SoC01 Tubadili mfumo wa elimu ili tulete mageuzi nchini

Stories of Change - 2021 Competition

Bravo55

New Member
Sep 8, 2021
1
1
Elimu ni ukombozi wa umaskini, hii nukuu kutoka kwa baba wa Taifa mwalim Nyerere, kutokana na kwamba Elimu iwe lazima na bure kwa kila mmoja awe na haki ya kuipata ili ajikomboe kiuchumi na kifkra.

Lakini leo hii tunapoizungumzia Elimu Tanzania imekua ni taasisi moja isiyokua na uwezo tena wa kuzalisha wasomi wanaoenda na wakati kuanzia awali mpaka vyuo vikuu. Kwanza kabisa kudharauliwa kwa skuli za serikali, si ajabu ukamkuta waziri mwenye dhamana ya Elimu nchini au yoyote ukamuona mtoto wake akisoma skuli za serikali Bali wote wamewapeleka skuli za binafsi ili wapate Elimu bora, hapa utaona wenyewe dhamana na Elimu na viongozi wanaoihubiri Elimu lakini bado wameidharau elimu wanayoishughulikia na kuwaacha watoto wa wananchi maskini wapambane chini ya mifumo duni ya Elimu isikua na viwango wala ubora, skuli zimekosa madarasa na vitendea kazi vya umuhimu. Jambo la pili mifumo mibovu ya Elimu nchini, baada ya kujua kua Elimu ni taasisi muhimu katika kuleta mageuzi nchini lkn bado hakuna mageuzi yanatokea kila leo na kubakia kama nyimbo tu bila ya kuchukuliwa hatua stahiki za kutatua tatizo.

Baada ya kuangalia matatizo mawili makuu ya kielimu Tanzania, sasa tugeuze mifumo ya Elimu ili tulete mageuzi nchini. Kwanza kabisa Elimu ya shule lazima iishie ngazi ya kidato cha nne, hakuna haja ya kuendelea na kidato cha tano na sita maana sjaiona faida yake madala ya kupoteza mda tu na kuyarejea Yale Yale ya kidato cha nne, mwanafunzi alomaliza kidato cha nne na kufaulu aendlee na masomo ya chuo kikuu na wale wote waloshindwa kujiunga na vyuo vikuu wapelekwe vyuo vya uzalishaji na ufundi ili tuzalishe wazalishaji wengi kuliko kuengeza wasomi waso na faida yoyote.

Jambo jengine mageuzi katika masomo ya vyuo vikuu, leo hii wengi ya wasio na ajira ni wahitimu wa vyuo vikuu nchini, mwanafunzi alisomeshwa darasani namna ya kufanya kazi kama muajiriwa lakini hakufundiswa namna ya kujiari, mwanafunzi anasoma chuo kwa miaka mitatu akimaliza mitaani hajui afanye lilpi, tukianglia vijana wengi waloishia kidato cha nne ndio walojiari na kuendlea na maisha yao tofauti na walohitimu vyuoni, sasa ipo wapi faida ya kusoma?

Jambo jengine twende na wakati, kwa sasa kuna vijana wengi sana hawana ajira walohitimu vyuo vikuu, hivyo serikali isitishe udahili wa wanafuzi vyuo vikuu mana tunaendelea kukusanya wasomi waso na faida kila miaka na hakuna kozi mpya zinazofundiswa madala yake tu tufungue vyuo vya ufundi na uzalishaji ili tupunguze tatizo la ukosefu wa ajira nchini kila mwaka. Mwisho kabisa Lazima tubadilishe mifumo ya Elimu ili tulete mageuzi nchini.

Tuziangalie upya Sera na mifumo ya Elimu na tueke zinazoenda na wakati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom