Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 789
Ndugu Watanzania wenzangu,
Kama Mjuavyo majina ya Miji, Mito,barabara n.k yapo yale ya asili na yale ambayo tumebadilisha kwa aidha kumuenzi kiongozi fulani au sababu nyingine yeyote ikiwa pamoja labda na kugawa mikoa na Kadhalika. Mfano... Pugu Road, leo Inaitwa Nyerere Road, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (DIA) leo Unaitwa Julius Nyerere Inter. Airport (JNIA) Mabadiliko mengi yaliyofanyika ya majina kabla ya leo hii ni kwa sababu za Kisiasa na Kijamii...
Leo hii nakuja na hoja ya Kubadilisha Jina la Jiji la Arusha kwa nia ya Kibiashara au Kiuchumi. Na napendekeza majina haya mawili... aidha jiji lile liitwe Kilimanjaro au liitwe Serengeti.
Nitazungumzia Jina la Kwanza zaidi yaani Kilimanjaro kwa kuwa jina la pili ni kwa ajili ya fall back plan tu!!!
Sababu ya kusababisha kuomba watanzania waridhie mabadiliko hayo ambayo najua yako chini ya TAMISEMI, Mhe. Rais Mwenyewe, Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha, pamoja na Wananchi wote wa Tanzania kwa Ujumla ni hizi zifuatazo:-
A. Kwa kuwa Watani wetu hawapendi kwa makusudi kabisa kusema Mlima Kilimanjaro uko Tanzania!!! (pam9oja na kwamba hawasemi uko Kenya).
B. Kwa kwa Mji wa Arusha ni Makao makuu ya Afrika Mashariki.
C. Kwa kuwa mikutano mingi ya Kikanda na Kimataifa itafanyika kwenye jiji la Arusha
D. Kwa kuwa ujenzi wa Nyumba umefanya sasa Mji wa Moshi na Jiji la Arusha kuunguna kabisa na hata usitambue mipaka kwa urahisi.
E. Kwa kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro pia uko katikati ya Mkoa wa Kilimanjaro na Jiji la Arusha.
F. Kwa kuwa tuna mji wa Moshi mpaka sasa na Hatuna mji unaitwa Kilimanjaro.
G. Kwa kuwa Jina la Arusha halina manufaa yoyote ya Kiuchumi zaidi ya kwamba ni jina la kuridhi tu, kwa maana halitangazi Mbuga ya Manyara, Serengeti, Ngororo au Mlima Kilimanjaro etc.
Napendekeza mipaka ya Mkoa wa Kilimanjaro na Mkoa wa Arusha iangaliwe upya ili, Mji wa Moshi na Halimashauri ya Jiji la Arusha... iwe jiji moja kwa Jina la "Kilamanjaro" Kwa maana pale city centre Arusha na Moshi paitwe Kilimanjaro City. Wilaya za Moshi vijijini, Rombo, Mwanga, Same etc... zawezapewa jina lingine na kuwa mkoa mwingine... Na wilaya za Meru...Serengeti etc.. Zawezapewa Jina lingine.... na kituo cha Mikutano cha Arusha kitaitwa Kilimanjaro International Conference Centre.. KICC... sorry naona inaanza kufanana na Kenyatta inter. conference centre... lakini inaeleweka..
Kwanini Basi napendekeza Hivyo.
Kwa kubadili Jiji la Arusha kuitwa,, Jina Kilimanjaro litatajwa sana duniana, na hivyo kufanya dunia kukumbushwa kwamba Kilimanjaro iko Tanzania. Hivyo kukuza Utalii wetu na Kuleta mapesa kibao.
Wale watakaopinga nawakumbusha jambo moja hivi ukiwa Ulaya/Amerika ukisema naenda Unguja au Pemba utaeleweka... lakini je Ukisema Unaenda Zanzibar?
Hivi ukiwa Ulaya ukisema naenda Moshi, Arusha unaelewaka haraka... Je ukisema Naenda Kilimanjaro... iko tofauti...
Haya wadau jadilini...
Kumbukeni Wenzetu South Afrika wanabadilisha majina ya miji yao... lakini wao ni kwa ajili ya kukumbusha historia... kwa hiyo uwanja wa Johannesbur Inter. Airport sasa ni Oliver Tambo Intertional Airport etc...
NB: Kama mtakataa kuliita Kilimanjaro basi liiteni basi Serengeti kuliko sasa ambapo jina hili(Arusha) halina mvuto wowote wa Kibiasha/Kitalii/Kiuchumi