Tubadilike. VVU/UKIMWI havitakuja kuisha kama tutaendelea kuendekeza haya

gasgas

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
1,090
978
Habari za asubuhi. Ni matumaini yangu wenzangu ni buheri wa afya.

Kuna hii kitu nilikuwa natafakari jinsi hali ilivyo kwa sasa katika jamii yetu. Kuna trend ambazo naziona ambazo zinaturudisha nyuma katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.

UKIMWI upo jamani. Sisi tunaofanya kazi sekta ya afya tunathibitisha hilo. Yes, hauzungumziwi sana kama hapo zamani na upatikanaji wa dawa unasaidia kupunguza makali ya ugonjwa ila ugonjwa upo na watu wanazidi kuambukizwa kila siku.


Baadhi ya vitu nilivyogundua:
1. Ongezeko la watu kutotumia kinga hata pale ambapo wanakutana na mtu mpya. We nenda tu uzi wa kimasihara hesabu watu wangapi ambao walitumia kinga, ni wachache. Lakini pia kuna wale ambao wananunua kinga lakini utamu ukikolea anatoa au anaamua kwenda kavu kavu.
Mnajiweka katika hatari kubwa sana ndugu zangu.

2. Ongezeko la wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume. Men having sex with men (MSM). Hili suala watu hawapendi kulizungumzia ila lipo. Na baadhi ya watu wanaopinga ushoga kwa maneno unakuta nyuma ya pazia wanashiriki kwa namna moja au nyingine.

Mwaka 2014 hivi, professa wetu mmoja pale chuo alipresent pepa yake na moja ya vitu alivyogundua katika tafiti ni kwamba hapa Tanzania 20+ % ya wanaume wameshashiriki au wanaendelea kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Ina maana katika wanaume 5. Mmoja wao ameshawahi au anaendelea kushiriki. Hii inahusisha vijana wadogo wa kiume, vijana ambao hawajaoa, vijana waliooa na hata wenye familia, wazee pia.

Ingia tu mitandao ya dating kama tinder, badoo n.k utajionea jinsi ambavyo vijana wengi wa kiume wanajinasibu tena bila kificho.

Miaka ya mwanzo wakati UKIMWI unaanza, ulikuwa unatambulika kama ni ugonjwa wa mashoga maana wai ndio walikuwa wanaingiliana kinyume na maumbile tena bila kinga.


3. Hali imebadilika kwa sasa. Idadi ya watu wanaopenda kufanya mapenzi kinyume na maumbile imeongezeka kwa kasi ya kimbunga. Mbaya zaidi watu wanafanya bila kinga na bila kujua hali ya kiafya ya mtu anayefanya naye.

Kutengeneza michubuko ya huko topeni ni rahisi sana. Anal sex ina one of the highest risk kuambukiza VVU. Lakini watu wanaona ujanja siku hizi

4. Uwepo wa kundi la watu ambao hawapimi afya zao na bado wanaendelea na ngono zembe. Ina maana kama mtu ana maambukizi hawezi kujua, hataanza dawa. Walau ukitumia dawa unapunguza kiwango cha virusi kwenye damu na hivyo kushusha uwezekano wa kuambukiza mtu mwingine. Lakini hali haipo hivyo. Watu hawataki kupima

5. Watu kutotumia dawa kwa usahihi. Dawa za ARV zikitumika vyema husaidia kushusha kiwango cha virusi kwenye damu, husaidia kinga ya mwili kupanda, hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa nyemelezi. Lakini watu hawataki hiyo. Mwisho wa siku wanakuja hospitali wakiwa na stage 4 HIV associated diseases na wengine huwa ndio mwisho wao.

Tubadilike jamani, uamuzi upo katika mikono ya kila mmoja wetu. Jikinge mkinge na mwenzako.

Uzi tayari

Sent using .... who cares anyway
 
Well said,atakayesoma na abadilike haraka na kuwaelimisha wenzake.Watu waache huu upuuzi wa mapenzi bila kinga,(Anal sex)Mapenzi ya njia ya haja kubwa ,huu sio ujanja hata kidogo .

Vile vile siku hizi maambukizi ya homa ya ini Hepatitis B(Silent killer disease) nayo yamezidi kupanda nayo yanaambukizwa kwa njia zinazofanana na za ukimwi.

Be careful Life is too short.
 
Hivi ukiwa kama daktari unafikiri ni kweli dawa ya ukimwi haipo..?
Maana kumekuwa na nadharia nyingi kuhusu ugonjwa huu!!

Je,wizara ya afya bado inaendelea kutafiti na kutafuta dawa au na wenyewe wamekaa tu....??

Hao washenzi wanaofurahia ushenzi ingefaa tuwauwe tu! Maana hawana tofauti na shetani muandamizi
 
Kuna mjamzito alikua positive na alikua hataki kutumia dawa. Kwa bahati alijifungua mapacha, alipopewa dawa ya pmtct kwa ajili ya watoto akaondoka nazo ila hakuwapa na anaendelea kunyonyesha. Mume aliamua kumuacha na kulea watoto mwenyewe.
 
Kweli mkuu! Ukimwi bado ni janga tahadhari ni muhimu sana.
 
.....Nawapa salamu za dhati wale wote tunaokutanaga Sinza mori na corner bar.:mad::mad::mad:
Watu wanaambukizwa sana huko.
Hawa wanaojiuza wengi wameshajikatia tamaa ya maisha.

Wakiombwa kupigwa kavu wanakubali kama kawaida

Sent using .... who cares anyway
 
20% ya wanaume wa Kitanzania wamewahi shiriki ulawiti?

Hii takwimu sidhani kama ina ukweli...hii ni namba kubwa sana aisee

Mwaka 2014 hivi, professa wetu mmoja pale chuo alipresent pepa yake na moja ya vitu alivyogundua katika tafiti ni kwamba hapa Tanzania 20+ % ya wanaume wameshashiriki au wanaendelea kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Ina maana katika wanaume 5. Mmoja wao ameshawahi au anaendelea kushiriki. Hii inahusisha vijana wadogo wa kiume, vijana ambao hawajaoa, vijana waliooa na hata wenye familia, wazee pia.
 
20% ya wanaume wa Kitanzania wamewahi shiriki ulawiti?

Hii takwimu sidhani kama ina ukweli...hii ni namba kubwa sana aisee
Ni tafiti na imekuwa published 2014 pubmed, hinari

Sent using .... who cares anyway
 
Ugonjwa hauwezi kuisha tatizo ugonjwa umekali mahali pabaya sana kwenye utamu kila mtu ni mdhaifu sana sehemu ile.
 
Back
Top Bottom