Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Matumizi ya sheria inayohusu masuala ya uhujumu uchumi yamekuwa mabaya sana awamu ya Tano. Kati ya watu walioteswa na sheria hizi kandamizi ni viongozi wa kisiasa wenye mtizamo chanya dhidi ya wananchi na wafanyabiashara.
Hizi sheria hazijafutwa, bado zipo na zinazidi kutumika vibaya na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
Kipindi hiki Cha uchaguzi watumishi wa Umma wanapaswa kuwawazia wale waliokuwa CCM kindakindaki 2015 lakini leo wanaozea jela bila kesi zao kusikilizwa kwa wakati.
Wafanyabishara mmeona namna mambo yalivyowaendea for five years, msiwaze kuwa Sheria zimefutwa. Unaweza wafadhili wanasiasa leo lakini wakiapishwa ukaenda kuishi jela.
Wakulima na wafugaji mmejionea namna mambo yalivyokwenda, waliotunga hizo sheria ndio hao hao waliopo mtaani leo kuwaomba kura msisite kuwahoji.
Wanasiasa wa vyama vyote, mmeona mlivyopokonywa uhuru wakisema, mlivyolazimishwa kuamini msichoamini, mnao muda wakuamua hatima yenu.
Lazima wapiga kura tutake kuwa na watu watakaoleta Sheria zakusimamia haki, mtu akituhumiwa apewe dhamana kesi isikilizwe ndipo atiwe hatiani. Kumweka mtu ndani bila hata kuwa na chembe ya ushahidi kisa mmechukuliana mke au mme si sahihi hata kidogo.
Tuchague watu watakaotuletea Sheria zinazojali utu wetu. Ukipoteza haki hii leo kwa sababu za ushabiki wa siasa utajuta miaka mitano mbele. Chagua kwa kuingalia familia yako, jamii na Taifa.