Tuchangamkie fursa za kununua ardhi mapema

kivike9

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
363
250
Habarini wanajamvi, kama wewe ni muumini katika kuwekeza ardhi basi chukua hii.

Chuo kikuu cha ardhi kinatarajia kujenga chuo kishiriki kikubwa saana jijini Dodoma.

Eneo walilolenga kujenga lipo wastani wa 25km kutoka njia kuu(lami).

Wakazi na wakulima wa eneo hilo tayari washaanza kuandaliwa kwa ajili ya malipo.

Hivyo basi kwa kuwa mara nyingi sehemu ambayo chuo kinakuwepo huwa kuna fursa nyingi zinazoendana na vyuo ikiwemo biashara pamoja na nyumba.

Hivyo kununua ardhi sasa hivi ni afadhali kama wewe ni mpambanaji lakini mtaji kidogo kwa sababu kikishajengwa tayari matajiri tu ndio wanakuwa na nguvu ya kununua ardhi.

Kila la kheri katika kumeng'enya hili.

Asante
 
kivike9

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
363
250
Eneo hilo linaitwaje
Kuna njia mbili, ya kuingilia kutoka chamwino ikulu, na ya kuingilio Hombolo bwawani.

Kwa njia ya chamwino unaingilia kijiji cha msanga, kabla hujafika kilipo kiwanda cha mvinyo (cetawico) basi unakuwa ushafika.

Njia ya hombolo , ukifia hombolo unapitia kiwanda cha mvinyo kisha unaenda kama mita mia saba mbele
 
Majan

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
969
1,000
Kuna njia mbili, ya kuingilia kutoka chamwino ikulu, na ya kuingilio Hombolo bwawani.

Kwa njia ya chamwino unaingilia kijiji cha msanga, kabla hujafika kilipo kiwanda cha mvinyo (cetawico) basi unakuwa ushafika.

Njia ya hombolo , ukifia hombolo unapitia kiwanda cha mvinyo kisha unaenda kama mita mia saba mbele
Ubarikiwe chief
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom