Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,912
Tufike mahali tupambane na chanzo cha matatizo na si kusubiri kupambana na matokeo vinginevyo mambo haya hayawezi kwisha wala kupungua.
Eneo mojawapo ni hili la mtu kutumia vibaya madaraka yake na muathirika wa matumizi mabaya ya madaraka anapokwenda mahakamani na kufungua kesi na kushinda,serikali ndio inatakiwa kumlipa mtu huyo fidia na wala si afisa wa serikali aliehusika.
Nadhani wakati umefika tubadili sheria ili afisa atakaethibitika kusababisha kwa uzembe serikali kudaiwa fidia wajibike kulipa na akishindwa akatwe asilimia 30 ya mshara wake mpaka hela yote iliyolipwa na serikali irudi na akishindwa akatwe asilimia 50 ya mafao yake ya kustaafu na kiasi kinachobaki ndio apewe.
Sometimes watu wanakuwa na viburi,jeuri na wasiotaka kufuata ushauri wa watalaam kwasababu wanajua lolote litakalotokea ni ofisi yake/serikali ndio itawajibika kulipa na si yeye kama yeye.
Huu nao ni ufisadi tu kama ufisadi mwingine.
Kama kijana anaetoka masomoni leo hii anakatwa asilimia 15 ya mshahara ghafi wake(basic salary) ili kulipia mkopo wa Bodi ya Mikopo,ni kwanini afisa mwandamizi wa serikali anaetia hasara serikali kwa uzembe asikatwe asilimia 30 au hata 40 ya mshahara wake kulipia sehemu ya fidia aliyoisababisha?