Tuanzisheni kampeni ya kususa miamala kukabiliana na tozo

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,877
Hii nchi inaendeshwa kama mtu anayetembea kama amekatwa kichwa

Serikali ni uwakilishi wa wananchi! Na wananchi wanaamua kusalimisha uhuru wao na nguvu zao wanampa mtu au kikundi cha watu kisimame kwa niaba yao.

Mnamove kutoka state of nature na kuwa na kitu kinaitwa "social contract" ambapo ni makubaliano ya kukubali mtu flan au kikundi kiongoze kwa niaba ya wananchi wote.

Sasa hizi tozo asilimia 99.999 ya wananchi wanazipinga wewe kiongozi ni nani upingane na wananchi ambao wamekutuma?

Tuanzisheni kampeni ya kususia miamala naam tuanzisheni hii kampeni ya kususia miamala maana hii serikali haisikilizi kero za wananchi na malalamiko badala yake wanaziita kelele.

Kwanini kiongozi unakosa uchungu na wananchi?

Tuanze mgomo wa kimataifa wa kususia Tozo na makato na ianze tarehe 1 September

Wakuu tupeane mawazo ya kuanza kuanza kampeni ya kususia miamala ya simu yote kama hatua ya kupinga tozo

Tena ianze rasmi tarehe 1 September hizi siku tulizonazo ziwe ni za kuhamasishana kila mahali mtandaoni ili tuanze mwamko wa kupinga tozo kwa nguvu zote

Lengo ni kuanza mgomo na ususiaji wa miamala ya simu ifikapo tarehe 1 September ambapo tutaendelea hadi serikali isalimu amri

Najua kiwango cha miamala kikishuka lazima watasurrender tu ukicheka na nyani utavuna mabua wachaga wanasemaga "ukicheka na mjinga atakupasua jicho" tusiache serikali ya huyu ssh itupande kichwani

Huyu mama hawezi kubadilika na atazidi kutunyonya tu, amini nawaambia hana uchungu na sisi hapa, maana wenyewe mnajua hilo

Wakuu tupeane mawazo ili tuanze kampeni hii ya kitaifa!!
 
Umesema kuwa serikali ni uwakilishi wa wananchi!

Pole kama bado una wazo hilo, kama ina mawazo kuwa mbunge anayekuwakilisha bungeni ni kweli yupo kwa ajili yako basi hata hii miamala wewe pia ulishiriki kutunga sheria kuisaidia serikali yako kupata mapato, Sheria ilianzia bungeni kwa mwakilishi wako ikajadiliwa na kupitishwa na rais wako uliyemchagua akasaini kwa ajili yako, vumilia mkuu hakuna kugoma na haifutiki, uli mind acha kutumia huduma hizo kwani lazima?

Vile vile hiyo sio changamoto kwa sasa, changamoto iliyopo kama wananchi ni kupambana namna gani wakubwa hawa ambao wameruhusu tugongwe chanjo ya lazima japo unaambiwa ni hiari.

Je utaweza kuishi bila chanjo? Maana kukataa chanjo ni kuzikosa huduma za msingi ikiwemo kutumia Cash money..lazima uwe na chanjo ndo upate huduma yoyote kwenye ofisi za serikali na kupanda usafiri wa umma. Wenzetu Wafaransa kesho jumatatu restriction zinaanza kwa wale ambao hawana chanjo, hakuna kuingia kula kwenye migahawa, wala kupanda Usafiri wa umma.

Najiuliza bongo watatubana kwenye nini sijui kama hutakuwa na chanjo, usisahau serikali yako inataka waliochanjwa wote watakuwa na electronic passport ku cross anywhere kupata huduma.
 
Kabisa
 
Tuanze mgomo wa kimataifa wa kususia Tozo na makato na ianze tarehe 1 September

Wakuu tupeane mawazo ya kuanza kuanza kampeni ya kususia miamala ya simu yote kama hatua ya kupinga tozo

Tena ianze rasmi tarehe 1 September hizi siku tulizonazo ziwe ni za kuhamasishana kila mahali mtandaoni ili tuanze mwamko wa kupinga tozo kwa nguvu zote

Lengo ni kuanza mgomo na ususiaji wa miamala ya simu ifikapo tarehe 1 September ambapo tutaendelea hadi serikali isalimu amri

Najua kiwango cha miamala kikishuka lazima watasurrender tu ukicheka na nyani utavuna mabua wachaga wanasemaga "ukicheka na mjinga atakupasua jicho" tusiache serikali ya huyu ssh itupande kichwani

Huyu mama hawezi kubadilika na atazidi kutunyonya tu, amini nawaambia hana uchungu na sisi hapa, maana wenyewe mnajua hilo

Wakuu tupeane mawazo ili tuanze kampeni hii ya kitaifa!!...
 
Sisi hatuwezi kugomea maana sisi wanaccm tozo hatukatwi Wala Petrol hazitugusi,wanaoguswa na Makati na upandaji wa bidhaa ni upinzani hasa Chadema.

Sisi wanyonge tozo zinatuogopa!
 
Hata mfanyeje hamna uwezo wa kubadili chochote, mmeshaambiwa kama tozo za miamala ni ishu kwenu hamieni Burundi.
 
Sisi hatuwezi kugomea maana sisi wanaccm tozo hatukatwi Wala Petrol hazitugusi,wanaoguswa na Makati na upandaji wa bidhaa ni upinzani hasa Chadema.

Sisi wanyonge tozo zinatuogopa!
Watz wachache wajanja tuhamieni ccm tuitafune nchi vizuri.
 
Kweli mkuu tuangalie namna ya kupunguza matumizi ya mobilemoney ili hawa makubwa jinga yasije yakanogewa
 
Wala haihitaji Kampeni.
Watu wengi sana ninaofahamiana wameacha kufanya miamala ya simu, ile ya lazima sana ndiyo mtu anajikuta anafanya
 
Tuendelee kususia
JamiiForums560600929.jpg
 
Back
Top Bottom