sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Nimeguswa sana na tukio la ajali huko Manyara,tumepoteza watoto,ndugu,jamaa na Watanzania wenzetu,Allah awarehemu wote waliotangulia mbele za haki na awanyie wepesi majeruhi waliolazwa hospitalini amen.
Ajali ni ajali na haina kinga,lakini ni muhimu kujua chanzo cha ajali hiyo iliyopelekea kuangamiza watoto wale na walimu wao,lakini ni wakati sasa kwa jeshi letu la polisi kupitia kitengo chake cha usalama barabarani kujikita zaidi kwenye usalama wa vyombo vya usafiri kuliko kuligeuza jeshi hilo chanzo cha mapato.
Imekuwa ni desturi madereva kupigwa notification ya shilingi 30,000/- bila hata kukaguliwa kwa umakini kama gari hilo lina matatizo zaidi ya kosa alilofanya dereva na kupelekea dereva kuachiwa kuendelea na safari bila kujali usalama wa chombo chenyewe.
Bila kubadili mfumo wa ukaguzi wa vyombo vya usafiri kwa kutumia zana za kisasa(diagnosis ) tutaendelea kupoteza wapendwa wetu siku hadi siku, hakuna budi sasa kwa jeshi letu kupatiwa vyombo vya kitaalamu vya uchunguzi wa matatizo ya magari kwa usalama wa abiria na chombo chenyewe.
Kujikita zaidi kwenye kukusanya pesa za adhabu ya makosa(penalty notification) hakuleti tija kwa taifa zaidi ya kujenga utamaduni wa kulimbikiza ubovu wa vyombo hivyo na kusababisha majanga ya ajali.
Tumezoea kukimbilia kwenye sababu moja tu ya mwendo kasi bila kujali uimara wa magari yenyewe. Tukiweza kuyakagua magari haya na matokeo yakaonekana kuna hitilafu yapaswa mbali na kulipia faini abiria washushwe na gari kupelekwa gereji kwa matengenezo,kisha lirudi kukaguliwa tena ndiyo liruhusiwe kupakia abiria tena.
Pia kuna haja ya kubadilishana uzoefu na wenzetu ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kuzuia ajali zinazopoteza nguvu kazi ya taifa. Tujifunze kutoka kwao,huenda ikasaidia kupunguza tatizo hili kwa kina.