Blue G
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 5,335
- 3,652
Habarini Wadau wa MMU, suala la malezi ni changamoto sikuzote,kulea watoto halijawahi kuwa rahisi hata mara moja
tena wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,kwamba utu au tabia za mtoto wako ni matunda ya malezi yako,kama ni ukatili,upendo,huruma,uchapa kazi au uvivu vyote ni matokeo ya malezi yako(japo kuna wengine ambao licha ya jitihada nyingi ambazo mzazi hutumia bado huishia kuwa watu wa ajabu katika jamii)
Mfano kuna mahali nilisoma japo nimesahau chanzo ila nakumbuka nilisoma kuwa watoto ambao hawakuwa wakikumbatiwa mara nyingi wakiwa wachanga wanakabili ugumu wa kuonesha upendo pindi wakikua
lakini pia kuna baadhi ya watu katika stori za hapa na pale ambao wanakiri labda kumkumbatia mtoto wake,au ile mke au mume kutaka taka ukaribu wa mwili inawawia vigumu maana ni vitu ambavyo ni vigeni kwake hakuvizoea
lakini pia kuna dhana kuwa zamani haikuwa rahisi kabisa kuwa Rafiki na baba,yaani akifika kila mmoja anatafuta pa kwenda ili kulinda heshima ya baba,na hivyo kukuta watoto wakibase upendo wao Zaidi kwa mama kuliko baba
Naombeni tushare experience zetu wadau,kuna ukweli kiasi gani kuhusu swala hilii la malezi?kuna mtu anayedhani malezi ambayo mzazi anampa mtoto wake yanaweza kuathirii utu wake hapo baadae?kuna mtu ambaye anahisi malezi aliyoyapata yameamuathiri kwa namna moja au nyingine?kuna mtu ambaye anahisi hatamani kulea watoto wake kama wao walivyolelewa?
Karibuni wana MMU