Tubadili mfumo wa kufundisha hesabu Tanzania

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Tujadiliane,

Ufumbuzi wa ugumu wa kufundisha somo la hesabu Tanzania umeshindikana na kufanyika janga la taifa.

Nadhani warasimu waliokasimiwa jukumu la kuleta mfumo rafiki wa ufundishaji hesabu wamejipa dhima hiyo kwa kujihesabia haki ya uelewa wa somo hilo kuliko wengine ambao wangestahili kuwapa ushirikishwaji. Hili peke yake ni tatizo kama lilivyo tatizo la ufundishaji hesabu.

Kadri mtaala wa hesabu unavyobadilishwa tangu 1967 tatizo limeendelea kubaki kama lilivyo kwamba hesabu inawawia wanafunzi wa ngazi zote za elimu ugumu wa kulisoma.

Gharama nyingi zimetumika katika mchakato wa maboresho ya mtaala wa somo la hesabu (yakiwemo masomo mengine) lakini tija ni ndogo sana. Mkwamo wa upatikanaji mfumo rafiki wa kufundisha hesabu hauna utofauti na mkwamo wa Katiba mpya Tanzania.

Ninaamini siyo idadi kubwa ya Watanzania kihivyo hawawezi (wanahofu) somo la hesabu bali ni ufumbuzi wa tatizo umetengeneza tatizo lingine kwenye mchakato wa kutafuta ufumbuzi.

Kwa maoni yangu, nashauri haya yafanyike hata kama ni kwa majaribio (pilot) kwa miaka 5:

1. Wanafunzi wote kwa hatua ya msingi wafundishwe kwa ulazima Mathematical Operations za kuongeza, kutoa, kugawa na kuzidisha, kwa sababu hizi hazikosekani kwenye aina (mada) zote za hesabu kwa ngazi zote za elimu zilizopo duniani.

2. Kwakuwa hesabu ni mtambuka kwenye masomo mengine na ni pana sana, wanafunzi wasibebeshwe zigo lote hilo bali waruhusiwe kubobea kwenye aina fulani ya hesabu ambayo wana uwezo nayo kuanzia ngazi za chini za elimu na kwenye somo la hesabu wasome aina hiyo hiyo pekee hadi hata ngazi ya uzamivu (PhD).

3. Namba 2 hapo juu ikitekelezwa kwa umakini unaoustahili, wanaobobea kwenye hesabu watamaliza mtaala wa hesabu hadi wa chuo kikuu kwa miaka michache ilhali masomo mengine yatakuwa labda yakirefuka muda wake.

4. Wanafunzi waruhusiwe kubobea kwenye mojawapo ya aina (mada) za hesabu zilizopo duniani mfano:-

a) Arithmetics
b) Algebra
c) Geometry
d) Trigonometry
e) Statistics
f) Word Problem nk.

5. Kanuni ya uumbaji inathibitisha kwamba kila binadamu ana kitu anachokiweza. Hivyo kati ya hizo aina (mada) za hesabu lazima tutapata wanaowezea kila mojawapo.

6. Ninaamini kwa hii hypothesis niliyopendekeza, taifa litakuwa na mabingwa wa hesabu kuliko wakati wowote ule katika historia yake, na ari ya kusoma na kufundisha hesabu itaongezeka maana mwanafunzi atasoma anachoweza na anachopenda katika somo la hesabu.

7. Kenya CBC (Competency Based Curriculum au ufundishaji mahiri) yao imedrop baadhi ya mada (topics) za hesabu tangu ngazi za awali za elimu.

8. Hata Isaac Newton hakuwa anajuwa mada zote za hesabu kwenye maisha yake lakini bado anaheshimika duniani kama mtaalam wa hesabu na fizikia. Ni vivyo hivyo kwa Pythagoras (Baba wa Pythagorean Theorem), Muhammad Al-Khwarizmi (Baba wa Algebra), Euclid (Baba wa Geometry), Hipparchus aliyegundua table of chords kwa mara ya kwanza na kuzaa Trigonometry, John Graunt na William Petty waliogundua Statistics, Brahmagupta (Baba wa Arithmetics), na Brahmagupta & Bhaskara waliogundua Fractions.

9. Kwa hypothesis hii taifa litazalisha walimu wabobezi na mabingwa wengi sana wa somo la hesabu.

10. Serikali iondokane na hulka ya kuogopa kujaribu jambo. Woga wako ndiyo mtaji wa adui yako.

Tujadili mada kwa mustakabali wa nchi yetu.

Screenshot_20230220-233053.jpg
 
Una hoja ya msingi, kijana wangu amefanya vizuri kwenye mitihani yake ya form four lakini mathematics amefeli.

Ukiangalia matokeo yake haliingii akilini masomo mengine apige ABC halafu Mathematics apate F, hili haliingi akilini Kwa mtu mwenye akili, kuna tatizo.
Hata hao wanaofaulu hesabu siyo kwamba wanaliweza somo la hasha, walimu wamegundua mbinu chafu ya ufundishaji ambayo ni hatari kwa taifa kwamba wanafunzi wakikaribia NECTA na bado somo ni gumu kwao, wanachofanya walimu kwa muda huo unaobaki ni kufundisha mbinu za kufaulu mtihani tuuu... na siyo kufundisha kuelewa hesabu na mwisho wa siku Mwl anazawadiwa kwa kufaulisha hesabu.

Hii ni hatari kwa taifa kwa sababu tunakuwa na mtu aliyepata A ya hesabu lkn ukimpa hesabu hizo hizo tena anapata F, kumbe alikaririshwa mbinu za kufaulu NECTA tuu.
 
Una hoja ya msingi, kijana wangu amefanya vizuri kwenye mitihani yake ya form four lakini mathematics amefeli.

Ukiangalia matokeo yake haliingii akilini masomo mengine apige ABC halafu Mathematics apate F, hili haliingi akilini Kwa mtu mwenye akili, kuna tatizo.
Na Mimi Nina kijana wangu anafaulu hisabati TU mengine yote F..YAANI maths A lakini mengine F...shida sijui Iko Iko wap?
 
Wakati mmoja nikiwa mwanafunzi sikuwahi kujua kama somo la Hisabati ni gumu kama watu wanavyolizungumzia.

Niliona ni somo la kawaida tu na nilikuwa interested nalo sana, hata kama sikupata A ni kwa vile sikuwa na juhudi tu za kulisoma somo lenyewe kwa bidii ( michezo nayo ilichangia hapa wakati ule)

Ugumu wa somo la Hisabati huenda unaanzia kichwani kwa mwanafunzi kwa kiasi kikubwa. Kuna kijana amenambia yeye anataka kusomea sheria hapo baadae, hivyo haitaji kusoma saaana somo la hisabati(ndio mtazamo wake huu kwa sasa)

Tuwajengee watoto interest ya somo la Hisabati kupitia mfano, 'games' zinazohusiana na concept yoyote ya mada katika somo la Hisabati. Kwa kufanya hivi tutawapata watoto wa kuwafundisha.

Baada ya kuwapata watoto wa kuwafundisha, sasa tutumie njia stahiki za ufundishaji kuwafundisha watoto wetu.

Naamini kwa mada hizi hizi zilizopo kwenye muhtasari wa sasa wa somo la hisabati watoto wataanza kuelewa vyema na kufanya vizuri.
 
Wakati mmoja nikiwa mwanafunzi sikuwahi kujua kama somo la Hisabati ni gumu kama watu wanavyolizungumzia.

Niliona ni somo la kawaida tu na nilikuwa interested nalo sana, hata kama sikupata A ni kwa vile sikuwa na juhudi tu za kulisoma somo lenyewe kwa bidii ( michezo nayo ilichangia hapa wakati ule)

Ugumu wa somo la Hisabati huenda unaanzia kichwani kwa mwanafunzi kwa kiasi kikubwa. Kuna kijana amenambia yeye anataka kusomea sheria hapo baadae, hivyo haitaji kusoma saaana somo la hisabati(ndio mazamo wake huu kwa sasa)

Tuwajengee watoto interest ya somo la Hisabati kupitia mfano, 'games' zinazohusiana na concept yoyote ya mada katika somo la Hisabati. Kwa kufanya hivi tutawapata watoto wa kuwafundisha.

Baada ya kuwapata watoto wa kuwafundisha, sasa tutumie njia stahiki za ufundishaji kuwafundisha watoto wetu.

Naamini kwa mada hizi hizi zilizopo kwenye muhtasari wa sasa wa somo la hisabati watoto wataanza kuelewa vyema na kufanya vizuri.
Kweli mkuu.

Ila nadhani tuanze ku-narrow-down hesabu tangu ngazi za awali.

Tutajikuta tunazalisha akina Newton na Pythagoras wengi sana.

Mwanafunzi asome ambacho akili yake inaweza na anachokipenda tangu kwenye msingi.
 
IPI namna nzuri ya kumjengea mtoto interest ya masomo flani moreso hesabu.?
Waongoze watoto katika kubuni michezo waipendayo inayohusiana na mada mbalimbali katika somo. Tumia mbinu ya kuwafundisha kupitia games na mshindi atambuliwe, hata kwa kupigiwa makofi tu.

Uzuri wa games nyingi huwa ni competitive in nature, hivyo mtoto anaweza kufikiri vizuri huku akiwazia kushinda game, wakati huohuo kumbe anajifunza jambo automatically.
 
Una hoja ya msingi, kijana wangu amefanya vizuri kwenye mitihani yake ya form four lakini mathematics amefeli.

Ukiangalia matokeo yake haliingii akilini masomo mengine apige ABC halafu Mathematics apate F, hili haliingi akilini Kwa mtu mwenye akili, kuna tatizo.
Mi kuna dogo ana 1.12, F ya physics na D ya hesabu ni kihoja kweli asee
 
Back
Top Bottom