Tuanze kwa dr.harrison mwakyembe, na twende mbele zaidi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuanze kwa dr.harrison mwakyembe, na twende mbele zaidi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Jul 10, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni mwa mwaka 2011 Mh.Mwakyembe alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuna watu wanataka kumuua. Lakini hakuishia alimtaja na Dr. Slaa kama miongoni mwa watu wachache ambao walikuwa kwenye kundi hilo. Vilevile itakumbukwa kwamba Dr. Slaa alipokuwa Mbunge alikuta vinasa sauti ndani ya chumba chake alichofikia kwenye hoteli ya 56. Mpaka leo hatujui malengo ya kumwekea vipaza sauti yalikuwa ni nini na nani amehusika?

  Wapo watu wanaodhani kwamba Dr.Slaa anatafuta umaarufu bila kuhusisha vichwa vyao kufikiri. Kwa hoja ya umarufu je wanaamini kwamba Dr. Mwakyembe alikuwa anamtafutia umaarufu Dr.Slaa? Uhai wa mtu unathamani kuliko CCM, CDM, CUF n.k. na ni haki ya kimsingi kwa kila raia wa nchi yetu ya Tanzania. Lazima tutambue Lema, Mnyika n.k. ni political figures ambao wanapata coverage kubwa, hivyo tatizo lisiwe kwasababu ni viongozi wa CDM bali tatizo ni hatarisho la UHAI wao.

  Kama ni ushahidi basi Dr. Mwakyembe ameukalia, na tuanze hapa. Kupotosha wajibu wetu ya kufikiri ni kulundika upumbavu ndani ya fikra zetu na kupotosha wajibu wa kibinadamu wa kufikiri kwa bidii. Kama ni UZUSHI tupinge kwa HOJA pevu na si HOJA nyepesinyepesi.
   
 2. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu hawa wabishi wasiotaka kuona ukweli kina Dr Nchimbi sehemu yao ni The Hague inawasubiria sijui hawaoni wenzao wanapelekwa wapi????

   
Loading...