Tuchague Kiswahili au Kiingereza. Tusifanye madudu

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Teknolojia ,utandawazi ni vitu ambavyo havikwepeki katika maisha yetu. Athari zake ni mpaka kwenye lugha .

Haya maneno yamekuwa yakitumika isivyo na wadau wengi na wengine ambao unategemea kuwa wameenda enda shule kidogo wawe wamebadilika.

Leave- neno la kiingereza maana yake ondoka, acha n.k

Mtu anapokuwa kwenye group la whatsapp akajiondoa inakuwa - Boribo has left au kifupi tu Boribo Left.

Left ni past na present participle ya leave. Yaani. Leave, Left, Left kama Break, Broke, Broken.

Kwa lugha sahihi ulitakiwa usema Boribo has left au Boribo left the group. ukirudisha kwenye kiswahili basi iwe Boribo ame leave the group. Au nimeamua ku leave lile group la whatsapp na siyo nime left.sema nme leave .

Maneno kama.
Dunia haipo Fare X - ni Fair
Njoo tu ChaRt X - Chat
Kwani hapo uta Loose nini X - Lose
Jana nme Loose wallet yangu X- Lose

Loose - legeza
Lose - poteza

Ukiacha wale wengine wapuuzi wanaoandoka.

Xawa - badala ya Sawa
Bana - bwana

Kuna mengi ambayo mtu anaweza akaandika ukaona ana reveal kichwani ana nini. Kukosea lugha ya kiingereza si dhambi. Najua ni lugha ya wenyewe basi tuchague pale ambapo hatulazimishwi tutumie kiswahili chetu ni lugha nzuri tu mbona?

Mbaya tunapokosea kiswahili , na tunapokosea kiingereza.
 
Kila kitu kina umuhimu wake.
Kiingereza kinahitajika kwani ni official language ya ulimwengu.
Kiswahili kinahitajika kama lugha ya kuwaunganisha watanzania wote and Swahili speaking countries.

NB: Kulingana na eneo lako la specialization fanya kile unachopaswa kufanya ila English and Swahili are basic languages in our nation.
 
Teknolojia ,utandawazi ni vitu ambavyo havikwepeki katika maisha yetu. Athari zake ni mpaka kwenye lugha .

Haya maneno yamekuwa yakitumika isivyo na wadau wengi na wengine ambao unategemea kuwa wameenda enda shule kidogo wawe wamebadilika.

Leave- neno la kiingereza maana yake ondoka, acha n.k

Mtu anapokuwa kwenye group la whatsapp akajiondoa inakuwa - Boribo has left au kifupi tu Boribo Left.

Left ni past na present participle ya leave. Yaani. Leave, Left, Left kama Break, Broke, Broken.

Kwa lugha sahihi ulitakiwa usema Boribo has left au Boribo left the group. ukirudisha kwenye kiswahili basi iwe Boribo ame leave the group. Au nimeamua ku leave lile group la whatsapp na siyo nime left.sema nme leave .

Maneno kama.
Dunia haipo Fare X - ni Fair
Njoo tu ChaRt X - Chat
Kwani hapo uta Loose nini X - Lose
Jana nme Loose wallet yangu X- Lose

Loose - legeza
Lose - poteza

Ukiacha wale wengine wapuuzi wanaoandoka.

Xawa - badala ya Sawa
Bana - bwana

Kuna mengi ambayo mtu anaweza akaandika ukaona ana reveal kichwani ana nini. Kukosea lugha ya kiingereza si dhambi. Najua ni lugha ya wenyewe basi tuchague pale ambapo hatulazimishwi tutumie kiswahili chetu ni lugha nzuri tu mbona?

Mbaya tunapokosea kiswahili , na tunapokosea kiingereza.
mm huwaga napata shida moja,kw mfano,nmb ni kifupi cha "national microfinance bank" sasa mtu anaposema tukutane nmb bank inakuwaje??ina maana angeamua kulitamka neno kw kiref chake angesema tukutane national microfinance bank bank??????
 
Fungua mlango wa emergency door
 
Fungua mlango wa emergency door
hahahahaaaaaa hahahahaaaaaa,kw kweli ni shida tupu,halaf viumbe tumeshayafanya haya makosa ni common sana halaf ikawa ni kawaida,nmecheka kwny mlango wa emergency door
 
Hahaha kuongea kiingereza kama huna pesa/hela ni bora kuongea kimakonde tu.
Hiyo tafsiri ya watu wa jamii yangu. Yani kwao kiingereza=elimu =pesa.
 
hahahahaaaaaa hahahahaaaaaa,kw kweli ni shida tupu,halaf viumbe tumeshayafanya haya makosa ni common sana halaf ikawa ni kawaida,nmecheka kwny mlango wa emergency door
Neno - panic linamaanisha "sudden fear". lakini mara nyingi nakutana namarafiki hulitumia kama linamaanisha ku kakasilika au "furious" kwa kiingereza.....na kosa amani kwao kabisa tena niwasomi
 
Umebugi mzee, hakuna cha ame leave ni ame left (ambayo ni PP na PT kwa kuwa kitendo kimeshatendeka)

Kiswahili kilituunganisha kama Watanzania, tungetumia Kiingereza shuleni tusingekuwa,na utangamano kama sasa kwa kuwa kiingereza ni kigumu na watu wangebaki na vilugha vyao

Ila kwa sasa utengamano tayari upo wa kutosha na tukifanya elimu yote kwa Kiingereza ndio bora ili ku catch up na speed ya dunia ya utandawazi
 
mm huwaga napata shida moja,kw mfano,nmb ni kifupi cha "national microfinance bank" sasa mtu anaposema tukutane nmb bank inakuwaje??ina maana angeamua kulitamka neno kw kiref chake angesema tukutane national microfinance bank bank??????
NMB ni brand mkuu,kama Cocacola vile

Yaani ulitaka aseme tukutane NM bank? Au tukutane benki ya NM? Asingeeleweka

Lazima ataje NMB ili ijulikane ni benki ipi, na akisema NMB bila kumalizia benki pengine haitatosha maana waweza kuta kuna vitu vingine vinaitwa NMB pia

So sentensi isiyoacha maswali na kueweka ni benki ya NMB
 
Umepitwa kidogo. National Microfinance Bank imebadilishwa jina na kuwa NMB BANK. Pia CRDB imebadiliahwa na kuwa CRDB BANK.
 
NMB ni brand mkuu,kama Cocacola vile

Yaani ulitaka aseme tukutane NM bank? Au tukutane benki ya NM? Asingeeleweka

Lazima ataje NMB ili ijulikane ni benki ipi, na akisema NMB bila kumalizia benki pengine haitatosha maana waweza kuta kuna vitu vingine vinaitwa NMB pia

So sentensi isiyoacha maswali na kueweka ni benki ya NMB
nmekuelwa mkuu,niambie basi pale ambapo ww utaamua kutotumia abbreviation( NMB) na ukaamua kutumia kiref chake,utainclude na hilo neno na kusema "tukutane national microfinance bank bank" kwa sabb national microfinance bank ni brand????
 
Kuna member hapo juu kasema NMB siku hizi imebadilisha jina inaitwa NMB Bank, nime search mtandaoni ni kweli inaitwa hivyo sio NMB tu, nadhani wenyewe waliona ni muhimu kuifanya hivyo sababu ya watu kulitumia sana, wakaona ni convenient jina rasmi liwe hivyo....japo ukiitaja kwa kirefu ndio hivyo inakirudia maneno
 
Neno bugi nadhani umelitoa kwenye neno boogie - hili ni neno la kiingereza sisi tunaoifaham lugha tutakwambia maana yake ni- kucheza music wa rock au pop na pia ni kifaa kama piano cha music.

Sasa kama tu neno hili dogo hujui matumizi yake unapoteza kabisa credibility ya kuzungumzia lugha.

Boogie ni verb- kitenzi/kitendo ambalo hilo neno past tense yake ni boogied.
Sasa kwa nini usisema
Ume- boogied? Unasema ume boogie?
Ila unataka kusema
Ume- left badala ya ume leave ?

Haya mambo waachie wanaojua ku reason na wenye ufaham wa lugha.ukileta ujana ujana utaajiabisha tu.

Huelewi ungetulia ungepata darsa. Ame - ni kauli ya wakati uliopo kamilifu. Ame - ondoka
Ukitumia kiswahili na kiingereza unapaswa uwe unazifaham lugha zote mbili vizuri.kaa kitako nikuelekeze bure kabisa.

Left- wakati uliopita wa leave.
He left - aliondoka
Leave - ondoka
Ame leave yaani ame-ondoka
Ungesema kwa kiswanglish ameeenda ungesema ame -go = ameenda
Ame- come = amekuja
Ana - eat = anakula
Ame - eat = amekula

Ame- hii tayari inaelezea wakati uliopo kamilifu kwenye kiswahili
Otherwise tumia kiswahili tu moja kwa moja kuwa
Ameondoka au english moja kwa moja kuwa
They have left.

Back
Top Bottom