Tubadilike! Mfumo wa kupata viongozi mbalimbali TZ si mzuri. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tubadilike! Mfumo wa kupata viongozi mbalimbali TZ si mzuri.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mo-TOWN, Jul 23, 2011.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Mfumo mbovu wa kupata viogozi ndani ya CCM, serikalini na swala la viogozi kutowajibika kwa wananchi umechangia sana kudumaza maendeleo ya nchi hii.

  Kinachoshuhudiwa sasa ktk makundi mbalimbali ndani ya CCM kuelekea 2015 kinasukumwa zaidi na tamaa ya wana CCM kupata madaraka ndani ya chama na serikalini kutokana mfumo unaotumika sasa.

  Mfumo unaotumika sasa wa kupata viongozi unazingatia zaidi nani yuko kundi gani/anamsupport nani. Mwisho wa siku kundi linaloshinda (mara zote ni kwa mizengwe)linaunda serikali kutokana kundi lake zaidi na uswaiba.

  Kwa hiyo tunaona kuwa mwisho wa siku its about kundi fulani. Kwa hiyo kama kuna mtu anauwezo mfano ilivyotokea kwa Kigoda na yuko nje ya kundi husika basi hashirikishwi ktk uongozi...matokea tunapata viongozi ktk kada mbalimbali ambao hawana uwezo kiutendaji wanapata fursa muhimu za kuwatumikia wananchi wakati uwezo wao ni mdogo (mfano Guninita) na baya zaidi allegiance yao ina kuwa ni kiongozi na si kwa wananchi. Hapa kuna mawaziri, wakuu wa mikoa, wenyeviti wa mikoa na makatibu CCM (mfano Mary Chatanda) etc

  Wote tu mashaidi tunashuhudia kila siku bungeni kwa viongozi kusifiana. Wabunge (hasa wa CCM) kuwasifia raisi, WM, mawaziri etc. Kitendo hiki hakifanywi kwa bahati mbaya, mbunge ana matatizo kibao jimboni kwake yet anachofanya ni kumsfia waziri in anticipation say ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa bodi fulani. Kauli kama raisi au waziri anaangushwa na watendaji wake (Beatrice Shelukindo and others) ni za kinafiki zaidi zenye lengo la kujitenezea majina mbele ya viongozi wakati fursa za uongozi zinapojitokeza.

  Nimalize kwa kusema kuwa mfumo ulipo sasa na unaotumika na CCM na serikali yake hauzingatii competence za wahusika kiutendaji bali unazingatia zaidi uswaiba(mfano Ngeleja). Ni wakati sasa kama nchi tubadilike (hii ni fursa kwa upinzini) tuwe na vigezo makini ktk kupata viongozi vinavyozingatia uwezo na si nani ni nani.
   
Loading...