Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Rais ana bifu na Waziri mkuu wake na anataka kumtimua kazi.Ili kujitoa lawamani,anamwambia Waziri mkuu;nimekuandalia barua hizi mbili;moja imeandikwa ndani'YOU WILL STAY' na nyingine imeandikwa 'YOU ARE FIRED'.Hatma yako ya uongozi itatokana na bahati nasibu katika kuchagua mojawapo ya barua hizi mbili.Kabla ya kwenda kuchagua barua mojawapo,spy mmoja anamvuta waziri mkuu kando anamwambia kwamba Rais ana bifu na wewe hivyo zile barua zote mbili zimeandikwa 'YOU ARE FIRED'.Swali;kama wewe ndo WAZIRI MKUU utafanyaje ili usipoteze kazi yako?HINT;ni lazima uchague barua moja kati ya mbili ulizotengewa.