi kungofoa kucha na meno yao? What a shame!!!

  Ukishaanza Kuua kama namna ya kutatua matatizo hutaacha kamwe hadi Tanzania iwe Kama Syria and yet that isnt the solution ... Wake up guys!!

  Kwani yule kijana wa TBC comedy hawezi kutatua tatizo dogo hilo la mgomo ... !!!????

  Hakuna tatizo gumu kwenye mgomo wa Ma Dr ... Tatizo ni serekali "Weak and wimpy"
   
 16. B

  BARRY JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Hivi ukiondoa madaktari, kada zingine wanataka walipwe sh ngapi?
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Ebu tuambie uongo huo upo wapi? ni uongo Madaktari hawataki 7,700,000 kwa mwezi? Serikali hawana uwezo wa kulipa hiyo mishahara subirini Chadema wachukuwe nchi mtawalipa hata milioni 20 kwa mwezi.
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ila wana uwezo wa vigogo wake kujilimbikizia mabilioni katika mabenki ya nje! Kwa nini usiongeze hilo?

  You are really coward, gamba sumpathiser, lisilokuwa na huruma kwa Watz mamilioni walio masikini!
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama JK angekuwa jasiri na mtu anayesimamia kile anachoamini, siku moja aitishe mdahalo na watu wengine wakiwemo wanasiasa na wataalamu wa kiuchumi (nikiwemo mie) na mada iwe "iwapo serikali inayo au haina uwezo kuwalipa madaktari mshahara wanaodai."

  Hawezi kuwa na ubavu wa kujibizana ki-hoja katika mdahalo wenye mada ya namna hiyo, yeye kazoea kuhutubia wazee tu wa Dar wasiojua kitu (wanakubali hata fisadi kuwa mwenyekiti wao!) ambao huwa tayari kumpigia makofi kwa lolote analosema.

  Aidha anapenda tu kubwabwaja katika speech zake za kila mwezi ambako hakuna mtu wa kumuuliza!

  I dare him aitishe mdahalo -- yeye si anajidai kujua kila kitu? THUBUTU!!!!!!
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena: Hata aje na timu ya wachumi wake!! wale walioifikisha nchi hapa ilipo!
   
Loading...