Tuanze kuijenga Chadema

Uncle Rukus

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
2,415
398
Kutokana na kukubalika kwa Dr.Slaa na sera za chama chetu, Wazee wa Mbezi Juu tukishirikiana na vijana tuna jenga tawi la chama chetu.. Pia tutachukua kadi za uanachama wa wa Chadema. Tunategemea kumwalika Dr.Slaa kuja kulizindua.
 
Kila la heri wakuu na mjiandae na uchaguzi wa serikali za mitaa kabisa maana itabidi muanzie hapo ili kuwa na uhakika zaidi 2015
 
Siyo mbezi tu Mkuu Muga, nawashauri vijana wote bongo nzima waanze kazi ya kujenga chama chetu kwa kufungua matawi na kuwaelimisha watu juu ya umuhimu wa mabadiliko!
 
Kila la heri wakuu na mjiandae na uchaguzi wa serikali za mitaa kabisa maana itabidi muanzie hapo ili kuwa na uhakika zaidi 2015
Kazi njema na mbarikiwe na kupanda mbegu ya ushindani madhubuti katika nchi yetu. CCM lazima iondoke madarakani!
 
Kwanza, Uongozi wa Chadema inabidi uwe na sura za hali halisi ya WTZ. Bado ninashaka na structure ya uongozi ndani ya Chadema.
 
Sisi pia tumejiandaa kufungua tawi letu mtaani,tunaanza kuwabana ccm mapemaa,serikali za mitaa lazima tuwabane sana na tuwe na wanachama watiifu kama 7M hivi. Ccm wamekuwa wakitamba kuwa tayari wana kura 5M za wanachama wao lakini imebidi waibe kufikisha idadi hiyo. Hapa ni pazuri sana kujenga chadema,tuwapige KO
 
Kutokana na kukubalika kwa Dr.Slaa na sera za chama chetu, Wazee wa Mbezi Juu tukishirikiana na vijana tuna jenga tawi la chama chetu.. Pia tutachukua kadi za uanachama wa wa Chadema. Tunategemea kumwalika Dr.Slaa kuja kulizindua.

Mkuu Mganyizi, nakupa pongezi zangu kwa hii thread yako mkuu. Kama kuna lolote linalowezekana kufanywa na Chadema ni kufungua matawi nchi nzima mijini na vijijini, najua bado kuna mambo mengi ya kufanya lakini kama tutaweza kufanikiwa kwa asilimia kama 60 tu, basi 2015 ccm wakae mkao wa kung'oka hata kwa mbinu chafu.

Tuendelee kufikisha haya maoni yenu kwa viongozi wa juu ili wayafanyie kazi. Mapambano yanaendelea hakuna kulala ndo sifa ya wapiganaji siku zote huwa hawarudi nyuma, ni kupanga plans nyingi za kutosha.
 
Tukitaka mabadiliko lazima tuyagharamie. Fedha, muda na hata usumbufu kutoka kwa uongozi wa kifisadi ikiwepo hata kukamatwa ni gharama ambazo lazima tuwe tayari kuzitoa. Tufungue matawi na tuwe tayari kuchangia CHADEMA kuanzia sasa kifedha.
 
Wakazi wengi wa Mbezi juu ni wapenzi wa Chadema, wengi wetu tunataka kuondokana na upenzi kwenda kwenye ngazi ya kuwa wanachama wa kudumu ili kukipa chama chetu nguvu zaidi... Cha kufurahisha ni kwamba Wazee wengi wa Mbezi Juu wanaunga mkono chadema, tofauti na maeneo mengine amboko chadema inakubalika na vijana pekee... Nadhani sasa umefika muda watu wenye mapenzi mame na chama chetu kufanya vitu kama hivi ili kuweza kuweka mizizi kuanzia ngazi ya chini kabisa.
 
Mkuu Mganyizi, nakupa pongezi zangu kwa hii thread yako mkuu. Kama kuna lolote linalowezekana kufanywa na Chadema ni kufungua matawi nchi nzima mijini na vijijini, najua bado kuna mambo mengi ya kufanya lakini kama tutaweza kufanikiwa kwa asilimia kama 60 tu, basi 2015 ccm wakae mkao wa kung'oka hata kwa mbinu chafu.

Tuendelee kufikisha haya maoni yenu kwa viongozi wa juu ili wayafanyie kazi. Mapambano yanaendelea hakuna kulala ndo sifa ya wapiganaji siku zote huwa hawarudi nyuma, ni kupanga plans nyingi za kutosha.

Mkuu, Pole sana kwa Ban... Tuko pamoja kwenye ujenzi wa kukijenga chama, huu siiwakati wa kukaa na kuanza kulaumiana bali ni muda wa kurudi nyuma na kukipanga kikosi chetu vizuri.
 
nice thread. wapi wanafundisha elimu ya uraia. maana tukifungua matawi halafu hatuna elimu ya uraia tutaambiwa vijiwe sasa na si matawi.
 
Good strategy ngoja nikachukue kadi yangu ya uanachama fasta.....
nasi huku namanyere tuko pamoja kaka pipooooozzzz pawa daima
 
Mbinu rahisi yakupata wafuasi,undeni makanisa kibao lakini nyanda za juu..ila sehemu za Coast mmefulia,vip mteueni Slaa awe mkuu wa makanisa maana hata kujijenga bado,Habari zinazochipuka ni kwamba Slaa anajuta kuliacha KANISA,MMH ETI TZ KWA YESU,SIRAHISI HATA KIDOGO
 
Hili ni la muhimu sana, asante kwa hoja hiyo. Kila mpenda Tz anataka CHADEMA kikomae kisawasawa ili kuwepo upinzani makini nchini kwa manufaa ya waTz wote. Huyu ndugu hapa juu (Ibnabdilahi) anasumbuliwa tu na udini, hajui kuwa sisi tunatafuta maslahi ya nchi. Hawa ndio wale waliosikika wakisema kipindi cha kampeni misikitini na kwa sms kuwa eti "waislamu safari hii tumchague mwislamu mwenzetu Kikwete, na 2015 Lipumba, tusikubali kutawaliwa na Padri." Hayo ni mawazo finyu sana. Udini hauna nafasi kwenye bongo zilizopanuka, na wanamapinduzi wa kweli hawaiungi mkono CHADEMA kwa misingi ya dini hata kidogo.

Heko wanambezi, lakini haitoshi Mbezi wala Dar pekee, matawi yafunguliwe nchi nzima, tena haraka iwezekanavyo. Tujiandae kuchukua mitaa na kuishikilia. Aluta continua.
 
Heko wanambezi, lakini haitoshi Mbezi wala Dar pekee, matawi yafunguliwe nchi nzima, tena haraka iwezekanavyo. Tujiandae kuchukua mitaa na kuishikilia. Aluta continua.

Hii tumeanza tu kwa mbezi, mtandao wa Chadema ni mkubwa sana na hatimaye utasambaa nchi nzima, uzuri ni kwamba wanachadema wengi ni tatu walio elimika na tunafanya mambo yetu kwa umakini wa hali ya juu...
 
Haya Shime watanzania, fungueni matawi, wao wafungue mashina... Ukiagalia hoja za mtandaoni waweza kuona kweli watanzania wapo tayari kalini....kiukweli hamjawa tayari:smile-big:

Pana mambo mengi yanahitajika kabla ya hayo,
wengi walifungua matawi na leo hii yamechakaa,
wengi wamebakia kusema ile ofisi yetu hakuna hata kifaa kimoja,
bila kubadilika nafsi na kuwa na malengo ni bure tu,
itakuwa kujisumbua kusiko maana na kupotoa watu ukichanganya na kupoteza nguvukazi za taifa:tape:
 
Back
Top Bottom