Tuchague majaji kwa kuwapigia kura?

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Wandugu,

Katika pita pita hapa marekani nimekumbuna na hili suala la uchaguzi wa majaji kuanzia Court of Common Pleas mpaka Suprem Court ( Katika Ngazi ya State). Hawa wagombea wa nafasi hizi wanafanya kampeni kama kawaida na wanachangisha michango kwa ajili ya kampeni ( Kumbuka michango hii inafuatiliwa kwa karibu ...on the face of it, hakuna longo longo aka takrima).

Hawa majaji wanafanya kazi kama majaji kwa kipindi cha miaka sita kisha wanarudi tena kwa jamii zao kuomba kura ya kwenda kuhudumia umma.

Swali: Je mnaonaje hii dhana tunaweza kuipeleka Tanzania na ikafanya kazi? Je wananchi kuruhusuiwa kuwachagua mahakimu na majaji itapunguza rushwa na ubabe wa taasisi moja au mtu mmoja kuwa na maamuzi mazito ya kuteua majaji?

Naomba kuwakilisha mjadala huu,

Shadow.
 
Back
Top Bottom