Tuanze kutabiri "visingizio" vya kushindwa kwa sera ya viwanda ifikapo 2020

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Binafsi hupenda kutabiri au kueleza mtazamo wangu juu ya nini kinaweza kutokea hapo baadae based on what is happening now.

Kwa msingi huo huo,naona kuna viashiria vyote vya sera hii kufeli kwasababu ya siasa kutawala badala ya taalumu za watu kuachwa zifanye kazi na wanataalumu/wasomi kugeuka wanasiasa na kuweka kando taaluma zao.

Kabla ya mtu kuamua kuwekeza katika nchi yoyote ni lazima kwanza ajiridhishe kuwa akiwekeza katika nchi husika hata pata hasara na zaidi atarudisha hela aliyowekeza na pia atapata faida na pia biashara au uwekezaji wake utakuwa sustanaible.

Kwa kawaida mambo ya kuzingatia ni kama hali ya uchumi wa nchi husika, political stability, viwango vya kodi katika nchi husika,hali ya hewa, upatikanaji wa malighafi,soko la ndani na la nje,n.k kutegemeana na aina ya uwekezaji mtu anaotaka kuufanya. Wataalamu wanaelewa zaidi na wanaweza kutusaidia hapa.

Kwa nchi yetu factors nyingi ziko under control iwapo tutaacha siasa na tutakuwa serious na isitoshe nchi yetu imejaliwa kila kitu kuanzia hali nzuri ya hewa(hatuna extreme weather,n.k) ,maliasili mbalimbali na hata mito,mabonde na maziwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Pamoja na yote haya, sera hii ya viwanda bado inaweza kufeli tu kama tulivyofeli katika maeneo mengine ila wanasiasa wetu huwa hawakosa sababu za kujitetea wanaporudi kwa wananchi kuomba kura.

Kwa msingi huu,tutarajie sababu gani kutoka kwa wanasiasa iwapo kweli sera hii itatenda kufeli?

Mimi nataraji kusikia yafutayo:

1.Ukame
2.Mtikisiko wa uchumi duniani
3.Upotoshaji wa vyombo vya habari kuhusu hali ya uchumi wa nchi.
4.Tunahitaji muda zaidi hivyo tunaomba mtupe miaka mingene 5.

Unaweza kuoongeza kwenye hii list.
 
Hilo ndilo muwezalo,, kuiombea Serikali ishindwe!!!
Too low!!!
Mjomba mwaka umekatika hakuna hata kiwanda cha kufunga maji ya kandoro , sasa hilo nalo ni sisi tuliombea ?

Mipango ya kuleta viwanda si mdebwedo , kwa serikali kama hii inayofikiria kudhibiti chadema kila asubuhi haitoweza lolote , endelea kuwepo hapa na tutakukumbusha tena baada ya miaka hii mitano kwisha , kumbuka kwamba huyu aliyekuwepo sasa ndiye rais wa mwisho kabisa wa Tanzania kutokea ccm , na amebakisha miaka minne tu na si vinginevyo .
 
Hilo ndilo muwezalo,, kuiombea Serikali ishindwe!!!
Too low!!!
Ukisoma zaburi ya 109....kwa sababu umependa kulaani kuliko kubariki basi mabaya hayata kutoka kamwe . ..INATISHA HEBU TUANZE KUBARIKI ILI NA SISI TUBARIKIWE NA VIZAZI VYETU . .
 
Mjomba mwaka umekatika hakuna hata kiwanda cha kufunga maji ya kandoro , sasa hilo nalo ni sisi tuliombea ?

Mipango ya kuleta viwanda si mdebwedo , kwa serikali kama hii inayofikiria kudhibiti chadema kila asubuhi haitoweza lolote , endelea kuwepo hapa na tutakukumbusha tena baada ya miaka hii mitano kwisha , kumbuka kwamba huyu aliyekuwepo sasa ndiye rais wa mwisho kabisa wa Tanzania kutokea ccm , na amebakisha miaka minne tu na si vinginevyo .
Mwaka unaishi nguvu wamezielekeza kwenye uhakiki,kutumbua majipu na ku-deal na wapinzani alafu wanaimba sera ya viwanda.
 
mtakufa kwa presha. pitia wipkedia u-google air tanzania, tiyari magu kasha-order BOEING737 next gen. mtanyooka tu.
 
Mtoa Maada ni mchambuzi mzuri WA siasa zetu hasa mambo to kiuchumi aliyosema yupo sahihi japo Kuna WATU wanaona kama a Nafurahi SERIKALI kushindwa Ila wenye akili tunajua
 
mtakufa kwa presha. pitia wipkedia u-google air tanzania, tiyari magu kasha-order BOEING737 next gen. mtanyooka tu.
Kazi ni kununua ndege au kuendesha biashara ya ndege?Kwa madaraka aliyonayo kuna ugumu gani wa yeye kuagiza ndege kwa kodi zetu?Umsesikia Fast Jet wanafuta baadhi ya route?Jiulize ni kwanini.

Kununua ndege kwa kodi za wananchi sio sifa bali sifa ni kuendesha hiyo biashara kwa faida otherwise mwisho wa siku utaambulia aibu tu.
 
Tumeanza na michakato ya kuweka mazingira wezeshi na tumetafuta wawekezaji wenye mitaji mikubwa ambao wamesema wako tayari. Tumeshapima viwanja vyote ambapo uwekezaji utafanyika. Lakini pia tumefanyia marekebisho baadhi ya sheria. Kwa hiyo kazi iliyobaki ni ndogo. Tupeni kura tumalizie ujenzi
 
Na mpaka sasa tunakwenda vizuri alafu wanamalizia na ule msemo wao wa..........oyeeee!!!
 
  • Thanks
Reactions: Izc
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom