Tubuni Mbinu Zetu za Kuwatangaza Mashujaa wetu wa Afrika akiwemo JK Nyerere

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,640
0
Ndugu Wanabodi,
Kila mtu aliyekuwa akifuatilia mazishi ya Nelson Mandela pale Qunu, Eastern Cape, Afrika ya kusini, atakubaliana nami kwamba Mh. Kikwete alitumia vizuri jukwaa lile kuieleze dunia mazuri ya Tanzania na Mwl. Nyerere katika ukombozi wa Afrika ya Kusini. Aliyosema ni mambo ambayo aidha yanonyesha kutokutiliwa manani na Mataifa ya magharibi ambayo wamekuwa wakimtangaza Mandela kama the greatest son of Africa. Hii ilionyesha pia Mh Kenneth Kaunda, raisi mtaafu wa Zambia. Hii inatokana na mapenzi Ulaya na Amerika kwa Mandela kinyume na Mwl Nyerere. Ukweli utabaki palepale kwamba Mwl. JK Nyerere ndo the greatest son of Africa.

Ili kuweka historia vizuri, nigependa tufikirie jinsi ya kuwatangaza viongozi wazuri kwetu Afriaka ambao obvious hawatapendwa na Ulaya na Marekani kwa sababu ya kukataa kuwa puppets.

1) Wasomi wetu waandike vitabu vingi na vizuri vya historia kama alivyoieleza Mh. Kikwete katika lugha mbalimbali na kuviuza duniani kote.
2) Wataalamu wa media wandae documentaries na cinema za JK Nyerere katika lugha mbalimbali na kuziuza au kuziweka katika Youtube.
3) Tuhakikishe kwamba panapokuwepo picha Mandela, asikosekana picha ya Nyerere ambaye atakuwa mbele au juu ya picha ya Mandela kuonyesha kwamba bila Nyerere Mandela asingekuwa vile.

Na mambo mengine kama hayo.

Watanzania na Waafrika wote, tutakaa kulaumu kwamba viongozi wetu hawatangazwi kwa sababu tunategemea tutagaziwe viongozi wetu. Mandela ametangazwa na Ulaya na Amerika kwa sababau amewapa ulaji wa kweli. Nasi tutangaze wapinganaji wetu wenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom